Hatimaye Erick Shigongo Atajiunga na chuo mwaka huu

HERUFI KUBWA

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2017
Posts
388
Reaction score
602
Mjasiriamali na Mtunzi wa vitabu mashuhuri nchini Tanzania, Erick James Shigongo anatarajia kurudi shule na kusoma elimu ya shahada baada ya kuhangaika muda mrefu kutafuta nafasi hiyo, huku akisukumwa na masimango na matusi ya mitandaoni.

Eric Shigongo

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Erick Shigongo ameandika waraka mrefu akielezea safari yake kitaaluma na furaha aliyonayo, ya kuweza kufikia ndoto yake ya kuwa na elimu ya chuo kikuu, licha ya kuwa na mafanikio makubwa kwenye kazi zake za utunzi na maisha kiujumla.

“Ndoto imetimia, hatimaye naingia Chuo Kikuu, nikiwa mtoto nilitamani sana kusoma hadi chuo kikuu lakini sababu ya umasikini na mazingira magumu hasa shule nilizosoma, sikufaulu mtihani wa darasa la saba, nikarudia darasa la saba katika shule nyingine lakini bado sikufaulu, nilijiona mjinga! Nikajaribu kupitia njia ya ‘vikozi’ vidogo ili hatimaye niingie chuo kikuu lakini sikufanikiwa, nikaachana na ndoto hiyo na kuanza ujasiriamali”, ameandika Erick Shigongo.

Erick Shigongo alendelea kuandika akisema kuwa ndoto yake hiyo imefanikiwa baada ya kujiunga na mfumo wa RPL ambao hufanya watu wenye uzoefu fulani katika jamii bila kuwa na elimu, na kuwapa nafasi ya kusoma elimu ya juu, ndipo alifanikiwa kupata nafasi mwaka huu, baada ya kufeli mwaka jana.

“Nikakusanya vitabu vyangu ambavyo nimekwishaandika na kuvipeleke Tume ya Vyuo Vikuu na kuomba niruhusiwe kufanya mtihani huo, nikaruhusiwa, mwaka jana nikafanya na kufeli, sikukata tamaa, mwaka huu nikafanya tena na kufaulu, hivyo mwezi wa tisa ninaanza mwaka wa kwanza “, ameandika Erick Shigongo.

Chanzo: Bongo5
 
Kumbe alikuwa hajasoma .
Kusoma sio kumaliza kila kitu, ila akili za ziada zinasaidia.
Nakumbuka Kuna jaamaa mmoja aliwahi kusema hivi.
"mimi sijasoma, nina nyumba nzuri, maisha mazuri, na chochote ninachokitaka napata."
Nashangaa Yeye kasoma lakini Hana maisha mazuri "alikuwa akimsema mtu.
 
Watu wanaopiga uo mtihan ujue vyeti hawana km wanavyo ni miswaki imepangana

Afu kwenda kusoma kwa majasiriamali mkubwa km yy ni kupoteza pesa tu

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
Sio kweli mkuu ishi kwa kiu na uchu kutoka moyoni
 
Wapiga dili

Sent from my iPhone6 using JamiiForums mobile app
 
Mjasiriamali na Mtunzi wa vitabu mashuhuri nchini Tanzania, Erick James Shigongo anatarajia kurudi shule na kusoma elimu ya shahada baada ya kuhangaika muda mrefu kutafuta nafasi hiyo, huku akisukumwa na masimango na matusi ya mitandaoni.

Eric Shigongo

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Erick Shigongo ameandika waraka mrefu akielezea safari yake kitaaluma na furaha aliyonayo, ya kuweza kufikia ndoto yake ya kuwa na elimu ya chuo kikuu, licha ya kuwa na mafanikio makubwa kwenye kazi zake za utunzi na maisha kiujumla.

“Ndoto imetimia, hatimaye naingia Chuo Kikuu, nikiwa mtoto nilitamani sana kusoma hadi chuo kikuu lakini sababu ya umasikini na mazingira magumu hasa shule nilizosoma, sikufaulu mtihani wa darasa la saba, nikarudia darasa la saba katika shule nyingine lakini bado sikufaulu, nilijiona mjinga! Nikajaribu kupitia njia ya ‘vikozi’ vidogo ili hatimaye niingie chuo kikuu lakini sikufanikiwa, nikaachana na ndoto hiyo na kuanza ujasiriamali”, ameandika Erick Shigongo.

Erick Shigongo alendelea kuandika akisema kuwa ndoto yake hiyo imefanikiwa baada ya kujiunga na mfumo wa RPL ambao hufanya watu wenye uzoefu fulani katika jamii bila kuwa na elimu, na kuwapa nafasi ya kusoma elimu ya juu, ndipo alifanikiwa kupata nafasi mwaka huu, baada ya kufeli mwaka jana.

“Nikakusanya vitabu vyangu ambavyo nimekwishaandika na kuvipeleke Tume ya Vyuo Vikuu na kuomba niruhusiwe kufanya mtihani huo, nikaruhusiwa, mwaka jana nikafanya na kufeli, sikukata tamaa, mwaka huu nikafanya tena na kufaulu, hivyo mwezi wa tisa ninaanza mwaka wa kwanza “, ameandika Erick Shigongo.

Chanzo: Bongo5
 
Attachments

  • upload_2017-8-14_8-45-57.jpeg
    13.3 KB · Views: 84
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…