Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

Sawa mkuu!

Vipi sasa juu ya msimamo wenu kama chama?
Sina tatizo na msimamo wa chama maana mimi sio sehemu ya maamuzi ya chama. Msimamo wangu uko pale pale, ule haukuwa uchaguzi bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Hao wadada waende wakatafute pesa, lakini wasikae wakategemea support yetu.
 
chadema kwisha habari yake., sasa maalim seif anasubiri nini naye aapishwe makamo wa kwanza, pia wale wabunge 4 wende zao bungeni na wawakilishi wakaape nao barazani tusubiri tena miaka 5 waendelee kuchinjiwa baharini
Wala CHADEMA haijaisha Habari yake! Upinzani Upo na ni imara kuliko mwanzo, tunaandamana ndani kwa ndani, na wanawake wa CHADEMA kwenda bungeni siyo kitendo cha aibu au kushindwa! Kwa hali iliyopona ushabiki, kama huu wa kwako, kile ni kitendo cha ujasiri mkubwa na kitakua na matokeo makubwa na mazuri! Kuna wana ccm mtajuta kushabikia au kuponda kitendo hiki!
 
Mzee ulivyoambiwa uandame ulishiriki?
 
Mbowe alifungwa MIEZI 4 Segerea...
BADO NI MWENYEKITI NA ANAPAMBANA🤣

Esther Bulaya alilala sana ndani mpaka "akalazwa"....
Leo KAAPA kuwa MBUNGE🤣

Shemeji Jesca Kishoa kakutana na changamoto NYINGI mno....
Jana mumewe komredi D.Kafulila AMELISIFU JEMBE LETU MAGUFULI KWA SIFA STAHIKI...
Leo ameshuhudia mh.Kishoa anazama "mjengoni"🤣

Kamarade mh.Hallima James Mdee ni "mkulungwa" wa Kuishi SEGEDANCE......
Leo ameapa kuwa mbunge na ATAIJENGA KAWE akiwa na mh.Askofu Gwajima🤣🤣🤣

Na huyu FUNGA KAZI mh.Nusrat Hanje....
Dada kapambana Sana na MBU "mule ndani" leo hakika ni MBUNGE....🤣🤣

SIASA NI HARAKATI ZA DAHARI....
MAISHA NI MAPAMBANO....
MAISHA NI SAFARI NDEFU...
SEHEMU YA KUINAMA INAMA NA KAMWE usiunyooshe mgongo....UTAVUNJIKA!!!!

Nimeyapenda maneno ya kushukuru ya mh.Mdee....

Anasema ATAMPA USHIRIKIANO SPIKA...hapa amemkubali spika,inakuwaje AMKATAE MWENYEKITI wa CCM wa mh.Spika NDUGAI?!!!😂😂😂
 
Kwisha habar yenu, wabongo na siasa ni vitu 2 tofauti
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 tuombwe radhi tulioitwa majina ya ajabu ajabu kisa hawa wapinzani halafu leo wanasema viti sio hisani bali sehemu ya ushindi so wanakubali magu alishinda nyingi na lissu sehemu ya ushindi
 
Hivi kweli hawa Chadema wameshindwa kuvumilia kwa miaka 5 tu ..... Kwa mtindo huu kitachofanyika 2025 itakuwa zaidi ya sasa.
Uraiani kugumu
Hiyo miaka 5 watapiga mishe gani labda
Kuna wengine hapo walipotoka chuo ajira ya kwanza ubunge 😂

Ova
 
Yule mgombea wa muheza wamemwacha?
 
Lissu leo katettwet akitaka vikwazo, hajahusishwa
Wewe ndiyo unasema haukuwa huru na haki. Chadema wanajua ulikuwa huru na haki na leo wamepeleka wabunge viti maalum kuapa. Pole sana na kibaraka Lissu Amsterdam!
Trump naye tayari ameshaunga juhudi anamwachia presidaaa elect aanze kusafisha mapito.Lissu wewe nani na EU yako.Mwaka huu mtajibeba.Nchi kwanzA ushamba baadaye
 
Tunasubiri Neno la mbowe, na kuwafutilia mbali uanachama hao wasaliti
 
Harakati lazma ziendelee.
HAKUNA asiyejua kuwa chadema wamefanyiwa ukatili na magufuli lakini kwanini tuwakataze wawakilishi wetu wasiende bungeni.
Waache wakatetee chama.mimi naona Bora tuwaunge mkononna tuwasapoti hao wabunge.huku harakati za kupigania tume Huru zikiendelea.dunia haiishi Leo Wala kesho.magufuli ataondoka lakini chadema na ccm vitabaki.kikubwa mjipange kwa uchaguzi ujao
Narudia Tena em fikiri vzr. Hivi unafikiri ruzuku za Kila mwez 200million kwa chama kwa ajili ya uendeshaj hazitoshi pasiii na kuwepo wabunge bungen?? We una dhani ku a kuwepo wao bungen ndo Kuna endesha chama?? Em tafakar tena
 
Kupigania haki hakuishi na ni kitu cha lazima. Ubaya ni kumkadhi mtu/watu jukumu la kupigania haki yako. Hiki ndicho kinachofanya wanasiasa wawachezee watanzania. Watanzania karibu wote wamekabidhi jukumu la kupigania haki zao kwa wanasiasa bila kufahamu kuwa wanasiasa wengi wako kwenye siasa kupigania matumbo yao. Na mbaya zaidi hii hali imeshingia mpaka kwenye dini.

Waumini wengi wanategemea viongozi wa dini kuwaombea kwa Mungu ili atatue matatizo yao bila kujua kuwa viongozi wengi ni matapeli. Kazi ya kumuomba Mungu inatakiwa ifanywe na muumini mwenyewe. Infact uvivu wa kutotaka kujihangaisha ndiyo mama wa janga hili. Raia wengi hawataki kujihusisha na vitu vinavyo-affect maisha yao bali wanataka watu wengine wawafanyie.
 
Sasa kama siasa za Africa hazijawahi kuwepo kwa ajili ya kupigania wananchi hilo ni jambo la kufurahia au la kuunga mkono kwa mtu mwenye akili timamu au linapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote?
Kinachofurahisha na kuchekesha,ni kwamba mlichelewa sana kulijua hilo,huku mkikinasibu chama chenu CHADEMA kama wapigania haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…