Hatimaye Msuva atua Rwanda kuiongezea nguvu Stars

Hatimaye Msuva atua Rwanda kuiongezea nguvu Stars

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
salehjembe.jpg

Baada ya kukwama jijini Dar es Salaam, hatimaye Msuva ameondoka kwenda Rwanda kuungana na kikosi cha Taifa Stars.

Stars iko jijini Kigali kuivaa Rwanda keshokutwa katika mechi ya kuwania kucheza michuano ya Chan. Katika mechi ya kwanza mjini Mwanza, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Awali, Msuva alipanga kwenda Rwanda, jana alifika hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JKIA), lakini baadaye alirejea nyumbani.

Lakini leo amefanikiwa kuondoka kwenda Rwanda kuongeza nguvu katika kikosi cha Stars.

“Kweli nimefanikiwa, nitaondoka leo jioni,” Msuva aliiambia SALEHJEMBE leo mchana.
 
Asante kwa taarifa na kila la heri Taifa stars huko Rwanda
 
Back
Top Bottom