KERO Hatma ya Vijana Wetu na Juhudi za Kukomesha Uvutaji Bangi Hadharani: Hili Ni Tatizo la Nani?

KERO Hatma ya Vijana Wetu na Juhudi za Kukomesha Uvutaji Bangi Hadharani: Hili Ni Tatizo la Nani?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kama mkazi wa mtaa wa Msisiri A, nyuma ya Mahakama ya Kinondoni, nimesikitishwa mno kuona idadi kubwa ya vijana wadogo wakijihusisha na uvutaji wa bangi maeneo ya wazi. Wanavuta bila hofu, bila kujali athari za kiafya kwao binafsi na kwa wakazi wengine wa mtaa huu. Hii ni hali inayotufanya tujiulize, ni wapi jamii yetu imekosea?

Swali linabaki, je, jamii imeshindwa kuwalea vijana wake? Inaonekana kama tumekubali hali hii kuwa ya kawaida, kana kwamba hakuna njia ya kuizuia. Hata pale ambapo serikali hujaribu kuingilia kati kwa kuwakamata vijana hawa, si mara moja wala mara mbili ambapo tunashuhudia wakiachiliwa baada ya muda mfupi kwa sababu ya mlungula.

Hali hii inazua maswali mengi kuhusu usimamizi wa sheria zetu za kupambana na mihadarati. Je, sheria inashindwa kutekelezeka ipasavyo, au kuna mianya inayotumika kuwarudisha mitaani wale wanaopaswa kuwajibishwa?

Ni muhimu tukafahamu kuwa uvutaji wa bangi si tatizo linalowaathiri tu vijana wanaovuta, bali linaathiri pia jamii nzima. Siku baada ya siku, mtaa unaharibika, na kizazi kijacho kinapata mfano mbaya wa kuiga.

Wakati umefika kwa serikali, jamii, na wadau wote kuweka nguvu za pamoja kuhakikisha tatizo hili linashughulikiwa kwa ufanisi na kizazi kijacho kinapata malezi bora. Ni wakati wa kuchukua hatua thabiti, na tusikubali hali hii kuwa ya kawaida tena.
 
kuna mwamba kipind nko form 3 tulikuaga tunavuta mtaan hatuogop usela mwingi yule doni akaenda obey kawapa hela sjui aisee miez mwili doria mtaan hadi vijiwe tukahamaga
 
Bi mkubwa,...tusamehe tu wanao, si unajua tena life....
 
Back
Top Bottom