Hatimaye Masogange amtaja aliye mtuma mzigo wa dawa za kulevya

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
HATIMAYE yule Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange' aliyepatikana na hatia ya kuingiza nchini Afrika Kusini malighafi haramu aina ya ephedrine, amemtaja mtu aliyemtuma mzigo huo kuwa ni Mkongomani, Risasi Jumamosi limedondokewa na ‘kismati'.Masogange aliamua kumwanika kigogo huyo huku akimtaja jina bila kuuma maneno.

TWENDE PAMOJA
Risasi:
Masogange tumekuita leo hapa kwa ajili ya mahojiano maalum. Tangu umerudi Bongo toka Afrika Kusini ulikokutwa na ule msala wako, naamini hujawahi kuzungumza na chombo chochote cha habari. Uongo, kweli?
Masogange: Kweli kabisa.
Risasi: Risasi linakukaribisha tuzungumze mambo muhimu, lakini kubwa kuliko yote, hebu mtaje mtu aliyekutuma kubeba ule unga ambao ulikamatwa nao Afrika Kusini.
Masogange: (akionesha sura ya umakini) kusema ule ukweli, ni…(anamtaja jina). Huyu bwana ndiye aliyeniponza kwa yote yale.
Risasi: (bila mshtuko baada ya kutajwa kwa jina hilo). Huyo mtu ni Mtanzania kweli?
Masogange: Hapana, ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ila anaishi Tanzania miaka nenda, miaka rudi.
Risasi: Sasa Masogange, huyu mtu ilikuwajekuwaje hadi akakutuma kupeleka mzigo ule Afrika Kusini, hapo pana utata kidogo.
Masogange: Wengi hawajui. Iko hivi, siku ile (Julai 5, 2013) mimi nilikuwa nasafiri kwenda Sauz kwa mambo yangu tu. Nilipofika pale Uwanja wa Ndege (Julius Nyerere International Airpot) nilimkuta huyo mtu.
Risasi: Naye akiwa anasafiri kwenda huko?
Masogange: Hapana. Yeye tunafahamiana kwa muda mrefu, aliponiona aliniuliza kama nakwenda Sauz, nikamwambia ndiyo. Akasema anaomba nimbebee mizigo yake ya sukari.
Nilimkatalia, lakini akasema kuna mtu atanipokea Uwanja wa Ndege (wa Kimataifa wa Oliver Tambo) uliopo (Kempton Park) Johannesburg.
Basi nilimkubalia, lakini…
Risasi: Subiri kwanza Masogange. Hapo una maana wewe kazi yako ilikuwa kubeba tu, baada ya kutua kule ungekutana na mwenye mzigo, Je, uliuangalia mzigo wenyewe kama kweli ni sukari?
Masogange: Ndiyo. Nilimwambia anifungulie nione kama kweli ni sukari, akafungua begi moja, nikachungulia na kuona kweli ni sukari nyeupe!
Nilimwambia kama anataka nimsaidie kuufikisha Afrika Kusini, apeleke mpaka kwenye ndege ili kunipunguzia kazi ya kubebabeba. Nikifika Sauz nitamtolea huyo mtu sukari yake.
Basi, akapeleka mpaka kwenye ndege, mimi nikapanda na safari ikaanza.
Risasi: Subiri kidogo Masogange. Wewe ulikamatwa na mtu anayedaiwa ni ndugu yako, Melisa Edward. Mbona humtaji?
Masogange: Oke, yule tulikuwa safari moja tu. Lakini yule Mkongomani anajuana na mimi.
Risasi: Oke, endelea.
Masogange:
Tulifika uwanja wa ndege salama. Nikashuka na yale mabegi nayo, lakini cha ajabu wakatokea askari na kutukamata.
Waliniuliza nimebeba nini? Nikawaambia sukari, wakasema siyo sukari, wakanitaka nilambe. Kulamba hivi, ndiyo nikajua kweli siyo sukari, tukawekwa chini ya ulinzi na kupelekwa kwenye vyombo vyao vya sheria kwa hatua zaidi.
Risasi: Pole sana. Kwa hiyo yule mtu ambaye angepokea mzigo kule Sauz ulimwona ulipotua uwanjwa wa ndege?
Masogange: Sikuwa namjua kwa sura, nilipewa mawasiliano yake tu. Kuna uwezekano alituona wakati tumekamatwa na polisi maana tulizungukwa na watu wengi.
Risasi: Unakumbuka yalikuwa mabegi mangapi ya hiyo ‘sukari'?
Masogange: Hata sikumbuki vizuri mimi, nilishachanganyikiwaga jamani, yalipita yale.


ANAYEMJUA MWAKYEMBE
Siku chache baada ya mlimbwende huyo kunaswa Sauz, Bongo, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe alimtaja kijana ajulikanaye kwa jina moja la Mangunga kwamba ndiye aliyedaiwa kuwa na video queen huyo ndani ya ndege kwenda Afrika Kusini.


Mwakyembe aliamuru kijana huyo asakwe na kukamatwa ili kujibu mashitaka ya kusafirisha madawa ya kulevya aina ya Methamphetamine kwa Tanzania huku Sauz ikisema ‘unga' huo ni ephedrine ambao si wa kulevywa bali ni malighafi haramu.
Nassoro.
Masogange na mwezake, Melisa walikamatwa Julai 5, mwaka jana kwenye uwanja huo wa ndege nchini humo wakiwa na madawa hayo yaliyokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi bilioni 6.8.
Kesi yake iliendeshwa na Mahakama Kuu ya Gauteng iliyopo Kempton Park nchini humo na alikutwa na hatia ambapo alihukumiwa kwenda jela miezi 32 au kulipa faini ya randi 30,000 (shilingi milioni 4.8). Masogange alilipa faini huku mwenzake, Melisa akiachiwa huru kukutwa hana hatia.


Source:GPL

Mfululizo wa kukamatwa, kesi, hukumu na kuachiwa huru kwa Agnes Masogange kwenye kesi ya Madawa ya kulevya
Masogange ajisalimisha mwenyewe Mahakama a Kisutu
Kupandishwa kizimbani na kusomewa shitaka
Yaliyojili wakati wa kesi ya Masogange
Masogange kupelekwa kwa Mkemia Mkuu
Kesi kusikilizwa
Tetesi za kuachiwa huru
Hukumu
 
Ndio Tz yetu hii, sina hakika kama alie mtuma ni mkongo man kweli! Alie tengeneza mpango asikamatwe uwanja wa ndege hapa bongo nae ni mkongo man? There is a long que que.
 
Hii story hata chizi hawezi kuamini. Hivi mimi najiuliza kuna mamia ya watanzania wamefungwa nje ya nchi. Inakuaje huyu ndio kina Nzowa na wenzake wakaenda S. A. kufanya nini? mbona wengine hawawafatilii? Hii nchi hii yangu macho.
 
Hii story hata chizi hawezi kuamini. Hivi mimi najiuliza kuna mamia ya watanzania wamefungwa nje ya nchi. Inakuaje huyu ndio kina Nzowa na wenzake wakaenda S. A. kufanya nini? mbona wengine hawawafatilii? Hii nchi hii yangu macho.

Umeongea jambo la ukweli sana
 
Hizi stori wabaki nazo huko huko GPL si huku JF.

eti Mkongoman.....
 
Umeongea jambo la ukweli sana

Unafikiri Money Stunna kweli yaani Watanzania hatujali kabisa. Hao walioenda ingekuwa nchi nyingine wangejiuzulu nafasi zao. Kwanza walitumia kodi zetu.
Pia Tanzania bado hatuna malord wa drugs kama Colombia au Mexico. Tungekuwa na dhamira hii nchi sembe tungeisikia tu.

Wanajulikana wote yaani wangepukutishwa wote. Kama hatutaki kuchafuliwa na sembe tupate Raisi atakayeahidi kudeal na vigogo wa sembe.
 
Ngumu kumesa kwahyo huyo mkongo alikuwa na sukari Airport akisubiri mtu ambebee ? Je wasingetokea mtu ambaye anamjua ingekuwaje? Asingeisafirisha? Changa la macho ilo masogange mwenzako huyu anatumia umbo lake kufanya u-model wewe kubeba unga.
 
Eti mzigo ulikuwa ni wa mkongo man......eti kakutwa tuu airport akapewa apeleke......eti alikuwa na mawasiliano ya atakayempokea...je mmemuuliza hayo mawasiliano yametumikaje kumkamata mpokeaji ? na mbona hamkumuuliza ni nini ilikuwa dhumuni la safari yake huko SA.

Nadhani naye alijua kwa kupeleka hiyo "bahasha" na stori yake...otherwise angetafuta mtu timamu (let say Jenerali Ulimwengu, Marin au...) na kuanza kueleza hayo mauzauza yake angeishia MOI kama sio icu.

Jack naye akirudi ningewashauri msimuhoji nyie, hebu tafuteni watu serious ili habari pia zifuatiliwe na watu serious, ila kama atasisitiza kuwa naye anafanya utani kama Aginesi...basi muitane woote...kina risasi, kiu, ijumaa n.k ili kwa pamoja mfurahie figa lake.

Mtu akikueleza upumbavu na wewe ukaamni basi nawe anakuona ni --------...kwa mtazamo huo....thanx mleta uzi na risasi yako kwa kuwa wakala wa upumbavu.
 
Mim nionavyo,magazeti na agnes wako ktk kusafisha safisha uchafu waliofanya drug dealers,ambao wanafahamika vizuri kwa watu.
Kwa upande mwingine ni kufifisha issue ya yule "punda" aliyekamatwa mashariki ya mbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…