Hatimaye Libya yawa shamba la Bibi, officially

Je kwa Tanzania hali ikoje? kwamba inaweza kutokea watanzania kuchochewa kufanya machafuko?
 
Muammar Gaddaf alistahili yale yaliyo mkuta, na kila mtu anakula chumo la mikono yake na Qiyama kila nafsi itahesabiwa na kupewa haki ha haitadhulumiwa nafsi yoyote hata kiwango cha chembe ya Khardali.

Mola aliye juu atusamehe.
 
Mkataa pema, pabaya panamwita!
 
Kila ikikaribia uchaguzi mkuu tz mnaleta hizi adithi, aacha vitisho, ugaganizi wake wa madaraka ndio uliifikisha nchi hapo, kwa maana nyingine watawala ndio waalibifu wa nchi wanazotawala wanajisahau mno.
 
Yote haya naayajua kama ni ceremonial leader unahisi yeye pekee ndio anasifa zote zakua hapo alipo zaidi ya miaka 40 kuliko raia wote wa UK zaidi ya 50M ?!
Swali halijajibiwa hili.

Maana kama ujerumani ceremonial leader ni rais, na uchaguzi unafanyika kila baada ya miaka mitano,

Wagombea kibao wa binafsi na wavyama wanashiriki kugombania urais, Mfano mwaka 2017 wagombea walikuwa watano.

Mwaka 1960 northern ireland ilitaka kujitenga kwenye ufalme hasa wakatoriki ambao ndio wengi, baadae jeshi la uingereza lililo chini ya malkia likapelekwa na vita vikaisha 1998.

Sasa kama hali kama hiyo ufalme una tofauti gani na gadafi.
 
Swali langu hawataki kulijibu wanasahau hata ISRAEL kuna rais ceremonial leader na kuna waziri MKUU ambae ndio anaisimamia nakuiendesha nchi ila Kunakua nauchaguzi wakumpata rais kila baada yamiaka fulani ila ukiwauliza kuhusu MALKIA wanakupiga chenga

MALKIA ni DIKTEITA tu Kama hao MADIKTEITA wengine.....
 
uchochezi huu, picha za baad aya dadafi zimepigwa uswazi mbona.

anyway gadaffi ndio kafanya nchi iwe hapo alipo, alitaka kujifanya mfalme
 
Uingereza ni Monarchy, haiongozwi na rais bali Mfalme au Malkia ambaye ndiye Monarch.

Constitutional Monarchy kama ilivyo Uingereza ni mfumo wa utawala wa Kifalme wenye kusimamiwa na bunge. Kila kinachofanyika ndani ya uwezo wa kiti cha Ufalme kilikwisha kuidhinishwa na bunge hapo zamani. Muda wa kukitumikia kiti hicho kama Monarch (Head of State) ulikwisha idhinishwa na bunge.

Kuna mataifa kama vile Ufaransa ambayo ilikuwa nchi ya Kifalme hapo kabla lakini Ufalme wake ukaanguka. Kwa upande wa Uingereza, bunge la Uingereza ndilo lililouweka Ufalme wa Uingereza mpaka sasa baada ya vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe. Kama ni suala la kuufuta huo Ufalme lingekuwa limekwisha fanyika muda mrefu.

Majeshi yanaapa kwa Head of State, hiyo ni formality ya Constitutional Monarchy. Linapokuja suala la majeshi kuingia ama kwenda vitani au katika operesheni mbalimbali za kijeshi za kimataifa ni suala la kibunge chini ya Waziri Mkuu ambaye ndiye mkuu wa serikali ya Uingereza.

Waziri Mkuu pia hafanyi maamuzi binafsi. Maamuzi yake kuhusiana na suala la majeshi na vita hutokana na bunge la serikali anayoiongoza. Waziri Mkuu sambamba na Wizara ya Ulinzi yenye dhamana ya kuyasimamia majeshi ya Uingereza hufanya maamuzi kutokana na kura za wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi.

Malkia kama Head of State hatoi amri kwa majeshi kama atakavyo yeye. Bunge ndilo linaloshauri kiti (Crown) kupeleka majeshi vitani na si vinginevyo. As a formality, Malkia ana approve. Kinyume na hapo ni kusababisha mgogoro wa kikatiba ambao utapelekea kutokea kwa yale yaliyoikumba Uingereza zamani sana kipindi cha King John na Mfalme Charles wa kwanza.

Huo ndio utofauti wenyewe na isitoshe swali hili nilikwisha kulijibu hapo awali humu humu jukwaani, labda kama kuna swali la nyongeza.
 
Who is a dictator? What is a dictator?
 
Arab League wametulia kimyaaa
 
Wa Tz bora tuendelee kunekana mazezeta na CCM yetu potelea mbal
Tanzania chini ya CCM ni tofauti na ilivyokuwa
Libya. Ukifuatilia figure za GDp tu utaona utofauti.
Watu walikuwa na maisha mazuri hela ziko hata kama unakosa kazi ila uhakika wa kuishi comfortable ulikuwepo.

Shida ni mamluki waliopandikizwa kuja kujaza chuki raia kwa kuwahadaa kuwa life was more better than that in case wakiwa na demokrasia ya kuchagua na kuondoa raisi.
 
Ndo wakome,na bado hiyo ni trailer tu.waliyataka wasilie wavumilie tu ,nawapambane na Hali zao.
 
UK napo ni afrika?
muhanga wew
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…