samirnasri
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 1,388
- 213
Kuna taarifa kuwa uongozi wa chuo kikuu cha dodoma umewafukuza wale ambao unawaita vinara wa mgomo ambao ulianza juzi chuoni hapo na kuwataka waondoke chuoni hapo kabla ya sa kumi na moja jioni jana. Uongozi wa UDOM mara nyingi umekuwa na roho nyepesi kufanya maamuzi ya kufukuza wanafunzi mapema mara tu unapotokea mgomo lengo likiwa ni kuwafurahisha viongozi wa chama na serikali. Ukweli ni kwamba madai ya wanafunzi ni ya msingi na ndio maana jana waziri wa elimu shukuru kawambwa aliridhia serikali kuwa na mpango wa mpito kuwawezesha wanafunzi hao kufanya mafunzo kwa vitendo. Naushauri uongozi wa udom kuacha tabia ya kufukuza fukuza wanafunzi wakidhani kwamba watamaliza migomo kwa namna hiyo.