Hatimaye Trump audhihirishia Ulimwengu kuwa, Marekani siyo Taifa kubwa tena.

Hatimaye Trump audhihirishia Ulimwengu kuwa, Marekani siyo Taifa kubwa tena.

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Posts
2,869
Reaction score
3,187
Dola la Marekani kutoka kuiokoa Ulaya:
  • Mwaka 1917 isiangukie mikononi mwa Ujerumani;
  • Mwaka 1924 kupitia Dawes & Young Plan isiangukie kwenye Socialist Revolutions;
  • Mwaka 1941 baada ya Pearl Harbour isiangukie kwa Hitler;
  • Mwaka 1948 kuipitia Marshall Plan isiangukie kwa Urusi.
Na kisha kuwa-convince Wazungu kuungana pamoja katika Umoja wa Kijeshi (NATO) kujikinga na vitisho vya Warusi. Kuonyesha nguvu, Marekani alianzisha military bases nyingi dunia nzima kuanzia Panama, Ujerumani, Uturuki, Japan, Korea etc.
Ghafla sasa, Mmarekani anamuonea wivu Mjerumani eti anauza zaidi USA kuliko anavyonunua. Anamlaumu kutenga bajeti ndogo ya kijeshi kwao. Wanamlaumu Mchina kwa kudhibiti bidhaa za Marekani. Cha ajabu Trump analalamikia mambo waliyoyasnzisha wao kipindi wakiwa strong kiuchumi.
Shida yote hiyo ni kwa sababu, There's a New Sheriff in Town in the name of China. Watapata tabu sana.
 
China ameuza silaha nyingi Africa kuliko US. China ameanzisha kongamano kubwa la Wakuu wa majeshi Africa. Trump siyo strategist hawezi Ku counter China. Ngoja akimaliza muda wake upime hali kwa atakayekuja. Kama akiwa stragegist consecutive
 
Sasa Wewe jiulize, kulikuwepo sababu gani ya Trump kutaka kujenga ukuta mpaka ni na Mexico kuzuia Walatino kuingia kwao? Kwa nini hatua hizi zije sasa hivi?
 
Mtakumbuka kuwa, baada ya German Unification 1871 na hasa ukuaji wake mkubwa wa uchumi, Waingereza walianza kuionea wivu mkubwa Ujerumani. Na hata ukichunguza vyema narration na sequence ya matukio kuelekea WW I, utagundua kuwa, Uingereza alikuwa tu na hamu ya kuipiga Ujerumani kwa kuwa alijua atashinda tu hiyo vita kupitia ushirika wao na Ufaransa (Tripple Alliance). Kwa kuwa, hawakupata ushindi namna walivyotaka ikiwemo kwenye WW II, basi wameendelea kuichukia Ujerumani hasa baada ya Economic Miracle ya Ujerumani miaka ya 1950s wakati wao wakikua taratibu licha ya kutoathirika kwenye WW II kama Ujerumani.
 
Matatizo ya kiuchumi duniani yaliyoanzia Marekani na kusambaa Dunia nzima kati ya 2008 - 2012, yaliidhohofisha sana Marekani na haikuwahi tena ku-recover, hivyo kuifanya Dunia kuitegemea China kama inspirational kwao kutokana na uwezo mkubwa wa kuagiza bidhaa za nje na hivyo kusaidia kufufua uchumi wa nchi nyingine.
Ndo hiyo waswahili wanasema: Usiyemtaka kaja.

In African visit, Xi Jinping aims to step in where US steps aside
 
Tangu Trump aingie madarakani, ameifanya Marekani kuwa Nchi ya kupinga mikataba mbalimbali ya kibiashara na kimazingira. Mfano mkubwa ni Mkataba wa kuizuia Iran kutengeneza Silaha za Nyuklia.
IMG_5286.JPG
 
Back
Top Bottom