Hatimaye Mazda wazindua EZ-6 Electric sedan!

Hatimaye Mazda wazindua EZ-6 Electric sedan!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Baada ya tetesi za muda mrefu, hatimaye Mazda wameamua kuzindua officially Mazda EZ-6 ambayo ni EV version ya Mazda 6/Atenza.
IMG_0040.jpeg

Kuonesha ubabe wake kwenye EV, Mazda aliamua kushirikiana na kampuni la Kichina la Changan katika kutengeneza hii chuma.
IMG_0041.jpeg

Itakuja na flavor mbili, either full Electric Vehicle au Range Extended EV.
IMG_0042.jpeg

Full EV yenyewe utakuja na 190 kW motor itakayokua nyuma, na utachagua battery ndogo 56 kWh au kubwa 68 kWh, ambazo zitakupa range ya kilometa 480 au 600. Hizi battery zinaweza fast charge kutoka 30% hadi 80% kwa dakika 15 tu.
IMG_0043.jpeg


REEV yenyewe itakua na 1.5L engine pamoja na 160 kW motor. Kumbuka hii engine ina act kama generator, na jumla inaweza kufika range ya kilometa 1300. Pia nayo ina fast charge option ambapo itajaza kutoka 30% hadi 80% kwa dakika 20 tu.
IMG_0044.jpeg

Kwa sasa pre-orders zimeanza China, kwa bei ya $23,000 hadi $28,000!
 
$28000/= siyo ghali sana.... Ila sasa kwa mazingira ya bongo itavumilia?


Tukomae na akina Prado, V8, Hillux nk tu
Sema mazingirs uchawi na miundombinu ila iyo REEV inafaa maana unaweza ukawa hauichaji.
 
Unasubiri mzee. Kufika 2030 unakuta zimejazana Beforward.
Kipindi hicho ndo itakuwa new model yetu.,...tupo nyuma kila sehemu mpaka mafundi wa kuendana na hii teknolojia. Tumezoea magari ambayo ni mechanical zaidi hata haya yanakuja sasa hivi tu unakuta ni shida

Power steering inaroga kidogo mpaka umpate mtu afanye fixing iwe laini ni kasheshe maana tumezoea power steering za hydralic
 
Back
Top Bottom