Hatimaye Pierre Konki Liquid anaendelea tu ' Kumuumbua ' Kivitendo Mwana Mpendwa wa Kivukoni Ferri

Hatimaye Pierre Konki Liquid anaendelea tu ' Kumuumbua ' Kivitendo Mwana Mpendwa wa Kivukoni Ferri

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nilikuwa siziamini baadhi ya Kauli hasa hii isemayo ' Kumpiga Teke Chura ni Kumuongezea Mwendo wake ' ila kwa kadri ambavyo naanza Kumuona Pierre Konki Liquid tokea adhihakiwe na adharauliwe na ' Mswahili ' mmoja ambaye kiuhalisia ni wa ' hovyo hovyo ' naona ndiyo Kwanza ' Nyota ' ya Pierre wa Watu inazidi Kung'aa tu na nina uhakika kuwa itang'aa daima.

Kama ulidhani Kumdhihaki na Kumdharau Pierre Konki Liquid kiasi kile ungemmaliza sasa taarifa ikufikie ya kwamba Kitendo ulichokufanya Wewe Mtu wa ' hovyo hovyo ' ndiyo Kwanza umfanya akubalike na cha Kupendeza zaidi si tu kwamba Pierre anapendwa na Watanzania bali sasa hivi hata Mabosi wako ' Kimamlaka ' na ' Kiitifaki ' kama Makamu wa Rais na Spika wa Bunge nao wanamkubali na wanampa kila aina ya Ushirikiano.

Una Chuki na Wivu sana Wewe Mtu wa ' Hovyo Hovyo ' na nina uhakika kuna ' Laana ' zinakuandama ndiyo maana unaona hukubaliki japo unajitahidi mno kuji ' Brand ' huku na kule kwakuwa unalindwa na ' Babaako ' wa Hiari ambaye nina uhakika tena wa 100% kwa hili ulilolifanya kwa Pierre hata Yeye pia hajapendezwa nalo na huenda sasa likamthibitishia kuwa hufai na una matatizo makubwa hivyo afikirie Kukuondoa.

Mimi binafsi siyo Mnywaji wa Pombe ( Gambe ) bali nina Kilevi changu cha ' Kutukuka ' kilichopo maeneo muhimu ya Binadamu wa Jinsia ya Hawa ( Eva ) ila kila nikimuona Pierre Konki Liquid na ' Vituko ' vyake huwa naburudika mno na wala sijaona ubaya wake wowote. Sina cha kumpa Pierre wa Watu ila ninachoweza tu kufanya Kwake ni Kumuombea ' Mafanikio ' mema kwa Mwenyezi Mungu kwani najua hadi Yeye kufika hapo leo hii atakuwa amepitia katika Shida na Taabu nyingi hivyo huu sasa ni wakati wake nae pia kula ' Matunda ' ya Uvumilivu wake.

Kuna Watu ni Wanaume lakini mna Wivu wa Kike Kike sana.

Nawasilisha.
 
Nilikuwa siziamini baadhi ya Kauli hasa hii isemayo ' Kumpiga Teke Chura ni Kumuongezea Mwendo wake ' ila kwa kadri ambavyo naanza Kumuona Pierre Konki Liquid tokea adhihakiwe na adharauliwe na ' Mswahili ' mmoja ambaye kiuhalisia ni wa ' hovyo hovyo ' naona ndiyo Kwanza ' Nyota ' ya Pierre wa Watu inazidi Kung'aa tu na nina uhakika kuwa itang'aa daima.
Mzee baba anajiandaa kulivua nguo bunge zima!
Wenye vibamia wajiandae
 
Isije ikazima ghafla tu,Pierre hatakiwi kuonyesha kiburi kwa kiongozi wake....
Aendelee kuwa mnyenyekevu waka asitoe kauli yoyote mbovu
 
IMG_8075.JPG
Iyooooooh!!!!
 
Isije ikazima ghafla tu,Pierre hatakiwi kuonyesha kiburi kwa kiongozi wake....
Aendelee kuwa mnyenyekevu waka asitoe kauli yoyote mbovu

Kama ameshakubalika na Makamu wa Rais na Spika wa Bunge je huyo Kingozi wako wa ' hovyo hovyo ' Yeye ni nani Kwake?
 
Mzee baba anajiandaa kulivua nguo bunge zima!
Wenye vibamia wajiandae

Mkuu hapo kwenye ' Vibamia ' sijakuelewa vyema unataka kusema ' nanihii ' Yule ' hovyo hovyo ' kumbe ni ' Kibamia ' Mkuu au?
 
Mkuu hapo kwenye ' Vibamia ' sijakuelewa vyema unataka kusema ' nanihii ' Yule ' hovyo hovyo ' kumbe ni ' Kibamia ' Mkuu au?
Teh teh teh!
Vibamia vya "brain" mkuu!

Huzuiliwi kuelewa zaidi ya hapo.
 
Pierre Oyooooo Oyooooo Oyooooo Oyooooo Oyooooo Oyooooo Oyooooo Oyooooo Oyooooo Oyooooo Oyooooo Oyooooo Oyooooo Oyooooo Oyooooo Oyooooo utabaki kuwa juuu juuu kileleni mawinguni
Kulamaisha mzee baba hadi kenge waone wivu Pumbavu zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasituumize vichwa wote lao moja,huyo si mlezi wa WCB na huyu pierre si wanamtumia kikazi anawezaje kumuumbua,akawashike washambawashamba.
 
Unajua Watanzania pamoja na mambo mengine tunapendana sana sana.
Unaweza kwenda baa kupata kinywaji na ukashangaa mtu asiyekujua anakununulia bia hadi unazikataa.
Unaweza kwenda Pub kula chakula na mtu asiyekujua akakukaribisha chakula chake kwa moyo mmoja kabisa.
Mimi niliwahi tumia likizo yangu moja kwenda kijiji fulani kwa rafiki yangu.
Niliishi hapo kwa upendo kabisa na wanakijiji. Kwa upendo wa dhati kabisa wanakijiji wakiongozwa na Mtendaji walinishauri nijiunge kuwa mwanakijiji mwenzao, wakasema kama nitakubali watanipatia shamba kubwa wa ekari kama hamsini hivi bure kabisa.
Na kama nitahitaji kuoa hapo kijijini basi watafurahi zaidi, hata nikitaka kugombea uongozi wataniruhusu tu.
Upendo wa kiasi hiki haupatikani kirahisi katika nchi nyingi duniani kwa sasa.
Mimi nimetembea nchi mbalimbali sikuwahi kuuona upendo kama upendo tulionao sisi watanzania,
Unaweza kwenda mkoa wowote ukajitambulisha kwenye vikundi kama, vya upenzi wa timu yaani ni Simba au Yanga, kwenye Dini au dhehebu, kwenye michezo ya bao au drafti nk.
Na ukapata marafiki wenyeji wakakuhudumia kila kitu bure kabisa, yaani ukala ukalala na kufanikisha jambo lako.
Sapoti ya watanzania kwa Piere ni udhihirisho mmoja wapo wa hii kauli yangu hapa.
Piere kimwonekano ameoneka mtu duni, asiye na kipato kikubwa.
Kwakuwa Piere hana rekodi ya uhalifu basi kwa kufanya utani kidogo tu pale Uhasibu Liquid Bar watu wamempenda.
Peire anapendwa sio kwa uwezo wa vichekesho vyake tu.
Bali kwakua anaonekana mtu duni na watanzania wameona bora wampe sapoti fulani kwakuwa ni watu wanye upendo wa kweli.
Watanzania tutumie hizo fulsa za kupendana kwetu kujiletea maendeleo.
Asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasituumize vichwa wote lao moja,huyo si mlezi wa WCB na huyu pierre si wanamtumia kikazi anawezaje kumuumbua,akawashike washambawashamba.
upooo mwali wewee.. KAH!!! si kwa kupotezea huko😛😛
 
Back
Top Bottom