Jpinduzi
Senior Member
- Feb 26, 2011
- 136
- 68
- Hatua ya kuamua kuingia katika biashara
- Hatua ya kuchanganua uwezo na udhaifu wako
[TD="width: 197, bgcolor: #EEEEEE"] Mazingira wezeshi [/TD]
[TD="width: 197, bgcolor: #EEEEEE"] Mazingira pingamizi [/TD]
[TD="width: 197, bgcolor: #EEEEEE"] Mazingira ya Ndani [/TD]
[TD="width: 197, bgcolor: #EEEEEE"]
UwezoUwezo wako katika kuendesha biashara mfano: utaalam, vitendea kazi, kiwanja nk.
[/TD][TD="width: 197, bgcolor: #EEEEEE"]
UdhaifuUdhaifu wako katika kuendesha biashara mfano: ukosefu wa utaalam, vitendea kazi, kiwanja nk.
[/TD][TD="width: 197, bgcolor: #EEEEEE"] Mazingira ya Nje [/TD]
[TD="width: 197, bgcolor: #EEEEEE"]
FursaKuwepo kwa sera nzuri, katiba nzuri, hali ya hewa nzuri, mwitikio wa jamii nk
[/TD][TD="width: 197, bgcolor: #EEEEEE"]
VitishoKutokuwepo kwa sera nzuri, katiba nzuri, hali ya hewa nzuri, mwitikio mbaya wa jamii nk
[/TD]- Hatua ya kupata mafunzo
Mfano:- Ya kupata ufundi au kubadili mitizamo
Kupata utaalam wa kiufundi katika biashara husika
- Hatua ya kupeleleza mazingira utakayofanya biasha ili kujua:
ii) Vitisho au hatari zitakazoikabili biashara yako (vihatarishi vya biashara husika kama vile sera mbovu, barabara mbovu, hali ya hewa mbovu nk)
- Hatua ya kuchagua biashara gani ufanye
ii) Kuuza bidhaa (Trading)
iii) Kutoa huduma (Service)
Kutengeneza bidhaa (Manufacturing)
Kutengeneza bidhaa ni kutumia rasilimali watu na malighafi ili kutengeneza bidhaa ya kuuza kwa mlaji au mchuuzi. Bidhaa ni kama vyakula, vyombo, nk
Kuuza bidhaa (Trading)
Kuchuuza bidhaa zilizotengenezwa hapo juu no. A(a)
Kutoa huduma (Service)
Kutumia ujuzi wako au wa wengine katika kuwahudumia watu na shida zao kwa malipo. Mfano kufundisha, kutibu, kusafirisha, kutumbuiza nk
- Hatua ya utafiti wa soko (Market Survey)
ii) Mgawanyo wa soko
iii) Aina ya soko/masoko
iv) NK
- Kuamua aina ya mfumo wa biashara utakayofanya
i) Mtu mmoja (sole proprietor)
Faida yake
Kuanzisha ni rahisi
Maamuzi hupitishwa kwa haraka kwa hiyo hakuna urasimu
Hasara yake
Biashara ikipata shida mmiliki anahusika na hasara kama vile ya ufilisi nk
ii) Ushirika (>watu wawili) (partnership)
Faida yake
Kuanzisha ni rahisi
Maamuzi hupitishwa kwa haraka kwa hiyo hakuna urasimu
Hasara yake
Biashara ikipata shida wamiliki wanahusika na hasara kama vile ya ufilisi nk
Mikataba inayoingiwa na mmoja wa washirika huwabana na wengine wasiohusika
iii) Kampuni ya umma au mashirika ya umma (public companies)(zaidi ya watu wawili bila kikomo)
Faida yake
Utambulisho wa kisheria
Ukomo wa ufilisi upo kwenye kampuni husika na sio wenye hisa
Ni rahisi kuvutia mitaji mikubwa kupitia masoko ya hisa
Hasara yake
Haina usiri hivyo ni hatari kwani washindani wa biashara husika wanaweza kutumia taarifa hizo kujipanga
Muda na rasilimali muda kupotea kwa shughuli za kihasibu na kazi za makaratasi
iv) Kampuni ya binafsi yenye ukomo wa hisa (private companies limited by shares) (watu wawili hadi 50)
Faida yake
Utambulisho wa kisheria
Ukomo wa ufilisi upo kwenye kampuni husika na sio wenye hisa
Kazi za makaratasi ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma
Mlolongo wa taratibu za kisheria ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma
Hasara yake
Gharama katika kuanzisha tofauti na biashara binafsi
Huruhusiwi kuuza hisa katika masoko ya hisa
Kampuni li lazima angalau iwe na wakurugenzi, katibu na mhasibu
Ni lazima ifanyiwe ukaguzi wa mahesabu kila mwaka
v) Kampuni ya binafsi yenye ukomo wa udhamini (private companies limited by guarantees) (watu wawili hadi 50)
Faida yake
Utambulisho wa kisheria
Ukomo wa ufilisi upo kwenye kampuni husika na sio wenye hisa
Kazi za makaratasi ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma
Mlolongo wa taratibu za kisheria ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma
Hasara yake
Gharama katika kuanzisha tofauti na biashara binafsi
Huruhusiwi kuuza hisa katika masoko ya hisa
Kampuni li lazima angalau iwe na wakurugenzi, katibu na mhasibu
Ni lazima ifanyiwe ukaguzi wa mahesabu kila mwaka
vi) Jumuiya (association)
Faida yake
Utambulisho wa kisheria
Inavutia wahisani
Ni ya watu wachache waliokubaliana
Hasara yake
Ukiritimba katika kupitisha maamuzi
Ugomvi wa mara kwa mara
Haina kinga kwa waazilishi
vii) Vyama vya ushirika
Faida yake
Utambulisho wa kisheria
Inavutia wahisani
Ni ya watu wachache waliokubaliana
Hasara yake
Ukiritimba katika kupitisha maamuzi
Ugomvi wa mara kwa mara
Haina kinga kwa waazilishi
viii) Mashirika yasiyo ya kiserikali
Faida yake
Utambulisho wa kisheria
Inavutia wahisani
Ni ya watu wachache waliokubaliana
Hasara yake
Ukiritimba katika kupitisha maamuzi
Ugomvi wa mara kwa mara
Haina kinga kwa waazilishi
- Ukishachagua mfumo mzuri wa biashara yako, unatakiwa kuanza mchakato wa kuisajili katika mamlaka ya usajili wa makampuni inayoitwa BRELA ambayo ofisi zake zipo Jengo la shirika Dar es salaam
- Hatua ya kuchagua sehemu ya biashara
- Hatua ya kuchagua technolojia
a) Aina ya watumishi
b) Aina ya vitendea kazi mashine /mitambo
Mfano kilimo cha maksai na kukamua kwa mashine
ii) Teknolojia nzuri ni lazima iwe na sifa zifuatazo
a) Ni rahisi kutumiwa
b) Iwe rahisi kupata msaada kama mafundi nk
c) Iwe inaendana na tamaduni husika
d) Iwe ni rafiki wa watu na mazingira
e) Iwe na gharama ndogo za uendeshaji
f) Inaendelezeka
- Hatua ya kununua mashine na vifaa
Mashine zote na mitambo ni lazima kuzingatia yaliyotajwa hapo juu 8(ii)
- Hatua ya usajili wa biashara
- Hatua ya kuandika Mchanganuo wa Biashara (Business Plan)
- Baada ya kufanya hayo yote sasa ni wakati mzuri wa kuandika mchanganuo wa biashara yako
- Mchanganuo wa biashara ni maelezo ya kina ambayo inaonyesha biashara yako ilikotoka, inakokwenda, hali ya masoko, sekta, kifedha na uongozi wa biahara yako. Ni taarifa muhimu ya kuwavutia wawekezaji na watoa mikopo kama mabenki
- Muhtasari wa biashara yako
- Historia na maelezo ya biashara yako
- Maelezo ya bidhaa au huduma ya biashara yako
- Mchanganuo wa masoko
- Ukubwa wa soko
- Mgawanyo wa soko
- Aina ya soko/masoko
- Mchanganuo wa ushindani
- Watoa huduma au wauza bidhaa kama yako
- Udhaifu wao
- Uwezo wao
- Mkakati wa utekelezaji
- Uongozi na usimamizi wa kazi
- Uchambuzi wa madhaifu, nguvu, fursa na hatari zinazokabili biashara yako
- Mkakati wa Uzalishaji
- Mkakati wa kuuza
- Mpango wa fedha
- Uchambuzi wa mahitaji ya mtaji
- Wapi utatoa mtaji
- Matumizi ya mtaji
- Makisio ya Mauzo
- Uchambuzi wa kurudisha gharama (break even analysis)
- Makisio ya faida au hasara
- Makisio ya mzunguko wa fedha katika biashara yako (cashflow)
- Makisio ya oanisho la mali na madeni ya biashara yako (balance sheet)
- Ulinganifu wa sehemu mbalimbali za biashara (business ratios)
- Viambatanisho
i. Lesseni
ii. Cheti cha ulipaji kodi
iii. Cheti cha usajili
iv. Taarifa mbalimbali za biashara yako ambazo hazikupata nafasi ndani ya mchanganuo huu
v. nk
- Hatua ya kupanga juu ya pesa.
Taasisi nyingi huhitaji yafuatayo
- Dhamana ya mkopo
- Uzoefu wa biashara husika
- Mchanganuo wa biashara
- Maombi ya mkopo
- Hatua ya ufahamu wa kiufundi.
- Hatua ya kujua vyanzo vya nishati:
Kama ni mafuta uhakikishe mafuta inapatikana na bei haitaadhiri bei ya bidhaa
- Hatua ya kuweka vifaa: (Machines installation)
- Hatua ya kuajiri wafanyakazi.
Unashauriwa pia kutumia marafiki na ndugu wa karibu ili upate mfanyakazi ambaye ni bora zaidi
- Hatua ya kujua upatikanaji wa malighafi
- Hatua ya uzalishaji mali
ii) Kuanza biashara rasmi
- Hatua ya kuhakikisha bidhaa yako hainakiliki
ii) Tunza vizuri siri zingine za biashara yako
- Usalama wa biashara yako
- Hatua ya kuuza (Selling)
- Kusambasa huduma/bidhaa
- Kuweka bei
- Kutangazia biashara
- Promosheni nk.
- Hatua ya Utafiti wa soko (Market Research)
- Kujua biashara yako imekamata asilimia gani katika soko
- Kupata maoni ya wateja ili kuboresha biashara/huduma/bidhaa
Namna ya kufanya utafiti
i) Utafiti wa kuendelea
Kila mteja anaponunua bidhaa, ajaze fomu maalum ya maoni. Mfano ya jinsi alivyohudumiwa, bei ya bidhaa, usindikaji, ubora nk
ii) Utafiti maalum
Huu ufanywe wakati wa kutoa vivutiuo maalum au promosheni maalum.
Mteja wa promosheni ajaze fomu maalum ya maoni. Mfano ya jinsi alivyohudumiwa, bei ya bidhaa, usindikaji, ubora nk
- Hatua ya kusimamia na kuthibiti biashara:
- Hatua ya kutathmini biashara.
Mambo ya kuangalia
- Mapato na matumizi
- Bajeti iliyiopita
- Matokeo ya utaifit/wa soko
- Hatua ya kufanya maboresho/mabadiliko
Fanya sawa sawa na matokeo ya tathmini/utafiti