Elections 2010 Hatua hii ya NEC ina maana gani?

Elections 2010 Hatua hii ya NEC ina maana gani?

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2008
Posts
1,246
Reaction score
402
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imezibadilisha karatasi za kupigia kura.
Karatasi hizo sasa zitakuwa na nembo ya chama cha siasa cha mgombea.
NEC imeagiza kuwa, mchakato mzima wa uchaguzi ufanyike kwa uwazi.
Katika mabadiliko hayo, kwanza kutakuwa na nafasi ya jina, chama, nembo, picha na baadaye sehemu ya kuweka alama ya vema.

Karatasi za zamani zilikuwa na picha, jina na chini iliwekwa sehemu ya kuweka alama ya vema.
Karatasi hizo bado hazijasambazwa kwenye majimbo ya uchaguzi, zinachapishwa nchini Uingereza.

Source: Habari leo
 
Ina tegemea mwaka huu Nec wanamsimamo gani?.Kama watakuwa wamekubaliana demokrasia kuchukua mkondo wake bila kuchakachua basi hiyo ni habari njema.Pia tukumbuke kuwa boss wa Nec yuko mbioni kustaafu, je yuko tayari kuingia mtaani kama mstaafu kwa kashfa? Nahisi si hivyo yawezekana ameamua kustaafu kwa heshima na kuandika historia chanya, hasa akifikiria yaliyotokea kenya

Angalizo :tusisahau kuwa Samweli DOO wa liberia alimsaliti boss wake, kabila senior alisalitiwa pia, Makame anaweza pia kukataa uchakachuaji na kuacha system ya upigaji kura ikafuata mkondo wake.Mungu awe upande wetu waathirika wa demokrasia
Nikosoe tafadhali!!!!!
 
Hii ina maana nzuri. Mtu akiona kijani anakimbia moja kwa moja kwa Vidole mbili ChademaAAAAAAAAAAA
 
Back
Top Bottom