Hatimaye Saul Alvarez Canelo apata mbabe wake

godson njamakuya

Senior Member
Joined
Mar 6, 2021
Posts
170
Reaction score
196
Dimtry Bivol bondia kutoka Russia hatimaye ameweza kumshinda kwa points, bondia machachari kutoka Mexico Saul Alvarez Canelo katika pambano la raundi 12 lililofanyika Las Vegas. Pambano lilianza kwa Canelo kupiga ngumi mfululizo huku mpinzani wake akimsoma.

Bivol alionyesha utulivu na kushambulia kwa umakini mkubwa akipiga combination za uhakika zilizoingia sawasawa kwenye mwili wa Canelo, ambaye hakuamini, kwani kwenye press conference alikiri Bivol ni bondia mzuri, lakini aliisema atatumia uzoefu wake na tactics ili kumshinda. Haikuwa rahisi kama alivyofikiri kwani mpambano ulikuwa mgumu, wote walikuwa wakishambuliana kwa zamu, lakini alionekana Bivol kutumia vyema urefu wake uliomsaidia kurusha ngumi akiwa mbali na Canelo ngumi zilizompata vyema.

Mwisho wa raundi ya 12 alitangazwa Bivol kumshinda Canelo kwa points baada ya kupewa ushindi na majaji watatu. Hii ni mara ya pili kwa Saul Canelo kushindwa, mara ya kwanza ilikuwa alipopigwa na Floyd Mayweather Jr, "Team Money"
 
Sio bure ina maana wamarekani hawakumuwekea kikwazo chochote huyo bondia
 
Picha tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…