Hatua gani za kisheria nizifanye ili kuhalalisha cheti hiki

Suns

Member
Joined
Feb 21, 2014
Posts
69
Reaction score
14
Wanasheria naomba msaada wenu vyeti vyangu kuanzia cha kuzaliwa mpaka sekondary nimekuwa nikitumia majina mawili yan jina langu na la ukoo ,lakini cheti chanu cha college kina majina matatu yani na jina la kati ,nifanyeje ili kuhalalisha icho cheti kuwa ni changu?
 
Nenda kwa mwanasheria au mahakamani huko ndo kila kitu mkuu
 
Best wat ni ku-draft afidavit ku-prove kuwa majina ni yako.
 
Nenda mahakamani kale kiapo kwa maelezo zaidi wao watakujuza
 
Mkuu unaweza ongezea nyama kidogo hapa ikiwemo kutoa mwongozo wa namna yakufanya hiyo?
Afidavit ni kiapo, so unaweza kwenda mahakamani au kwa mwanasheria yoyote (mimi niko mbali so usije kwangu [emoji1] kidding!) ataandaa hicho kiapo and ndani atatoa maelezo ya kuwa hayo majina matatu ni yako na ataweka viambatanisho kama cheti cha kuzaliwa au kitu chochote kitakacho tambuliwa kiserikali kama uthibitisho. mwisho utasaini kiapo hicho na mwanasheria pia atasaini. And ili kiweze kutumika basi utapaswa kukisajili ambapo utalipia pesa kidogo kwa "registrar of documents" ili uweze kukitumia sehemu yoyote ambapo cheti hicho kitaleta shida.
 
Nadhani ni kama 20,000 mpaka 30,000 kwa miaka kama miwili iliyopita.
 
Back
Top Bottom