Hatimaye Manchester United yaona mwezi, yashinda 2-0 katika Premier League

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Baada ya kuwa na matokeo mabaya hivi karibuni ikiwemo kufungwa na kupata sare, Manchester United imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Brighton katika mchezo wa Premier League.

Mchezo huo uliochezwa usiku wa kuamkia leo Februari 16, 2022, mabao yamefungwa na Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa ana mechi zaidi ya sita hajafunga bao na Bruno Fernandez.

 
Mchezo huo, ukanikumbusha yale malalamiko ya kuongeza muda kabla ya kumalizika kwa mchezo.
Kuelekea dk ya 90, wakati huo Manutd wanaongoza goli moja, jamaa walikuwa wameongeza kasi ya kutaka kusawazisha. Zikaongezwa dk 5. Wapenzi wa MANUTD tukaona ni nyingi sana! Zimeisha hizo, refarii hapulizi filimbi ya kumaliza mchezo! Ikaingia dk ya 6 kuelekea ya 7,jamaa wanashambulia kwa nguvu kwenye lango la MANUTD. MAN wakaunasa mpira, na kupiga mbele, kuliko na wachezaji wachache wa Brighton, na kufanikiwa kupata bao la pili.
Hapo, tunakumbushwa kuwa, dakika za nyongeza, sio kwa ajili ya timu moja. Hao Brighton wangesawazisha ndani ya dk 5+ Ki-Tanzania, tungesema refarii aliongeza dk nyingi kuwabeba Brighton!
 
Mkuu uzi wa man u huujui? Matumizi yasiyofaa ya jf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…