Ndugu zangu watanzania uchaguzi umekwisha tunachongoja ni matokeo ya jumla ya urais.Nifuraha yangu kuona upinzani umeongezeka bungeni,kwani hii itasaidia kupunguza makubaliano ya miswada ambayo haina maslahi kwa taifa letu.Basi ndugu zangu tupunguze ushabiki wa kidini,kikabila,rangi na kikanda.Kwani hakika utengano ni udhaifu na umoja ni nguvu,basi na tuwe wamoja tujenge taifa letu hili changa.Siasa za mwaka huu zina harufu ya udini,hivyo kuifanya amani ya taifa kua mashakani.Watakao taka kuandamana na kuleta machafuko ni hiyari yao,ila kumbuka unaweza pata kilema au kupoteza maisha,aliyekuhamasisha tawari amekwisha kuwakimbia akiacha nchi inawaka moto.Dr.Slaa anapinga matokeo ni vema kwenda mahakamani kuliko kuingia barabarani hii ni hatari!
1. Udini na ukabila vimebuniwa na kutumiwa kisiasa kuchafua baadhi ya wagombea. Sijawahi kusikia mfano makanisani waumini wakihubiriwa wamchague kiongozi fulani. Natolea mfano Kanisa Katoliki kwa vile nasali huko. Kanisa hili lina wanachama kutoka vyama vyote hapa nchini. Kwa hiyo, haiwezekani askofu, padre au katekesta mwenye akili timamu kuwahubiria watu wamchague kiongozi fulani wa chama (kimojawapo) bila kuzua mtarafuku ndani ya Kanisa lenye waumini wa itikadi tofauti za vyama. Hali kadhalika kuhusu ukabila.
Jambo ambalo lilikuwa linahusishwa na udini ni kule Dr Slaa kuwa padre wa Kanisa Katoliki na baadhi ya wanasiasa kutumia hiyo kama nyenzo ya kuzusha kila aina ya uongo eti bado anapokea maagizo kutoka kwa maaskofu na mapadre ili akiwa kiongozi atetee maslahi ya Kanisa Katoliki. Naomba kama mtu yeyote ana mfano wa askofu, padre na katekesta wa kanisa hili, ambaye alikuwa anawahubiria waumini wake wamchague Dr Slaa ajitokeze na aseme ni nani, ilikuwa wapi na lini na kwa nini haikuripotiwa polisi au mamlaka husika ili ashughulikiwe kisheria kuliko kusababisha mtafaruku katika mahusiano ya Watanzania kuhusu imani zao za dini.
2. Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikitumika kupandikiza udini na ukabila vikidhani vinakisaidia chama fulani kutawala na bila kukemewa na serikali lakini yakitokea matatizo vyombo hivyo pia vitatuhumiwa pamoja na wale wote watakaotuhumiwa kwa kusababisha machafuko nchini - yawe ya kidini, kikabila au kisiasa. Mfano, ni Rwanda: vyombo vya habari vilivyochochea vita, wahariri wao na waandishi wa habari hizo za uchochezi walipata kesi ya kujibu.
Kwa hapa Tanzania, kuna vyombo vinachochea hali kama hii vikidhani vinaishi kwenye sayari tofauti na hii ya kwetu au vinaishi nchi ambazo mkono wa sheria hauwezi kufika.
3. Baadhi ya wanasiasa na hata vyombo vya dola vimesaidia kuwajengea wananchi hofu ya kuzuka vita au umwagaji damu. Wapiga kura wamekuwa wakiambiwa kuwa kuchagua vyama shindani nje ya chama tawala ni kutoitakia nchi mema. Walidhani kufanya hivi ni namna ya kuwafanya wananchi wapige kura kwa uhuru na utashi wao bila kujua kuwa waliwafanya wachague kwa hofu na hivyo kupiga kura bila hiari bali shinikizo. Hiyo ilikuwa 'kuwabaka' wapiga kura kiakili.
4. Siasa za namna hii ni hatari sana. Yaani, ili kupata kura mpaka mtu aseme uongo au aibe kura. Tanzania, tumefikia hapa na mazoea kama haya yanawafanya baadhi ya wananchi waone wale wanaojitahidi kutenda haki kama watu wabaya na wale waongo na wezi wa kura kama watu wazuri. Baadhi ya mijadala hapa JF inaonesha ukweli huu - kwamba mtu akihoji mchakato wa uchaguzi anaonekana mtu mbaya na yule anayekubali au kuhalalisha wizi wa kura kuendelea (kupoteza haki ya kuhoji pale mtu anapohisi kuna ukiukwaji wa haki) anaonekana si mpenda makuu na amekomaa kisiasa. This is rubbish!