Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,916
- 43,505
Ukweli usemwe Msanii Lava Lava ni mmoja ya wasanii chini ya WCB waliokuwa wanapitia kipindi kigumu sana tangu ajiunge ndani ya WCB!
Lava lava amekuwa na bahati mbaya sana kutoka kwa mashabiki pamoja na kujitahidi kuimba lakini mashabiki kwa kipindi kirefu wamekuwa hawamuelewi kabisa kiasi kwamba kuonekana ni moja ya mizigo ndani ya WCB maana walikuja wakina Mboso na Zuchu wakatoboa lakini yeye bado aliendelea kuonekana kama msindikizaji!
Hakika pengine naweza kukubali kila kitu kina muda wake kabisa na kwa hakika pengine mwaka 2021 tena mwishoni umekuwa wakati mzuri kwake toka aanze kazi zake za muziki kwani kwa kipindi hiki kuanzia mwezi wa kumi kumekuwa na mabadilliko kwenye nyimbo zake na hata mapokeo ya nyimbo zake za Inatosha na Ng*ari ng*ari zimefanya vyema sana hapa nchini na kwa hakika naweza sema hasa Ng’ari ng’ari umekuwa wimbo bora sana kuanzia mtaani!
Kwa hakika naweza kusema Lava Lava kafunga vyema mwaka na Ng’ari Ng’ari na kwa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka huu ndio unaweza kuwa ndio wimbo unaotamba sana ukiacha nyimbo zingine za wasanii!
Kwa kweli niwapongeze watanzania kwa kumvumilia huyu kijana na kumpa nafasi na sasa amepokelewa vyema japo kwa kuchelewa!
LavaLava mguu ulio amka nao mwisho wa mwaka huu usiuache!