Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

VIONGOZI WA CHADEMA WANAPASWA KUSHTAKIWA ILI WALIPE FIDIA KWA WAHANGA WOTE WALIODHURIKA WAKIPIGANIA CHAMA.
Kwani kikiwatuma una barua ukiyoandikiwa na Chadema kuwa ukipiganie? Si ulikuwa wehu wao wenyewe
 
Kwa usaliti huu wa Eva, Delila na Herodia na BAWACHA bado kuna mtu anapanga kuoa!
 
Nimeona watu wengi wanawashambulia wabunge wa viti maalum CHADEMA waliokula kiapo leo. Lakini kwa maoni yangu naona wako sahihi kabisa kwenda bungeni angalau kuongeza ladha ya bunge ambalo tayari limesheheni wabunge wa CCM. Ingekuwa vema kma CHADEMA wangekuja na suluhisho la nini watafanya baada ya kuonekana uchaguzi ulivurugwa na watu wachache na sio kususa. Kususa imeonekana sio njia sahihi ya kudeal na masuala ya uchaguzi na siasa za Tz kwa ujumla.

Tulishuhudia mwaka 2015 maalim Seif na wenzake walisusia kujiunga na serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar na miaka mitano iliisha na hakuna kilichobadilika.

Tulishuhudia wapinzani wakisusia bunge la katiba kwa madai ya kutaka serikali tatu kitu ambacho kisingekubaliwa kamwe na CCM, lkn kma wangekubali kupitisha rasimu ile angalau ilikuwa na mambo mazuri mengi kwa Taifa kma tume huru ya uchaguzi n.k. Mambo ya serikali tatu yangekuja bdae.

Kwa kifupi ni kwamba mkiamua kususia jambo mtafute njia nyingine sahihi ya kutatua tatizo na mashinikizo yatakayofanya serikali ikubali madai yenu, ktk hili sioni kma wapinzani wamejipanga na kma hawajajipanga ni bora kuruhusu hao wachache wakaongee kule bungeni na kuweka mashinikizo kwa serikali kuliko kutokuwa kabisa na wawakilishi wa upinzani
 
Namuona dada yangu NUSRAT HANJE....

Maisha ni safari....

Kalala na KUNGUNI kwa miezi 3 baadae huyooo MBUNGE...

Naam KESHO HAIJULIKANI jama.....

Naaam HAIJULIKANI...usishangae SEIF SHARIFF HAMAD ni MAKAMU WA RAIS....na Jussa WAZIRI WA AFYA....
Ha ha haaa hapo kwa Jussa pamenifurahisha zaidi yaani jamaa kapondwa na polisi kaenda kutibiwa Nairobi halafu anakuja kupewa/kupozwa na uwaziri wa afya... siasa bwana yani basi tu!
 
Chadema smart tunakataa hili dili la Mbowe kula pesa za CCM kuuza wabunge wa kike na nyinyi CCM wenye akili timamu kataeni dili la CCM kutumia pesa za walipa kodi kununua wabunge badala ya kuzitumia hizo pesa kuleta maendeleo, sisi tusipenda unafiki tumekataa na wasipenda unafiki huko CCM kataeni matumizi mabaya ya pesa za umma
 
Kwahiyo Lissu hajaondoka kwa kuogopa vitisho kumbe?
 
Ushauri mzuri kama huu ulishatolewa sana humu.
lakini walioshauri waliambulia matusi na kejeli.
 
Hii dunia kweli duara. Haya yanayoendelea katika taifa hili kuna kitu kinajitafuta.
Mimi sio mtaalum wa masuala ya sheria na uendeshaji wa Bunge. Je ni sahihi kuapisha mbunge ama wabunge nje ya vikao vya bunge?
 
Hii hotuba ya Mdee, akimshukuru Spika???? Sio kweli, sio uzushi kweli huu? Nitaamini nikimsikia Mdee kwa macho yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…