Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Mapenzi hayana bima wala hayana formula maalumu ambayo kila mtu anaweza kuitumia na kupata matokeo yenye kufanana.
Unaweza kutengana na mwenza wako saa yoyote,muda wowote bila kujali uwekezaji wako kwake.Hauwezi kudumisha mahusiano kama mwenza wako ameamua muachane.Utadumu na mwenza wako pale ambapo kila mmoja anatimiza majukumu yake kuhakikisha mnakuwa pamoja.
Soma ujumbe mpaka mwisho.
Watu wengi hivi sasa wamekata tamaa ya kupenda tena au kuamini tena wanawake au wanaume kwa sababu za kumbukumbu za kusalitiwa,kuachwa ghafla bila matarajio yoyote baada ya kuwekeza fedha, matumaini,malengo na matarajio mengi sana kwa wenza wao.
Leo tuangalie hatua 3 za kumsahau mwanamke au mwanaume ambaye amekuacha ukiwa ukiwa na kinyongo moyoni na imekuwa ngumu sana kuamini tena wanawake au wanaume kisha utaweza kujua hatua za kujenga mahusiano mapya mazuri yenye furaha na amani tofauti na huko nyuma.
Kabla ya kujua hatua hizo tuangalie viashiria vya mahusiano kuvunjika kisha tuangalie maumivu makali sana baada ya mahusiano kuvunjika kisha tuangalie makosa ambayo watu wengi hufanya kisha tuangalie hatua sahihi za kujenga mahusiano mapya mazuri yenye furaha na amani tofauti na awali.
VIASHIRIA VYA MAHUSIANO KUVUNJIKA
Kabla ya mahusiano kuvunjika utaona viashiria vifuatavyo kutoka kwa mwenza wako.
1.MAWASILIANO KUPUNGUA
Mahusiano yakiwa karibu kuvunjika utaona kwamba unatumia nguvu nyingi sana kumlazimisha mwenza wako apokee simu na kujibu sms lakini anakuwa mkali kupita kiasi,au anakaa kimya sana bila taarifa yoyote.
Utaona unatuma sms mfululizo,kupiga simu mfululizo lakini haonyeshi ushirikiano wowote, vilevile anaweza kukujibu vibaya, kukosoa kupita kiasi, kukufokea, kukutukana, kukupa vitisho,kuzima simu,mara kwa mara simu haipatikani, sms hazijibiwi na hatoi majibu yoyote kuhusu ukimya wake au anatumia muda mwingi sana kujibu sms hata kama sms za watu wengine anajibu haraka, vilevile ukipiga simu namba mpya anapokea lakini akijua ni wewe anakata simu au kutafuta dharura ya kukata simu.
2.UNATUMIA FEDHA NYINGI SANA ILI KUMFURAHISHA
Kama mahusiano yako na mwenza wako yanakaribia kuvunjika utaona unatumia fedha nyingi sana ili kumfurahisha mwenza wako lakini haonekani kushukuru badala yake anakuwa na hasira kupita kiasi kwa kiasi cha fedha ambacho umetoa.
Mara kwa mara atakwambia wewe ni mchoyo sana, mbinafsi,bahili sana na atakuwa anatishia kuvunja mahusiano ikiwa huwezi kumpatia kiasi fulani cha fedha ambacho huna uwezo nacho.
3.KULAUMIANA SANA
Kama mahusiano yako na mwenza wako yanakaribia kuvunjika utaona mnapeana lawama mara kwa mara kwa vitu vidogo vidogo sana ambavyo havina msingi wowote.
Utaona mnatumia muda mrefu sana kugombana mara kwa mara,kupishana kauli kwa vitu vidogo vidogo,kubaki na hasira kupita kiasi baada ya mazungumzo na mwenza wako.
4.KUKUMBUKA MABAYA YAKE KULIKO MAZURI YAKE
Kama mahusiano yako yanakaribia kuvunjika utaona upo na kumbukumbu mbaya sana za mwenza wako kuliko mazuri yake.
Mara kwa mara utakuwa huna kumbukumbu lini umeona tabasamu lake,lini umeongea nae kwa furaha,lini umekaa nae pamoja na kuzungumza kwa furaha.
Badala yake utakuwa na kumbukumbu za matukio mbalimbali kama kumfumania, kuvumilia matusi, vitisho, vipigo, lawama, kufokewa, kudhalilishwa,kukaa kukupa mapenzi,ametumia fedha zako nyingi sana bila ridhaa yako,utakumbuka umewahi kuugua lakini hajaonesha kujali chochote lakini yeye alipokuwa na matatizo umejitoa sana , utakumbuka hajawahi kukushukuru kwa chochote, utakumbuka hasira zake, utakumbuka umevumilia tabia zake zenye maudhi zenye kujirudia rudia, utakumbana anakumbusha makosa ya zamani mara kwa mara,kila siku anakuwa mkali kupita kiasi,anakuwa na dharura ya kuondoka kukwepa mazungumzo,akifanya makosa haombi msamaha, anageuza kibao kwako kwa makosa yake,
5.MAHUSIANO KUENDESHWA NA JUHUDI ZAKO TU
Utaona ni wewe ni ambaye unataka kujenga ukaribu na ndugu zake pamoja na wazazi wake lakini yeye kwako anakuwa na hasira kupita kiasi, dharura mbalimbali, kubadilika badilika,kukosa msimamo.
Utaona unajitoa sana kwake na kwa ndugu zake lakini yeye haonyeshi ushirikiano wowote kuhusu matatizo yako.Utaona anatoa majibu ya mkato, kukaa kimya muda mrefu sana,kuibua ugomvi kwa vitu vidogo vidogo sana,anaondoka unabaki na hasira kupita kiasi lakini hajali chochote.
BAADA YA MAHUSIANO KUVUNJIKA UTAONA MABADILIKO YAFUATAYO MWILINI MWAKO
Baada ya mahusiano kuvunjika utaona mabadiliko yafuatayo mwilini mwako
a.Kupata hasira kupita kiasi,kupata uchungu mkali sana moyoni, kichefuchefu, miguu kuishiwa nguvu, tumbo kuvurugika, moyo kwenda mbio sana, kizunguzungu, kuweweseka, kuumwa kichwa na mgongo, kukosa nguvu za kutoka kitandani,
b.kupoteza hisia za mapenzi, kujichukia kupita kiasi,kujiona mpweke sana, kujiona upo hatarini muda wote,kujiona hauna thamani,kujiona mbaya sana, kuuchukia muonekano wako,kuumia kooni, kutetemeka sana, kutokwa jasho viganjani, kutamani kumdhuru,
c. kumuombea mabaya sana,kuwachukia wanaume au wanawake wote, kubanwa na choo ghafla, uchovu mwili mzima, kuanza kulia,kuanza kujitenga na jamii, kupaniki sana, kuchanganyikiwa,kuhisi unataka kurukwa akili, kuhisi unataka kudondoka ghafla, kuhisi unataka kufa ghafla, kuhisi baridi ghafla,kuona aibu,
d.kuona ukungu,hofu ya kukosolewa, hofu ya kuonekana kituko,kukosa umakini,kulala popote, kulala sana mpaka unachoka au kukaa kitandani bila usingizi muda mrefu, kukonda sana ghafla au kunenepa kupita kiasi ghafla, kupoteza hamu ya kula au kula vyakula bila mpangilio.
MAKOSA AMBAYO WATU WENGI HUFANYA PALE MAHUSIANO YAMEVUNJIKA
Watu wengi hufanya makosa yafuatayo baada ya mahusiano kuvunjika
a.Kuamini hawawezi kupata mwenza mzuri zaidi ya huyo wa zamani, kuamini wataishi maisha ya upweke milele,kutaka kujenga ukaribu
b. kutaka maelezo ya kwanini mwenza wake amevunja mahusiano kitendo hicho cha kutaka kupewa maelezo ya mahusiano kuvunjika huzidisha maumivu makali sana moyoni na hasira kupita kiasi kwa sababu mwenza huyo hawezi kutoa majibu yenye kuridhisha
c.Kutaka kujenga nae urafiki haraka sana baada ya mahusiano kuvunjika, kujaribu kusahau maumivu na kumbukumbu zenye kuhuzunisha
d.Kumchafua kwenye mitandao, kutafuta mwanaume au mwanamke mwengine wa kuziba pengo haraka , kuendeleza mawasiliano husababisha kujipa matumaini ya kurejesha mahusiano kama zamani jambo ambalo husababisha maumivu makali sana.
e.Kujitenga, kujilaumu,kujuta, kujikosoa, kumuombea mabaya,kulipa kisasi,kumchukia mwenza baada ya mahusiano kuvunjika
f.Kujisifia kwenye mitandao au mtaani kuwa maisha yamekuwa mazuri sana kuliko zamani akiwa na mwenza huyo.
UFUMBUZI WAKE
Kwanza kabisa unatakiwa kujua mahusiano kuvunjika ni kama msiba wa mtu unaempenda sana hivyo lazima ujipe muda wa kuomboleza kinyume chake huwezi kujenga mahusiano mapya na mtu yeyote zaidi utaishia kuumizwa tena na tena mpaka utakata tamaa moja kwa moja.
Fuata hatua zifuatazo
1.PATA UTULIVU WA AKILI
a.Fuata hatua zifuatazo
Vuta pumzi taratibu taratibu kisha anza kuvuta pumzi ndefu sana kupitia puani, zuia pumzi kifuani kisha hesabu 1-5 kisha ruhusu pumzi itoke polepole huku unahesabu 1-5 ,fanya zoezi hilo kwa dakika 5
b.Vuta pumzi kupitia mdomoni na kuitoa pumzi haraka haraka kupitia mdomoni pumua haraka haraka sana kama Bata,kisha unaweza kupiga miayo mfululizo (Yawning),
2.WEKA MIPAKA
Tambua kwamba mahusiano kuvunjika ni jambo la kawaida na hakuna binadamu yeyote duniani ambaye yupo na guarantee ya kudumu katika mahusiano.
Huna kitu kipya cha kumpa mwenza wako ambacho watu wengine hawana uwezo wa kumpa ,hata kama unaona upo vizuri sana kitandani bado kuna watu wapo vizuri zaidi yako,kuhusu fedha huna fedha nyingi kuliko watu wote duniani,kuhusu muonekano wako huna muonekano mzuri sana kama unavyoweza kujiaminisha maana yake wazuri zaidi yako wapo wengi sana,kuhusu tabia njema huwezi kuvunja rekodi ya kuwa mtu mwenye maadili mema kuliko watu wote duniani.
Hivyo chochote ambacho unaona cha kipekee watu wengi sana wapo nacho na wanaweza kumfanyia mwenza wako. Ukiona mtu amekaa na mwenza wake miaka mingi sio kwamba yeye ni mtaalamu sana bali ni maamuzi tu ya mwenza wake.
Tambua tabia gani huwezi kuvumilia kutoka kwa mwenza wako mpya ,epuka kujitoa mhanga mpaka kuhatarisha maisha yako kwa sababu ya mapenzi,epuka kuchukua mikopo kwa ajili ya mwenza wako ili kuonyesha kwamba unampenda sana ikiwa yeye hawezi kufanya hivyo kwako kwa sababu watu ambao unajitoa mhanga kwao wanakuona huna pa kwenda wala sio kukuona mwema kwao.
Tumia akili katika mahusiano sio hisia kwa sababu unaweza kuhatarisha maisha yako kisa mapenzi lakini mwenza wako hawezi kufanya hivyo.
Epuka kuwekeza fedha nyingi sana kwa mwenza wako ikiwa yeye hawezi kufanya hivyo kwako,ukimpa zawadi mwenza wako hakikisha unatumia thamani hiyohiyo kujali mahitaji yako kwa mfano umetoa zawadi ya 10000 na wewe tumia 10000 kwa ajili yako.
Hakikisha akiwa na matatizo beba matatizo kulingana na uwezo wako sio mahitaji yake kwa sababu binadamu hawezi kutosheka kwa kitu cha kupewa.
3.MATATIZO YAPO KWA WATU WOTE DUNIANI
Mahusiano kuvunjika yanaweza kuvunjika muda wowote bila kujali wewe ni mchamungu au mshirikina, mwema au muovu, muaminifu au msaliti, mwenye huruma sana au mchoyo sana,tajiri au maskini, msomi au haujafika shule.
Hakuna bima ya mapenzi hivyo epuka kuwekeza fedha nyingi sana, nguvu nyingi sana,kwa mwenza wako ikiwa yeye hawezi kufanya hivyo kwako.