Hatimaye Polisi ni malaika, wahanga nao wamesahau?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Hiki ni kibwagizo kidogo tokea Tarime.

Ni majuzi tumeona kipigo cha mbwa koko kwa mtuhumiwa aliyekuwa kwenye pingu. Haifahamiki kama polisi wahalifu wale kuna angalau walio bado korokoroni.

Mtwara tuliyekuwa tukiambiwa jambazi kumbe ndiye aliyekuwa mhanga wa yale majambazi sugu yenyewe.

Ya majambazi wa kina Zombe nayo haikuwa habari ndogo.

Mifano ni mingi mno.

Kwamba ghafla polisi hawa wamegeuka malaika? Kwamba Hawabambikizi kesi tena? Hawauwi watuhumiwa kwa kuwaonea? Kwamba sasa ni haki kwa kwenda mbele?

Ya kwamba waliokuwa wahanga wao wa kudumu sasa wamesahau na ndiyo wanawashangilia kwa bashasha kweli kweli?

Labda kama ni mahsusi kwa ajili ya kuwaambia ndege.

Anasema beberu: "Tell it to the birds."

Haiwezi kuwa tofauti.
 
Nimegundua jambo, kutokuwa na consistence kwenye madai yetu ni jambo linalorudisha nyuma spidi ya kufikia mabadiliko kwenye hili taifa.

Mfano, wanasiasa wakianza kudai haki ya mikutano ya kisiasa tutawaunga mkono, kwasababu hili liko kisheria ni haki yao, lakini watuhumiwa watakapouliwa mikononi mwa polisi kabla ya kufokishwa mahakamani, pia tutawaunga mkono polisi, licha ya kuwa polisi wanavunja sheria.

Hii tabia ya ukigeugeu kwetu imeshajulikana kwa watawala, sasa wanajua tukianza kupiga kelele kudai haki zetu, watuache tu, kwani iko siku tutajichanganya wenyewe twende kinyume na zile haki tunazopigania, hivyo hatupewi tunachotaka kwa wakati.
 
Mmeanza kukanyagana wenyewe *****. Kwani mlifikiri wote waliokuwa wanalalamika walikuwa chadema?? Pole sana
 
Kushindwa kujipambanua tunasimama wapi waziwazi ni tatizo kubwa sana:

Kama tunataka Katiba Mpya, Tusiionee "Haya" Haki ya awaye yote

Kuwa unprincipled ndipo tatizo letu lipo yaani "mkuki kwa nguruwe."

Ajabu na kweli vyama vya siasa navyo kimya!

Vyama vya Siasa havijui au vimesahau wajibu wao?
 
Tulia kwanza wewe panya road. Sasa hivi tunawashughulikia ninyi.

Umejiangalia vizuri kwenye kioo? Kwa macho hayo? Wewe si ndiye baba lao? Haraka sana kajisalimishe. Siyo kwa macho hayo. Typical panya road!
 
Mmeanza kukanyagana wenyewe *****. Kwani mlifikiri wote waliokuwa wanalalamika walikuwa chadema?? Pole sana
Chadema imeingia vipi hapo?

Uwe unasoma na kuelewa, usikurupuke; sijazungumzia chama chochote cha siasa, nimezungumzia tabia za wadai haki kwa ujumla.
 
Akielewa jambo lolote huyo ndugu, basi tambua siku hiyo jua litachomoza magharibi na kuzama mashariki. Kama ni kile kipaji pendwa, chake kimsingi ni kikubwa kuliko wale wenzake.
 
Back
Top Bottom