Hatimaye unabii wa Afande Sele juu ya Saida Karoli umetimia

Hana jipya saida anaforce kurudi kama mr nice but atapaki tu
Evidence
Wimbo wake mpya kwa mimi judge wa music sijaona kipya kutoka kwa saida uchezaji ni uleule mistari nayo anarudia rudia aliyoimba zamani na ya wenzie kama darasa na chibu.
 
Muziki sio mpira ushindanishe ili upate timu bora. Kusema mwanamuziki fulani ni bora kuliko mwingine ni akili fupi, kwasababu binadamu hatufanani hisia. Kuna watu wakisikia nyimbo ya Bob Marley radioni wanabadilisha chanel lakini huwaambii kitu mbele ya taarab. Sasa unataka kusema Isha Mashauzi ni bora kuliko Bob Marley?
 
huyo saida ndio mnamlinganisha na vanessa?...kwaah!!!
 
Saida yuko vizuri sana na karudi kwenye game vyema. Ila kuna vitu anatakiwa abadilike kidogo. Clouds najua ni wazoefu watumie mwanya huo kumuelimisha.
 
tapeli ruge atampiga asipokuwa makini...sijawahi kuwaamini wale
 
Kuna siku nilikuwa naangalia movie moja ya Hollywood. Inaitwa "Peeples". Ni ya kuhusu familia moja ya matawi ya juu ya African Americans na matatizo ya kimapenzi.

Ghafla nikasikia ngoma nzito za wimbo wa Saida Karoli wa "Maria Salome". Nikaona si utani.

Saida Karoli alikubalika mpaka Hollywood.

Tatizo elimu na exposure.

Nilipokuwa Kampala kuna rafiki yangu Mganda aliniambia Saida Karoli alikubalika kichizi Kampala. Akaitwa kwenda kupiga muziki. Alivyoenda Waganda wakawa so disappointed kwa sababu walivyomtegemea awe na alivyokuwa ni tofauti. Walikuwa wametegemea mwanamuziki mmoja yuko very sophisticated, Saida akaenda very simple, even naive.

Ukitaka kuona sehemu ya movie yenye huo wimbo, video ya YouTube hii hapa.

Jamaa kaingia ukweni kamkuta mama mkwe yupo katikati ya kucheza wimbo wa Saida Karoli.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…