Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

We jamaa hauna story zingine nizidi kukufatilia?
Season 2 inakuja, maisha yangu yana matukio hadi nianze kukutana na Mzee, Accountant na Caryn.

Sasa hivi sina maajabu nashinda kutwa nzima kwa nyumba
 
Kwahiyo blaza huja experience chochote side ya Mapenzi nako unipe mawili matatu?
 
Noted mkuu, hii nayo naiongeza kwenye list katika zile Biashara nilizoshauriwa na wadau, kazi yangu kwa Sasa nikuzifanyia upembuzi... shukrani [emoji1545]
 
Na akiongea tu ukweli kwa Mama mkwe basi kazi hana, coz atakuwa kavunja uaminifu wote aliojijengea kwa huyo Bi mkubwa, na pia inaweza kumchafulia Jina kwa yule Mzee
 
Mwanzoni Mzee alitaka kufahamu kama unaweza kufanya biashara
Kwa vile wewe ulivyokua ukitamani mafanikio aliyonayo Mzee

Nimempenda Mzee Kwa sababu reasoning capacity yake ni kubwa kwenye kulea vijana wenye ndoto kubwa,kwanza Mzee anatukumbusha kua hakuna mafanikio Ya kibiashara ambayo hayana risk,pili anatufunza Ili uwe the really business expert ni lazima ujue namna ya kusimamia wazo dogo ulilonalo kulikukuza liwe kubwa na hatimae uishi kwenye ndoto zako

Pia carlyn ni mtoto wa Mzee ambae ni teenage lakini baba ake amemfunza kujiamini,japo kujiamini kwake hakutoshi kama asipopitia mitihani kadhaa (dady anamuandaa mwanae kuwa msimamizi Bora wa kampuni na biashara zake kwani ameona ndiye anaemtegemea Kwa Sasa )

Kuwa makini unapocheza karata zako ukiandaa wazo zuri la biashara na ukaweza kumsimamia dogo vizuri biashara ikakua ndani ya miezi 6
Dogo akawa na uwezo wa kujilipia Kodi ya laki Moja Kwa mwezi Mzee atajua tu unaweza kusimamia kitu na kikawa hivyo ni njia rahisi ya kukuingiza kwenye njia zake

Usimle calyn huu ni ushauri wa Bure nakupa kitendo cha kumla utajiingiza kwenye vita nzito ambayo kutoka itakugarimu sana kumbuka uko kwenye kipimo mkuu

Story ya mafanikio yako inaanzia hapa kwenye kipimo hiki labda kama
STORY IWE YA KUTUNGA
 
una vigingi vi3,,,...but mimi kwa uelewa wangu.......umelengeshwa Caryn........accountant napo kigingi....Annie nae....
ongea na Mungu wako......jipe mda ukae na wote mbali kama 7days.......mbali na hapo ulipopazoea..safiri ukatulie uzicheze karata alone........pia you are good story teller.......
 

Of course, Caryin ndo mtego na mtihani mkubwa kwa sababu wa pesa ameshashinda pale ambako aliruhusiwa kuingia ndani na kutochukua au kuonesha tamaa. Ila hapo naona hata Caryin naye anapimwa kutojiigiza na mapenzi na subordinates.

Hili tunalipata ktk maonyo aliyopewa BM na mzee kule mwanzoni ili aweze kufanikiwa.
 
Mkuu kuhusu yule kijana Sina wasiwasi nae sana, na nishaanza kulifanyia kazi swala lake, ila mtiti unakuja kwa huyo Caryn, inaonekana kama yupo mbele yangu Kuni challenge, unajua nilijiuliza kwanini Mzee asini connect na mwanae Mkubwa ambaye ni Michelle,

Na kuhusu vipimo, una zungumzia vile vitatu ambavyo ni Njaa Tamaa na Upuuzi au?
 
Mawazo yako kama Yana ukweli, unajua Ile siku Mzee alivyonambia kwamba maagizo yote yapo kwa Caryn, nilijiuliza kwanini yeye na sio Dada yake Michelle?
 
Eti ukaachiwa nyumba na funguo chunbani ukaelekezwa ulipo!!!daa
 
Kwasasa Accountant na Caryn nipo nao mbali, labda Caryn ndio nakutana nae japo si mara kwa mara. Annie ndio nipo nae muda mwingi
 
Kwasasa Accountant na Caryn nipo nao mbali, labda Caryn ndio nakutana nae japo si mara kwa mara. Annie ndio nipo nae muda mwingi
kitu ambacho n muhimu pia......kumbumka connection imeanzia kwa accountant.......bado nakushauri kaa na wote mbali......kuna misamiati mingi alikupa mzee baba.....ina vimelea vingi vya uhalisia....
 
Nenda kijijini jisaulishe mambo yote ya mjini kama wiki hivi then utapata jibu
 
Erick shigongo apite hapa kuna mchongo.

Anyway nna swali moja, huyo mzee alikuambia kuhusu mtihani wake kitambo sana akiwa hata hajaandaa content ya mtihani kivipi? Content ya mtihani imekuja coincidently kutoka kwa caryn. Inatia ukakasi kama ina ukweli.

Second doubt ni kwanini mzee asafiri akiwa bado na jeraha la ajali?

Au ni chai mkuu? Kama sio chai, huo ni mtego wa kutest uwezo wako wa kusimamia kitu from scratch na ukakiwezesha kisimame chenyewe. Kabla hujafikiria biashara yeyote inabidi kijana apate training kutoka kwa wazoefu wa hizo biashara unazofikiria. Mjenge awe royal, asiwe mwizi maana kwa nature ya mazingira aliyokulia associates wake ni watoto wa mtaani ambao tayari tabia zao zishaharibiwa na mazingira.

Ukimaliza hayo yote, naomba namba za caryn pm tafadhari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…