dem boy
JF-Expert Member
- Nov 4, 2016
- 6,580
- 15,739
Afadhali mwaka jana kidogo,robo fainali ya kombe la shirikisho ilitupa mdomo,lakini msimu huu umekuwa mchungu sana japo klabu bingwa tulifika robo fainali ila Utopolo wamefanya vitu vingi sana msimu huu vya kutukera ambavyo pasina shaka nakiri vitu hivyo ni mafanikio sana kwao
Walianza kutukera na ngao ya jamii,na bora magoli angefunga moloko au bangala lakini mtu aliyetufunga magoli yote mawili ndo mkeraji zaidi hasa ile staili yake ya kutetema,huyu mtu hatumpendi sio kumuona tu hata kumsikia huyu
Wakaja na na swala la kuongeza ligi,Utopolo tangu wachukue usukuni wa kuongoza ligi sijui mechi ya pili au ya tatu tu ya msimu hawakuwahi kutoka pale juu tena mpaka ligi inaisha hii pia ilitukera sana,maana zilikuwa kama mbio za mtu mmoja tu
Tukasema kama kawaida kimataifa Utopolo ana kawaida ya kufeli,hana analolijua kule.Kwahiyo tutapatumia kule kama fimbo ya kumchapia,kilichotokea Mungu mwenyewe anajua.Ni full dozi home/away.Labda leo atafungwa na huyu lakini wapi,Uto hao mpka fainali na waarabu walilala na viatu pale pale kwao
Matumaini ya mwisho yakabaki kwa Azam,hawa ni Utopolo wenye hela,wenzao wiki nzima wanakula bata mara ikulu mara parade tukasema sopu ,dube,akaminko,kipre watatutabasanisha.Kilichotokea bora fainali angecheza Ihefu
Ila hili la parade ndo limekuja kuua zaidi,siku nzima hakuna kitu kinafanyika na kuongelewa mjini ni Uto tu,nyomi lile la watu kuilaki Uto from airpot to jangwani itoshe kusema Uto wapo wengi kuliko sisi,lakini tunamshuuru mungu jana wamemaliza kutukera nadhani sasa tutapumua maana kila kitu kimeshakwisha tusubiri msimu ujao labda tunaweza kuwa challange hawa Uto maana wapo siriaz kinyama.
Vitu vilivyotupa furaha wanasimba msimu huu ni vya kijinga sana na wala havikusababishwa na timu yetu na wala havikuwazuia Uto kufanikisha malengo yao ya msimu ndo maana nasema ni vya kipumbavu,vitu hivyo ni sakata la fei toto,ihefu kumfunga Uto,Manara kufungiwa,marumo kucheza chenga twawala kwa mkapa
SIMBA TUSAJILI MSIMU UJAO UNAWEZA KUWA WA MATESO ZAIDI KWETU,HAWA WATU WANAWEZA KUCHEZA NUSU FAINALI KLABU BINGWA...OHOOOO

Upvote
3