Hatimaye Professor M.A.Mkumbukwa Mtambo wa SUA aula taasisi ya Nelson Mandela Arusha

malema 1989

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
1,319
Reaction score
520
Professor maarufu wa muda mrefu SUA kutoka idara ya veterinary public health Prof Mkumbukwa M.A.Mtambo ameteuliwa kuwa Deputy Vice chancelor Academic, Research and Innovative katika Taasisi ya NMAIST -ARUSHA. Wahadhiri na wanachuo mtegemee mengi mazuri kutoka kwa professor huyu. Hongereni kwa kupata jembe!!!!!!!!!!!!

source: utawala sua.
 
Ni sisi wenyewe ambao tunaendeleza fikra za ufisadi humu nchini. Maneno tunayoyatumia husaidia kufanya hivyo. Kwa mfano neno 'aula'. Hili neno linaashiria kuwa huko anakokwenda kuna 'kula'. je kazi au nafasi aliyokuwa nayo kabla ilikuwa haikidhi haja zake? ni vizuri kutumia neno 'kuteuliwa' kwa sababu huko anakokwenda atakuwa anatumikia nchi na si 'kula nchi'. Tabia ya 'kula nchi' tunaiona waziwazi jinsi viongozi wetu wanavyoila Tanzania.
 

mkuu samahani sana kwa kukukera, nilikuwa namaanisha kapandishwa cheo! maana sua alikuwa mhadhiri wa kawaida.
 
mkuu samahani sana kwa kukukera, nilikuwa namaanisha kapandishwa cheo! maana sua alikuwa mhadhiri wa kawaida.

Na mimi nikuombe samahani kwa vile nilikuwa sikusemi wewe binafsi na najua umeandika kwa sababu ni neno la kawaida tu. Nilichokuwa naongelea hapa inahusu sailolojia ya jamii na jinsi maneno fulani yanavyotumiwa kila mara ili kuhalalalisha kitu fulani. Hii inawezekana kama tabia hiyo imekuwa imezoeleka katika jamii, kwa mfano rushwa. Vile vile maneno mengine hurudiwa rudiwa kwa makusudi kabisa, ili jamii izoee neno hilo na kulikubali bila kulichunguza undani wake.

Kwa mfano, tumekuwa tukisia mara kwa mara Lowasa kuitwa 'waziri mkuu mstaafu'. Hivi ni kweli kwamba lowasa alisataafu uwaziri mkuu? La hasha. Ukweli ni kwamba alijiuzulu. Neno sahihi ambalo lingetumiwa hapa kumhusisha yeye na uwaziri ukuu lingekuwa 'waziri mkuu aliyejiuzulu'. Lakini hata hivyo kustaafu kumerudiwa mara kwa mara kiasi ambacho kwamba watu wengi hawakumbuki kujiuzulu kwake, na kile kilichosababisha yeye kujiuzulu.

Ieleweke kwamba wakati wote jamii inafinyangwa na watu walio kwenye madaraka kwa faida ya watu wachahche. Inabidi tuwe macho kila wakati na tusichukulie tu juu juu na kukubali kila tunachokisoma au kukisikia.
 
kweli mkuu!
kauli tunazotumia zina accelerate ufisadi na ndio maana tija ya wasomi tulionao humu nchini haionekani ukilinganisha na nchi nyingine kwasababu mtu akisoma anachowaza ni mafanikio yake binafsi na tumbo lake then baade tena kwa kiasi kidogo ndio alitumikie taifa, binafsi ntawalaumu sana maprofesa kwa kutojitolea ipasavyo kujenga taifa letu, mfano prof. wa nuclear physics eti unamfanya awe adminstrator wa taasisi fulani badala ya kumtumia directly kuratibu masuala aliosomea na kufanya research kuhusu field yake!
 
Na leo tena magazeti yameandika kuteuliwa kwake na rais kuwa mkurungenzi mkuu wa shirika la utafiti na maendeleo ya viwanda Tanzania (TIRDO) kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu. Sijuwi sasa hapo inakuwaje? Shirika hilo Kwa sasa liko taabani na linahitaji kufufuliwa ili liweze kufanyakazi zake Kwa maendeleo ya nchi yetu. Na ili afanikiwe kulifufua upya mabadiliko makubwa yanahitajika ikiwemo kuhamisha baadhi ya wakurugenzi hasa huyu anayekaimu ukurugenzi mkuu kwa sasa maana atamkwamisha.
 
wabongo bwana!!

hivi hujui aliyeleta uzi ni mtu wa aina gani!

mkuu kuna kitu kinaitwa rejesta... nadhani ulisoma katika somo la kiswahili!

kuula ina maana kwamba amefanikiwa katika jambo fulani.. wala hata haina maana mbaya!

kwa mfano, tunaposema, ameula wa chuya, tuna maana gani?
 
wabongo bwana!!

hivi hujui aliyeleta uzi ni mtu wa aina gani!

mkuu kuna kitu kinaitwa rejesta... nadhani ulisoma katika somo la kiswahili!

kuula ina maana kwamba amefanikiwa katika jambo fulani.. wala hata haina maana mbaya!

Asante sana kwa kunipa 'somo'. Ndio, nimesoma Kiswahili kuanzia darasa la kwanza mwaka 1962 mpaka High School, nimekuwa mwalimu wa Kiswahili shule za sekondari na vyuo vikuu.

Naelewa sana maana ya matumizi ya misemo kuwakilisha maana fulani katika lugha. Kila mtu vilevile anaweza kutafsiri lugha jinsi anavyoiona, licha ya kwamba amesoma au la.

Hata hivyo nilichokuwa nakisema ni jinsi maatumizi ya maneno fulani yanavyodumisha, kukuza na kuendeleza mitazamo na hali tofauti katika jamii. Kwangu mimi, neno 'kuula' japokuwa linamaanisha kupata kitu fulani, kwa mantiki hii, kazi, hata hivyo linabeba hisia ndani yake kuwa huyo aliyepata kazi 'atakula' huko kazini kwake. Hapo neno 'kula' lina uzito zaidi ya kufanya kazi.
 

mkuu unajua ukimchunguza sana kuku...... ok, hebu niulize kitu kwa mara nyingine... sorry sir, hivi mtu akisema anaenda kutafuta mkate wake wa kila siku anamaanisha nini?? si anatafuta 'kula'?... btw, unayosema ni kweli, kula za siku hizi inachukuliwa vibaya, ila nakumbuka mwaka 1954 wakati tunaanzsha TANU, haya mambo hayakuwepo kabisa!
 
ila nakumbuka mwaka 1954 wakati tunaanzsha TANU, haya mambo hayakuwepo kabisa!

Hii ndiyo nilikuwa naamanisha, ingawa miaka hiyo ya 1954 siwezi kuongelea!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…