[/COLOR]
Ni kweli kabisa. Kuna haja sasa ya hivi vyama vya siasa kuunganisha nguvu. Kuna maeneo ambayo wangeweza kushinda vizuri sana lakini wameishia kugawana kura na hivo kuipa ushindi CCM. Mfano mzuri ni Tarime.
Tatizo ni kwamba nani ahamie kwa mwingine lakini naona kinachowaumiza kichwa ni swala la ruzuku, uchu wa madaraka na ubinafsi uliojikita kwa vingozi wa vyama hasa hivi vyama vidogo pia. Kuna vyama kama TLP, Jahazi Asilia, PPT, UPDP, NRA na vinginevyo ambavo hata udiwani havijapata, ingekua busara sasa kwa vyama kama hivo kuunganisha nguvu na kuunda chama kimoja ambacho kitakua na nguvu lakini pia uzoefu wa kisiasa haswa ukizingatia kwamba tayari wameshashiriki uchaguzi mara kadhaa na wameona hali halisi. Sioni busara ya kuendelea kukaa kwenye chama ambacho kwa mara nne mfululizo katika uchaguzi mkuu wanashindwa hata kupata mbunge mmoja au hata asilimia 3% ya kura zote zinazopigwa na wananchi.
Ni busara sasa kwa viongozi wa vyama kuondoa aibu na ubinafsi sasa na kuona wataweza vipi kuunganisha utaalam, uzoefu, rasilimali ili kuleta mapinduzi ya kweli dhidi ya CCM.