Hatimaye wanalunyasi tumeiga mazuri ya Yanga

kilwakivinje

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
6,184
Reaction score
9,407
UONGOZI UNASEMAJE ??

Nilichoolezwa ni kuwa Uongozi wa mbugani unafanya mchakato wa kubadilisha utaratibu wa malipo ya posho (bonus) za wachezaji, Kutoka kwenye utaratibu wa malipo ya bonus kwa kila mechi kwenda kwenye malipo ya Bonus kulingana na mafanikio ya timu.

Awali bonus zilikuwa zikilipwa kwa wachezaji na benchi la ufundi kwa kila mechi wakishinda lakini kwa sasa Uongozi unapendekeza bonus ziwekwe kwenye mikataba na zitatolewa kwa wachezaji pale timu inapotimiza malengo.

Mikataba ijieleze kuwa endapo timu itafikia malengo ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu basi bonus itakuwa kiasi fulani, ikifika nusu fainali ya CAFCL bonus yake ni kiasi kadhaa na vilevile bonus ya timu ikifanikiwa kutwaa ubingwa wa FA.

Uongozi umegundua unaingia gharama kubwa za uendeshaji kwa kulipa posho kiasi kikubwa wakati huo malengo ya klabu hayafikiwi. Mfano msimu uliopita timu ilishinda michezo 22 na Uongozi ulilipa bonus zote za ushindi wa mechi hizo lakini hakuna malengo yaliyotimia kwa klabu zaidi ya kushika nafasi ya pili.

Sasa uongozi unakuja na mfumo ambao baadhi ya wachezaji wakongwe ndani ya klabu na haswa wagenyi hawautaki (Kipara, mwamba, na hata beki misifa)

Mchezaji kama kipara amekuwa akidai posho ya kila mechi wanayoshinda na hata inapocheleweshwa amekuwa akishinikiza migomo na ndo sababu kubwa inayotajwa ilimuondoa kule kwa watani zao yanga

Uongozi wa mbugani umeamua kuiga mfumo huo ambao ushaanza kutumika kwa watani wao na ndio umewaondoa baadhi ya wachezaji wengi wanaoweka maslahi yao mbele badala ya timu.

Sent from my SM-N975U using JamiiForums mobile app
 
Shikamoo mjomba
 
Kale kakipara kanapenda sana kulalamika hata kwenye maisha bunafsi.
Issue sio kulalamika, hawa viongozi wa soka wengi ni wapigaji, wao wanajilipa kila muda ila wachezaji sasa kulipwa mpaka walete mgomo

Mchezaji ukiwachekea na kuleta uzalendo sana utaishia kutumika na siku unaacha soka huna chochote mfukoni

Mashabiki wengi tunazingatia mafanikio ya timu lakini tunasahau, stahili za wachezaji ambao ndio maisha yao waliyoyachagua ili kuingiza kipato na kuendesha maisha yao
 
Toka ile J2 ya goli mpaka sasa, hakika Simba mnateseka saaana.
 
Simba kama CCM tu, makelele mengi mipango kipengele
 
Inapendeza sana! Something good is something to imitate;
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…