Hatua 5 za kuanzisha biashara ya mikopo ya ukarabati wa majengo ya kupangisha mwaka 2022

Hatua 5 za kuanzisha biashara ya mikopo ya ukarabati wa majengo ya kupangisha mwaka 2022

Aliko Musa

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2018
Posts
209
Reaction score
315
Mikopo ya ukarabati wa nyumba ni moja ya njia za kutengeneza fedha kupitia uwekezaji wa nyumba za kupangisha unaoweza kujenga utajiri mkubwa.

Katika kila halmashauri kuna nyumba za kupangisha. Nyumba zinaweza kuwa ni nyumba za makazi, nyumba za matumizi mseto (mixed-use properties) na nyumba za biashara.

Sababu Za Kutoa Mikopo Ya Ukarabati Wa Majengo Ya Kupangisha.

Moja.

Kupato endelevu fha kila mwezi.

Nimelenga kwenye nyumba za kupangisha kwa sababu ndio njia inayoingiza kipato endelevu cha kila mwezi. Hivyo itakuwa rahisi kuendelea kukusanya marejesho ya mikopo kutoka kwa wenye nyumba.

Mbili.

Idadi kubwa ya wawekezaji.

Kwa mazingira yetu ya Tanzania, kuna idadi kubwa ya wawekezaji kwenye nyumba za kupangisha kuliko wawekezaji kwa kununua na kuuza nyumba ndani ya miaka miwili (2) tu.

Hii itaifanya biashara yako ya mikopo ya ukarabati na maboresho ya nyumba za kupangisha iwe endelevu. Hivyo kila mwezi utaendelea kuingiza kipato kutokana na marejesho ya wakopaji.

Tatu.

Uwezo wa kusoma hali ya soko la nyumba za kupangisha.

Inawezekana kabisa kusoma hali ya masoko ya nyumba za kupangisha kwenye halmshauri unapokopesha mikopo ya ukarabati na maboresho ya nyumba.

Nne.

Ni rahisi mikopo kutumika kwa ajili lengo kuu.

Hii ni pale ambapo utakuwa unatoa vifaa, samani (furnitures) na malighafi ya ukarabati na maboresho ya nyumba za kupangisha.

Wamiliki wa nyumba hawataweza kutumia mikopo kwa ajili ya chanagamoto zao binafsi za kifedha badala ya ukarabati na maboresho.

Unaweza ukaenda mbali na kuwa msimamizi wa ukarabati na maboresho ya nyumba husika. Hii itasaidia sana kukamilisha ukarabati na maboresho kwa wakati sahihi.

Hivyo utaanza kukusanya marejesho ya mkopo mapema zaidi. Hivi ndizo utaweza kukuza biashara yako ya mikopo kwa haraka zaidi bila kumsababishia changamoto mmiliki wa nyumba.

Hatua 5 Za Kuanza Biashara Ya Mikopo Ya Ukarabati Wa Majengo Ya Kupangisha.

Hatua Ya Kwanza.

Kujifunza kuhusu majengo ya kupangisha.

Jifunze kuhusu nyumba za kupangisha ya kuhamishika, nyumba za kupangisha za matumizi mseto, nyumba za kupangisha za makazi na nyumba za kupangisha za biashara.

Jifunze hasa kuhusu kipato endelevu na kipato chanya kutokana na nyumba za kupangisha. Nyumba nyingi za kupangisha haziingizi kipato chanya.

Unaweza kufahamu kipato chanya kwa kukadiria thamani ya nyumba na kiasi cha kodi ambayo wapangaji hulipia.

Ukiweka shabaha kwenye nyumba ambazo zinaweza kupata wapangaji ndani ya mwezi mmoja tangu kumalizika kwa ukarabati wa nyumba ni vyema sana.

Pia, unatakiwa kuweka shabaha kwenye nyumba ambazo tayari zina wapangaji bora kuliko nyumba ambazo zina wapangaji wasiobora.

Wapangaji bora ni kundi la wapangaji wanaoweza kulipia kodi ya majengo kwa miezi mitatu (3) hata kama chanzo chao kikuu cha kipato kimeathiriwa.

Pia, unatakiwa kujifunza kuhusu majengo ya matumizi maalumu kama vile hoteli, resoti, moteli, gesti housi, vituo vya mazoezi ya viungo vya mwili, na vituo vya shule za chekechea na shule za msingi.

Hatua Ya Pili.

Kuwa na msimamizi wa biashara.

Huyu ni mshauri na mbobezi kwenye uwekezaji wa nyumba za kupangisha. Huyu atakuwa ni mshauri na msimamizi wa hatua zote unazopitia kwenye biashara ya mikopo ya ukarabati na maboresho ya nyumba.

Mimi ni mshauri mbobezi kwenye uwekezaji wa nyumba za kupangisha. Karibu ujiunge na kundi la UWEKEZAJI MAJENGO ili niwe mshauri wako kwenye biashara yako.

Msimamizi mwingine unayemhitaji ni wakili mzoefu. Wakili atahakikisha anapunguza chanagamoto za biashara yako. Wakili atakuwa anahusika na mambo yote yahusuyo mikataba, biashara na sheria za ardhi na nyumba.

Hatua Ya Tatu.

Bobea kwenye halmshauri moja tu.

Unapoanza kuendesha biashara yako, unatakiwa kubobea kwenye halmshauri moja tu. Hii itakusaidia kulifahamu vizuri soko la nyumba za kupangisha.

Pia, kwa kubobea kwenye halmshauri moja utaweza kusoma vizuri biashara, kilimo na uwekezaji kwenye halmashauri husika. Kilimo, biashara na uwekezaji vina matokeo ya moja kwa moja kwenye hali ya masoko ya nyumba za kupangisha.

Hapa utatakiwa kujifunza hali za masoko ya nyumba za kupangisha kwenye halmshauri unayotoa mikopo ya ukarabati wa nyumba.

Pia, utatakiwa kujifunza kuhusu kuhusu tabia na tamaduni za wamiliki wa nyumba za kupangisha kwenye halmashauri husika.

Mambo yote haya nitakuwezesha mimi baada ya kuwa mwanachama wa kundi langu la WhatsApp liitwalo UWEKEZAJI MAJENGO.

Hatua Ya Nne.

Pangilia mtaji fedha wako.

Njia kuu mbili (2) bora sana za kupata mtaji fedha kwa ajili ya biashara ya mikopo ya ukarabati wa majengo ya kupangisha ni kama ifuatavyo;-

✓ Kuweka akiba kutoka kwenye mshahara wako au faida ya biashara yako.

✓ Kuingia ubia na jamaa zako wa karibu.

Njia hizi mbili (2) ndizo ninazokupendekezea ili uweze kuanza biashara yako ya kutoa mikopo ya ukarabati na maboresho ya majengo ya kupangisha.

Tangu siku unaamua kuwa utaanzisha biashara ya mikopo ya majengo ya utakiwa kuendelea kuweka akiba kwenye akaunti maalumu.

Unatakiwa kutumia akaunti za benki ambazo zinaendeshwa kwa kiasi kidogo sana cha gharama za uendeshaji wa akaunti kama vile NMB Chapchap Account.

Akiba ni muhimu sana haijalishi unaingia ubia au unaanza biashara kwa njia zingine za kukusanya mitaji fedha. Ukiwa na akiba ni rahisi sana kuingia ubia wenye tija kwenu wote kuliko uwe na maneno matupu.

Ukitaka ufanikiwe kupitia njia yoyote ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo ni lazima uwe ni mtu wa kujituma kwa kukusanya fedha kupitia njia zote halali unazopata.

Acha kudharau kazi. Miaka mitatu inapita huna hata laki tano (5) benki. Miaka nenda rudi unasingizia huna mtaji wa kutosha. Jitoe fanya kazi halali yoyote ile. Atakayekudharau hawezi kukupa ugali, hata akikupa ugali atakuchoka tu siku moja.

Hatua Ya Tano.

Anzisha biashara ya mikopo kwa kufungua kikundi au kampuni.

Unatakiwa kusajili kikundi endapo una kiasi kidogo cha mtaji fedha. Hivi ndivyo baadhi ya kampuni za kukopesha zilivyoanza biashara zao za mikopo.

Baada ya biashara yako kukua utasaijili kampuni ya mikopo kwa wamiliki wa nyumba za kupangisha. Unatakiwa kuambatana na menta/kocha mbobezi kwenye nyumba za kupangisha, dalali wa nyumba na wakili mzoefu.

Muhimu; lipia leo shilingi elfu arobaini (Tshs.40,000/= tu) ili niwe mshauri wako ndani ya miezi sita kuhusu biashara za kukopesha kwa wamiliki wa nyumba za kupangisha.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

WhatsApp; +255 752 413 711

GOOGLE; UWEKEZAJI MAJENGO BLOG
 
Sijaona changamoto zake

Zipo kama vile mtaji fedha, kufahamu hali ya soko la nyumba za kupangisha n.k.

Haiwezekani makala moja ikawa na kila kitu. Hata kitabu hakiwezi kuwa na kila kitu.

Chanagamoto zipo ila hazijainishwa moja kwa moja.

Nashukuru sana kwa ushirikiano wako kwenye maoni haya.

Karibu sana rafiki yangu.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi wa ardhi na majengo.
 
Wenye nyumba wasumbufu hamtaishia mahakamani kweli

Inafuatana na mfumo wako wa ukusanyaji wa marejesho.

Kila kundi la binadamu kuna wasumbufu. Labda usifanye kabisa biashara.

Usumbufu huo ndio unatengeneza kundi chache la wafanyabishara bora na wenye mafanikio makubwa.

Kwa ujumla utapata changamoto ndogo ukilinganisha na kutoa mikopo ya moja kwa moja kwa wenye nyumba.

Karibu sana rafiki,

Rafiki yako,

Aliko Musa.
 
Asante kwa Malala nzuri.
Utaratibu wa ufunguaji wa kampuni ya ukopeshaji wa mikopo ya ukarabati wa nyumba za kupangisha unatofautianaje na kampuni ya ukopeshaji fedha ?
 
Utaratibu wa ufunguaji wa kampuni ya real estate nao ukoje? kama hutajali tafadhari
 
Wakuu hizi kampuni zinazokopesha mikopo ya ukarabati wa nyumba zinasajiliwa wapi? na zinaoparate vipi?
 
Back
Top Bottom