A Kafkaesque kerfuffle.Habari hii inahusu tukio la hivi karibuni mnamo Aprili 2026 nchini India, ambapo mwanaume mmoja anayejulikana kama Jitu Munda alilazimika kuchukua hatua kali ili kupata haki yake kutoka kwa benki.
Munda alikuwa akijaribu kutoa fedha kutoka kwenye akaunti ya marehemu dada yake aliyefariki miaka kadhaa iliyopita. Licha ya kufika benki mara nyingi, maafisa wa benki walikataa kumpa fedha hizo wakidai anahitaji kutoa uthibitisho zaidi wa kifo chake.
Kutokana na kukatishwa tamaa na urasimu wa benki, Munda aliamua kufukua kaburi la dada yake, kutoa mifupa (mabaki) yake, na kuipeleka hadi kwenye mlango wa benki hiyo ili kuwathibitishia kuwa dada yake amefariki kweli.
Video ya tukio hilo ilisambaa sana mitandaoni (viral) na kuzua mjadala mkubwa kuhusu changamoto wanazopata wananchi vijijini wanapojaribu kupata huduma za kibenki. Baada ya shinikizo hilo na hasira ya umma, benki hiyo ilichukua hatua na kumlipa Munda fedha hizo nyumbani kwake.
Hata hapa bongo ndugu yako akifa na huna no.yake ya Siri ni huzuni!Asingekomaa hiyo pesa ingepotea.. Imagine ni wangapi wanapigwa kwa style hii
Ahsante kwa mungozo Bank Manager...Utaratibu wa kupatikana kwa fedha za marehemu kama alikuwa ana akaunti benki
kuna taasisi zinazohusika kufikisha bakaa ya marehemu kwa wahusika mfano mahkama kuu, claimers wanatakiwa wapeleke kitambulisho cha muhusika, kadi ya bank, cheti cha kifo na minutes za kikao cha familia kilichomteua mmoja katika ndugu wa marehemu. Baada ya hapo mahkama inapeleka barua bank kuomba akaunti ifungwe na haki za wahusika zinawafikia wenyewe. Kwenda tu benk na kudai kama mwenye akaunti amefariki na alikuwa ni dada yako bila uthibitisho benk haiwezi kukupatia hio pesa. Sasa kwenda na mifupa au mabaki ya marehemu sidhani kama ni uthibitisho, coz maiti imeshakuwa mifupa nani amethibitisha kama huyo ndie mwenyewe
Na vilevile kwenda mtu mmoja tu bank kutaka kutoa bakaa ya marehemu jee anakuwa mtu sahihi, jee kama anataka kuwadhulumu wahusika wengine?
Ni kutokujua taratibu tu ndio maana watu wanadhulumika
Ha ha haaaaa, mambo mengine huwaga yana muongozo, sio kama mapenzi 🤣Ahsante kwa mungozo Bank Manager...
Mimi nianyo miongozo ya mapenzi...Ha ha haaaaa, mambo mengine huwaga yana muongozo, sio kama mapenzi 🤣