PENDO STEPHANO
New Member
- Jun 26, 2024
- 2
- 21
Shajara ni kitabu maalumu ambacho hutumika kuandika kumbukumbu za matukio ya kila siku. Watu wengi huitambua kama “diary” kwa lugha ya kingereza na kuandika historia kuhusu maisha yao, vitu wanavyopendelea na mawazo kadha wa kadha. Karibu katika makala hii kama mfano wa shajara yangu iliyobeba kurasa za simanzi, furaha, ucheshi na upendo utakaoenda kubadilisha fikra na mitazamo juu ya binti na mwanamke wanaotokea katika mazingira magumu.
Ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto nane. Nilitamani sana nifike mbali kielimu na hata familia pia ilihitaji msomi. Lakini kipato ndicho kilikuwa kikwazo kikubwa kwa wakati huo mimi kuendelea na masomo. Hali hiyo ilipelekea wazazi wangu kutaka kuniozesha mara tu baada ya kumaliza darasa la saba ili wapate pesa na ng'ombe kama sehemu ya kipato cha kuinua uchumi wa familia. Niliamua kutoroka na kukimbilia katika machimbo ya Mererani kwani sikutaka kuolewa katika umri ambao bado nilihitaji kuendelea na masomo.
Nilifanya kazi ya kuwapikia chakula wachimbaji wa madini na baadae kuhamia katika mji wa Dar es salaam kama mtumishi wa kazi za ndani. Nilifanya kazi za ndani sehemu tofauti tofauti huku mshahara wangu mkubwa ukiwa ni Elfu ishirini na tano tu. Lakini nilichokipata niliwatumia nyumbani ili kusaidia kupata chakula na mahitaji mengine.
Ndani ya mafanikio kuna maumivu makali na mazito mno. Kiukweli nilipita katika maumivu, mateso na manyanyaso mazito mengi katika nyumba za watu. Nilipovunja chombo hata kwa bahati mbaya basi hesabu za uhakika ni kwamba sina mshahara wa mwezi mmoja. Nilitukanwa na hata wengine kunitaka kimapenzi lakini nilipambana kuhakikisha ndoto zangu zinatimia.
Miaka inaenda na umri unasogea. Nikabatika kupata mume na mpaka sasa tuna jumla ya watoto sita. Lakini mara zote nilipokuwa nikitafuta kazi, elimu ilikuwa ndio kikwazo kikubwa kwangu kupata fursa. Uthubutu ni nusu ya kutimiza malengo yako. Hivyo niliongea na mume wangu kwamba ni muda muafaka sasa wa mimi kurudi shule na kuendelea nilipoishia. Na kwakuwa alikuwa anajua nia na matamanio yangu kielimu basi akanipa kibali na rasmi nikaanza kusoma elimu ya sekondari huria kwa miaka mitatu.
Nilimkataa rafiki aitwaye aibu na kutokubali uoga na kuona siwezi, nikasimama na kusema ninaweza na kwa hakika nilifanikisha kupata elimu ya sekondari huria kwa muda wa miaka mitatu hadi pale nilipojiunga na chuo kikuu. Wengine walinicheka kuniona natembea na madaftari na umri niliokuwa nao. Wengi walishangazwa na wengine kutaka kujua imekuaje nimeweza kufanya maamuzi magumu ambayo wengi hushindwa kuyafanikisha.
Utu uzima dawa na si kwamba kila dawa ni mitishamba kwa maana itakuwa michungu japo itatibu lakini nashukuru, utu uzima wangu ulikuwa dawa kwa mabinti na vijana kupona ugonjwa wa aibu, kukata tamaa na kujiona hawafai tena katika jamii yetu baada ya masomo yao kukatishwa kwa sababu mbalimbali kama ujauzito, kukosa ada, umri mkubwa na sababu nyingine nyingi. Nia yangu ya kujiendeleza kielimu ikiwa umri wangu ulikuwa mkubwa ilikuwa ni dawa iliyowasaidia wengi kupata ujasiri, uthubutu na uvumilivu katika kufikia malengo yao.
Baada ya kumaliza miaka yangu mitatu ya kusoma elimu ya watu wazima, matokeo yalitoka na ndipo nilipofungua ukurasa mpya wa elimu yangu ya chuo kikuu. Mkaa bure sio sawa na mtembea bure, nawaza je? Ningekaa nyumbani kwa kuhofia watu watanicheka kwa umri wangu kurudi shule, leo nisingekuwa nachukua shahada ya kwanza ya Mawasiliano kwa Umma Chuo Kikuu, kuwajengea nyumba wazazi wangu na kuhakikisha nailinda na kuihudumia familia yangu.
Muungwana ni vitendo na sio maneno, kwahiyo ni muhimu Serikali na jamii kwa ujumla kuamka usingizini na kuhakikisha tunamuinua binti wa kike kwenye upande wa elimu ili kumpata mwanamke na mama bora wa baadae katika kuhakikisha tunatimiza malengo yetu kama Taifa katika nyanja za Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii.
Nitoe rai kwa Serikali kuanzisha shule za elimu huria hususani maeneo ya Vijijini, ambapo kuna wanawake wenzangu na mabinti zetu wa kike wengi wanaotokea katika mazingira magumu na kukatishwa kwa masomo, kupata elimu hii kusudi kujiendeleza katika upande wa elimu. Wapo wengine waliokatisha masomo kwa kupewa ujauzito, wapo wengine waliokosa pesa ya kununua vifaa vyao vya shule kutokana na ugumu wa maisha.
Haitoshi kusema tutakuwa tumemaliza tatizo kama hatutawafadhili masomo mabinti wa kike, wanaotokea katika mazingira magumu ambapo serikali itashirikiana na wadau ama taasisi binafsi kuwatambua wanafunzi hawa na kuwashika mkono kwa kuwasomesha ili kusudi watimize ndoto zao na kutimiza msingi wa kijana kuwa Taifa la kesho.
Kuanzisha matamasha na warsha mbalimbali hususani maeneo ya vijijini, ili kutoa elimu juu ya umuhimu na mchango wa elimu kwa jinsia ya kike, ili kupunguza ndoa za utotoni na Imani potofu kwa mabinti wa kike. Pia kuzuia mfumo wa shule za jinsia moja kwani wanafunzi wa kike wanapaswa kuchanganywa na wanafunzi wa kiume kwani kunaleta ushindani wa kitaaluma na kumuinua mtoto wa kike kuonekana anaweza kama wanafunzi wa jinsia nyingine.
Hali hiyo pia itapunguza na kuondoa mambo machafu yanayofanyika katika shule zenye wanafunzi wa jinsia moja yanayopelekea kuharibu ndoto za mabinti wa kike.
Kuna msemo unasema “Katika mafanikio ya mwanaume, basi kuna mwanamke nyuma”. Na mimi nipende kuongeza sauti yangu juu ya msemo huu kwamba ili tutimize Dira yetu ya Taifa ya Maendeleo 2050, hatupaswi kuwaacha wanawake nyuma kwa kuanza na maeneo ya vijijini ambako athari ni kubwa zaidi.

Upvote
47