Kampuni ya udalali ya Legit Auctin Mart ya Dar es Salaam imetangaza mnada wa kuuza basi la kampuni ya Kilimanjaro Express kwa amri ya mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam.
Kutangazwa kuuzwa kwa basi hilo kutokana na kampuni la Kilimanjaro kushindwa kulipa deni la shilingi milioni mia tatu (300,000,000.00) kama walivyoamriwa na mahakama hiyo kutokana na madai yaliyofunguliwa hapo na ndugu Leonard Kisenha.
Katika madai hayo, ndugu Kisenha aliiomba mahakama hiyo iiamru kampuni ya Kilimanjaro kumlipa fidia kutokana na mojawapo ya basi la kampuni hiyo kusababisha ajali iliyopelekea kifo cha binti yake Immaculate Kisenha (16), aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya sekondari Merriwa. Kutokana na basi lililosababisha ajali hiyo kutokuwa na bima, na kampuni hiyo kutokufanya chochote kuhusika na waathirika wa ajali hiyo, ndugu Kisenha ililazimika kufungua shauri la madai dhidi ya kampuni hiyo, mkurugenzi wake mkuu na dereva aliyekuwa akiendesha basi hilo.
Baada ya shauri hilo kusikilizwa, kampuni ya Kilimanjaro iliamriwa kulipa fidia ya shilingi milioni mia tatu, riba ya asilimia saba kwa ucheleweshaji wa malipo na gharama zote za kesi.
Basi la Kilimanjaro Express lilikamatwa kwa amri ya mahakama karibu wiki mbili zilizopita na sasa mahakama hiyo imetoa amri liuzwe baada ya Kilimanjaro kushindwa kulipa kiasi wanachodaiwa.
Mnada wa kuuza basi hilo utafanyika siku ya Ijumaa, tarehe 5/7/2024 saa 4 asubuhi kwenye yard ya Legit huko Mikocheni B.