Je, ni hatua gani zinapaswa Kuchukuliwa dhido ya ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa inapokataa kutekeleza hukumu ya Mahakama kuu iliyotolewa katika kesi ya ardhi?
Je, ni hatua gani zinapaswa Kuchukuliwa dhido ya ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa inapokataa kutekeleza hukumu ya Mahakama kuu iliyotolewa katika kesi ya ardhi?
Hakuna jibu la moja kwa moja unatakiwa ufanye nini, maana hujasema amri iliyotolewa ipoje.
Lakini kwa ujumla, baada ya hukumu kutolewa na Mahakama, mtekelezaji asipotekeleza kwa hiari kile alichoamriwa, basi mwenye hukumu unatakiwa kukazia hukumu kama kilichoamriwa kinakazika. Utakaza hukumu kulazimisha utekelezaji.
Sasa kuhusu Manispaa, ukazaji hukumu ulikatazwa enzi za JPM, ambapo ili ukaze hukumu ilitakiwa upate cheti kutoka mahakama kuu kikionesha amri iliyopewa serikali na kwamba hawajatekeleza amri hiyo. Ila kwa kifupi ni kuwa kwa sasa ni ngumu kukaza hukumu dhidi ya serikali kwa kesi za humu ndani (local).
Kuna Mkandarasi alifanya kazi na Manispaa na Manispaa ikawa inagoma kumlipa akaends kufungua Kesi dhidi ya Manispaa Akashinda lakini bado Manispaa ikawa haitaki kumlipa Akaenda Kukaza hukumu Mahakama ikaagiza Magari ya Manispaa yakamatwe Na kipigwa Mnada kuona vile Manispas ilimlipa
Kwa hiyo Bado kukazia Hukumu kupo.