Hatimaye wa Nigeria warudi makwao

Mimi Ni mtanzania ila Kuna mitanzania Ni Kama mizoga
 
Sisi ni ndugu... Huu ukenya na utanzania utaisha Lini?
 
Pwahahahaha!!!
Weka summary kijana, we have job to do. Ndiyo maana wakenya MNAKUFA KWA NJAA SABABU MUDA MREFU MNAUTUMIA KUANDIKA INSHA BADALA YA KUFANYA KAZI.

Niongeze volume!?

Uandishi pia ni kazi kama hukulijua hilo....
Kuna watu wanaishi mjini maisha full raha kwa kutegemea uandishi.
 
Umeongea point ya msingi sana
 
Mkuu kwa hayo uliyoyataja hakuna mkono wa mtanzania wa kawaida katika hayo. Sijawahi kuona mtu anabugudhiwa Tanzania maana tuna ujamaa uliokithiri hadi unaboa mitaani. Bongo hata uje na hiyo sheng sana sana utapendwa tu kama mzee ojwang au inspekta mwala [emoji4][emoji4]

Wakenya ni wengi tu hapa nchini tena wanajiita wajaluo wa Tz. Hawana vibali na wanaishi vizuri tu. Huko Kagera unapopataja ni kama shamba la bibi kwa wanyarwanda maana wapo kibao tu na wanajinasibisha ni wahangaza au wanyambo lakini hawana utanzania ndani yao na si ajabu hata hawazaliani na mtz wa kawaida

Huko Kigoma napo ni hivyo hivyo. Wamejaa warundi nao wanajiita waha na hawasumbuliwi kwa lolote na wanaishi kwa amani.
 

Hilo ni kosa sana hata kama ni Wakenya wenzangu, leo mpo mpo tu maana liinchi lenu likubwa sana limejaa mapori hayajalimwa, raslimali bado zipo nyingi. Lakini binadamu yeyote yule hubadilika kulingana na uchache wa raslimali.
Hiyo Tanzania pamoja na ukubwa wote huwa wa ardhi, bado utakuta matukio ya watu kudhulumiana, nakumbuka ipo siku Makonda alikua akizuguka kuwahoji wananchi waliodhulumiwa ardhi, tena akiwapa kipaza sauti wanaongea live.

Migogoro ya ardhi ipo kwenu japo sio sana, ni ishara siku raslimali zikipungua, mtaanza kuonana kama wnegine wanavyoonana leo.
Nenda kule Zanzibar ambapo wana ardhi kidogo, wahoji wabongo walionunua huko au kuishi wakuambie jinsi husemwa semwa na Wazenji.
 



Nyumbani ni nyumbani, tatizo la SA ni shida iliyotokana na "apatheid trauma", kabla hakujatulia, wageni wakaingia kwa wingi ikatokea "immigrants trauma"--- sasa wageni wanarejea makwao kitakachotokea ni "tribal crashes" kati ya Xhosa dhidi ya zulu, Wazungu dhidi ya xhosa-zulu, coloured dhidi Wahindi nk, SA itarudi tena katika aina mpya "apartheid" kwa sababu "ADUI" yao wahamiaji watakuwa out of their sight, kitakachokuwa in their sight ni wao kwa wao.

Kiasilia wa Xhosa wanawona Wazulu na Wazungu ni wavamizi.

Baada ya Wahamiaji kurudi makwao, vita ya kupambana na uchumi wa kibaguzi inayofanywa na J Malema itapamba moto kwa kasi kubwa, kwasababu inasemekana vita hiyo haikuwa na nguvu kutokana na wageni kufanya kazi kwa wazungu bila masharti, ilimradi mkono uende kinywani hii iliwachukiza sana Wenyeji.
 
Ardhi Tz kwa ujumla wake sio haba ila ardhi kwa baadhi ya sehemu za Tz ni haba mfano kilimanjaro tu..

Kuhusu migogoro ya ardhi kwa ukubwa hutokea sehemu za miji ambazo ardhi ina thamani kibiashara na kimakazi na pia sehemu zilizotokea uvamizi mfano wachungaji wa kuhamahama wanapovamia maeneo ya mashamba.

Kingine kugombania rasilimali ni human nature for survival na hakuna cha kushangaa. Kuhusu ardhi na rasilimali kuwa Idle ni kwa sababu ya uwepo mdogo wa sekta binafsi ambao uliondolewa kwa kiasi kikubwa na ujamaa hivyo vitu vingi vikubwa kama kilimo na ufugaji vilikuwa na umiliki wa serikali au foreigners. Kwa sasa mdogo mdogo kutokana ajira kubana na maisha kuwa ghali hivyo, imeshaanza kuwa kawaida watu kugeukia ujasiriamali kama kilimo biashara..

Hivyo sio mbali tu hivi vilivyo wazi kwa sasa si muda mrefu hutoviona tena. Naongea kama mtu wa kizazi hiki cha sasa.
 

Ni PM jina unalitumia.
 
Wewe si ni pessimist tu, wabongo kibao wamehamishia makazi na familia zao botswana, kenya, ug, rwands, namibia, zambia etc, nchi za,kiafrika zinazojielewa atleast. But you are a negative minded guy.
Tuishi Kwa undugu na amani kama waafrika Sisi ni wamoja maana tukibaguana katika bara letu mabara mengine pia yatatubagua . Tusikubali kutenganishwa na siasa ambazo hazina muelekeo.
 

Kwa yote uliyoyasema, cha maana ni hii sentensi 'Kingine kugombania rasilimali ni human nature for survival', binadamu akianza kupungukiwa raslimali, huanza kuonana wabaya, haijalishi yeye wa wapi wala nini.
Hata huko Kusini unakoskia haya yote, ingetokea serikali itimize majukumu yake ya kuhakikisha ajira na maisha bora kwa raia wake, leo hii wangekua wanaitana ndugu na kucheza kwaito kwa pamoja na wageni.

Hamna binadamu special ambaye hawezi akaingiwa na uwazimu pale raslimali zinamuishia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…