Hatimaye nimerudi kwenye mshahara wangu wa laki 4 kwa mwezi


Hapa kipindi nateseka juani..sio haba ilikua ukitoka asbhi saa zingine unarudi na laki 3..enzi za kutafuta uhuru..lakini tutaache yaliopita tugange yajayo..saivi naisubiria laki 4 kivulini kwenye air condition na uhuru nnao sbb sinyanyaswi na huyu boss wangu..naingia saa mbili nakula chakula cha ofisni narudi saa kumi na moja nyumbani naenda gym narudi nyumbani..na kunawili nimeshaanza [emoji3][emoji3]…usinionee wivu kwa kufukua makaburi
 
kweli wabongo tunapenda utumwa, sasa huzo zinazozidi laki nne si unaziapta kwa ujasiliamali au wewe mwizi unamwibia mwajili wako
 
Hongera mkuu

Muhimu ni kwamba kila mtu afanye lililo bora kwake.

Mimi huniambii kitu kuhusu biashara, naanguka nainuka, naanguka tena nainuka, sikomi na sijawahi kukoma.

Kila unavyoanguka ndivyo unavyozidi kugundua ulikosea wapi.

Lakini pia biashara ni kama mtoto wa binadamu, lazima apakatwe, aanze kukaa, atambae, asimame, atembee, ukitaka kuruka hizi hatua hakuna siku utaona biashara ni chaguo sahihi
 
Siku ukitumbuliwa ndio utajua biashara ni muhimu.

Hata huko kwenye biashara sidhani kama uliweka nia kweli coz ulikuwa unajua hata ukibuma utarudi kazini
 
Pumzika huko huko biashara tuachie akina sie
 
Duh mwezi mzima unakaa unasubiri laki 4 na unasema??
 
Nakumbuka ulikuja kuomba ushauri hapa,Umefanya uamuzi sahihi
 
Kiulaiiini umekubali mwenyewe......!
 
😂😂😂
 
Kwanza hongera , kwa kufanya maamuzi ya kufanya biashara lkn pole kwa kushindwa kufikia leo, ww ni sawa na mwanajeshi aliamua kujifunza ukomando, mwanajeshi halazimishwi kwenda kozi ya ukomando bali kwa hiyali yake mwenyewe na ikitokea ukashindwa kumaliza mafunzo unarudi jeshini na unaendelea na kazi kama kawaida, na ukirudi hakuna anaekucheka zaid ya kukupa hongera kwa hatua uliofikia kwa sababu mafunzo ya mwisho ya ukomando ni kupigana ana kwa silaha za moto ukifa ndio umekufa kweli nitolee hiyo. Umefanya kitu kimoja kibaya sana uliacha kazi ikiwa biashara yako haijakua hilo kosa kubwa sana anzisha biashara hakikisha ktk biashara yako hautoi hata mia kwa muda wa mwaka mmoja ina maaana uwe nasehemu nyingine ya kuendesha maisha yako simamia biashara yako kikamilifu hata kama unafanya kazi nyingine punguza kujifanya bosi yaani unao muda kuna kazi unaiweza alafu unamtuma mtu afanye kisha unamlipa cku ambazo huwendi kazini damka ww kwenda kwenye biashara yako, najua umerudi kazini lkn umejua changamoto zilizopo ktk biashara ukianzia kwa majirani wafanyakazi jinsi ya kununua na kuuza nk pole sana , jipange urudi tena ulingoni
 
Nilishafanya hivyo kwa almost two years lakini imeshindikana..najua ata hivi life litaenda tu..
Haha only two years!!!??? How soon ulitegemea biashara iku
Ilinichukua miaka nane ku master nilicho invest na sikuwa na option ya kuajiriwa .

Life doesn't get easier ,you just get stronger
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…