Frajoo
Member
- May 28, 2024
- 12
- 3
Baada ya kutumikia umma kwa miaka mingi na kufikia umri wa miaka Sitini, mfanyakazi alitoa mchango kwa taifa letu huitwa mstaafu. Anaacha kazi na kurudi kwenye jamii akiwa hoi kama sio hai ya kusuasua.
Japo sina ufahamu mkubwa kuhusu sheria taratibu na kanuni za utumishi wa umma, hivyo pengine nisijue hata changamoto ambao serikali yetu sikivu inapitia katika mchakato wa kuhakikisha kila mstaafu anapata stahiki yake, yaani kwa nchi nzima na kwa kada zote. Lakini yaliyonisukuma kuandika matamanio yangu juu ya Tanzania ninayotaka kuiona ni hali halisi ya maisha ya wastaafu na familia zao wakiwa na miaka Sitini na kuanza kukutana na changamoto mpya.
Awali ya yote nadhani umri wa kustaafu ungerudishwa nyuma kidogo au kupunguzwa, badala ya miaka Sitini (60) ni kufikia angalau miaka Hamsini (50) kwasababu mbalimbali.
Sababu ya kwanza ni weledi wa kazi, ni wazi kabisa binadamu anakuwa mwenye nguvu zaidi katika umri wa ujana, kadri umri unavyoongezeka umakini, wepesi wa kutekeleza majukumu, ubunifu, ustahimilivu wa changamoto na ushirikiano na wengine hupungua. Hivyo basi mfanyakazi akifikia umri wa miaka 50 na kuendelea bilashaka hawezi kufanikisha majukumu kwa weledi aliokuwa nao akiwa na miaka 30 hadi 40, kwasababu mtu huyu kachoka akili hadi mwili ni uzoefu tu ndio utakuwa unamsaidia kitu ambacho hakisaidii sana ustawi wa taifa lolote, maana dunia ya leo inahitaji ubunifu unaotokana na udadisi na ushirikiano na wengine.
Jambo la Pili ni kupisha vijana wakae kwenye nafasi hizo mapema ili angalau kupunguza (japo kwa kiasi kidogo) tatizo la ukosefu wa ajira.
Pia kuandaa Hatma njema kwa wastaafu kwenye maisha baada ya ajira. Mfanyakazi anatumika Serikalini zaidi ya miaka 20, ikiwa ndio sehemu ya maisha yake, kwa maana kwamba kwanzia asubuhi hadi jioni anakuwa eneo la kazi. Mtu huyu hawezi kujihusisha na mambo mengine labda kama nae kaajiri mtu au watu. Namtazama zaidi mfanyakazi ambaye ana majukumu ya familia kubwa, ikijumuisha kusomesha watoto, kulea ndugu na kuhakikisha anasukuma maendeleo ya familia yake ili apate kuishi maisha bora.
HALI ILIVYO KWENYE JAMII.
Mstaafu mara anapoacha kazi rasmi tu, ndipo anaanza kuwaza kuhusu kuwekeza au kufanya biashara. Sote tunajua biashara sio kitu cha kilamtu, biashara nayo inamtaka mtu mwenye uzoefu, mwenye mapokeo chanya pale inapotokea hasara, mwenye uvumilivu wa kuokota matunda ya biashara taratibu na sio papo hapo uanze kuona matunda ya uwekezaji. Kitu ambacho kwa mstaafu huwa ni mtihani mgumu sana, ukizingatia anakutana na ushindani kutoka kwa wabobezi kwenye biashara au uwekezaji huo. Matokeo yake ni msongo wa mawazo, ikumbukwe hata kwenye jamii anaanza kutoaminika anapohitaji mikopo.
Jambo lingine ambalo ni changamoto kwa wazee hawa ni afya ya mwili na hata ya akili. Kiuhalisia binadamu akifikisha miaka 60 hata kinga yake ya mwili inakosa nguvu, hivyo hushambuliwa na magonjwa kwa urahisi. Ukijumlisha na changamoto za uchumi usio wa uhakika hupata matatizo ya afya ya akili na magonjwa ya moyo, kisukari. Hapo tunaona kuna bajeti kubwa kwenye matibabu ya wastaafu.
Kwa tafsiri hii ni kwamba hatma ya wastaafu si njema, wanaishi kwa mashaka, majuto na lawama. Hapo hapo watoto na ndugu hukimbilia kwa wastaafu kuomba mitaji na fedha za kujikwamua wakiamini wazee wamepata fungu kubwa la kustaafu na pensheni juu.
Kwa utafiti wangu nimegundua asilimia kubwa ya wastaafu hawakujenga kipindi wapo Serikalini, kwahiyo baada ya kustaafu ndipo huanza kujenga. Hapo nadhani tumepata picha halisi jinsi maisha ya wastaafu yanapoishia vibaya. Ni asilimia chache tu wanaoishia vizuri ni wale waliokuwa na nyadhifu za juu na wakajenga na kufanya maendeleo wakiwa kazini, lakini wengi wao huishia mateso.
Kwenye mapendekezo yangu lipo jambo lapili ambalo ni kuhusu fedha wanazopata wastaafu.
KIKOKOTOO KIPYA. (33%)
Wastaafu wengi wanalalamika kuhusu malipo yao ya kustaafu, kama nilivyosema awali sijui kiundani changamoto ambazo Serikali yetu sikivu inapitia kuhakikisha kundi hili linapata ahueni ya maisha baada ya ajira. Lakini wastaafu wanasema zamani ilikuwa nafuu zaidi ukilinganisha na hali ya sasa.(Ilikua ni 50%)
Kwenye mfumo mpya wameamua kuwapa fedha kiasi (kidogo zaidi ya miaka ya nyuma.) lakini wastaafu wanapokea mshahara waliokuwa wanapokea wakiwa kazini kwa muda wa miaka 12, kisha zoezi la kuwalipa linaishia hapo. (Kitaalamu hii ilivyokaa ni kama wameangalia Lifespan ya mwanadamu kuishi ni miaka 70, baada ya hapo kifo kipo jirani zaidi.)
Sawa,pengine walifikia muafaka huu baada ya kuangalia changamoto za maisha na lengo ni kuwafanyia wepesi wa maisha.
Lakini kama tulivyoona hapo juu mabadiliko ya mfumo wa maisha kutoka kuwa mfanyakazi na kuwa mjasiriamali au mkulima ni changamoto kubwa sana. Mathalani Mwalimu aliyekuwa anastahili kupokea Milioni Mia moja na zaidi baada ya kustaafu, leo hii kwa mujibu wa kikokotoo kipya anapokea Milioni 60 wengine kwenye kada zingine hadi Milioni 40 hasa ukizingatia wazee wengi ni darasa la Saba au alijiongeza kupata cheti cha kidato cha kidato cha nne.
Hapo hajajenga wala hana uwekezaji wowote kama kitega uchumi, ndio kwanza anaanza kuhangaikia. Watoto na ndugu wanategemea hapo bado kuna kujiuguza.
Ninachokiona kwenye jamii wazee wanamalizia fedha zao za pensheni kwenye madawa na vituo vya afya. Mtu anapostaafu fedha zake kiasi zinaambatana na Magonjwa ya moyo, kisukari miguu na uti wa mgongo pasi na kufuta jasho lake alilotoa kwa miaka zaidi ya 20 na uwezo wa kupata matibabu yenye viwango bora hana.
Sasa basi natamani kuona wastaafu wanaboreshewa malipo yao. Kuhusu kucheleweshewa mafao si jambo la kusisitiza sana maana sitegemei iwe ni kawaida kama huwa inatokea basi ni mapungufu tu ya watekelezaji. Pia ni heri kuwapa fungu kubwa ili wajenge na kufanya uwekezaji wa uhakika ili kumudu changamoto mpya za maisha. Maana kuwalipa kidogo jumlisha mshahara uleule hakuna mabadiliko chanya wanaweza kuyafanya. Hii ni kwa pande zote yaani makubaliano kati ya Serikali kuu na Mifuko yakijamii yaani PSSSF na NSSF. (Lazima mjadala uanzie bungeni ili kupitisha kwa watunga sera na wafanya maamuzi, kulingana na Sheria za nchi.
Tafadhali tuwaoneshe vijana kwamba kuna faida ya kuhudumu serikalini, na watumishi wajisikie fahari kuwa chachu ya ujenzi wa taifa letu teule.
Hata kama sifahamu kiundani kuhusu Sheria, taratibu na kanuni zote za utumishi wa umma lakini hainizuii matamanio yangu ya kuona Sekta binafsi pia kuwekewa sheria za kuwalipa mafao wastaafu kwenye mashirika, makampuni na uwekezaji wao. Hii ni kwa kila muajiri anapomtumikisha mtu kwa miaka kadhaa basi kuwe na utaratibu wa kustaafu pia na kulipwa kulingana na kikotoo ambacho serikali itakiandaa maalumu kwa sekta binafsi.
Asante sana kwa muda wako.

Upvote
3