Hatua kali zichukuliwe kwa watoa Mikopo wa mtandaoni kama SWIFT FUND LOAN

Hatua kali zichukuliwe kwa watoa Mikopo wa mtandaoni kama SWIFT FUND LOAN

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Nimesikitishwa na taarifa niliyopewa na jamaa mmoja aliyekopa kwenye hizi application zinazotoa mikopo kama hawa SWIFT FUND LOAN huenda hawana nidhamu, pia wanao waajiri ni vijana wasiojua namna ya ku handle wateja wao.

Jamaa anasema walimdai kwa matusi siku 2 kabla ya deadline ya kulipa mkopo wake. Kati ya sms nilizo muomba anipe kama ushahidi alizipokea ni hizi hapo nimeambatanisa, nilishangaa kuona kama hawa wamepewa kibali na benki kuu halafu wanafanya kazi wao wanatukana sana wakati mteja wao alikuwa hata hajazidisha siku

Aliendelea kujuza kwamba alizungumza na manager wao anayetumia namba +255699027592 kumripotia kuhusu hilo wala hakuhangaika ku apologize kwa makosa ya watu wake ndio akaona kama wamefanya vizuri.

Namba wanayotumia kuwadai wateja na kuwatukana ni 0699027530 hii namba inayosoma kwa jina la ZANGO TRADING LIMITED kwenye namba nyingine za customer care kuna 0789926646 inayosoma KISASI FINANCE COMPANY.

Baadae alibaini kuna utapeli na wizi mkubwa kwa hawa, serikali na BOT iwachukulie hatua watu kama hawa. Ni hatari sana kwa jamii yetu.
Screenshot_20241106_191058_Chrome.jpg
 
Ninazo zilizo sajiriwa kwa majina yao baada ya kunipigia na kuniambia contact wangu wa karibu kakopa ivyo nimsisitize alipe kabla akija nuka

0674088227
 
SAMAHAN NIKO NJE YA MADA.

Hivi unakopaje elfu 48 Alafu watakiwa kulipa elfu 80 na ulipe ndani ya wiki moja..

Kabla ya kuwaita hao jamaa wanaokopesha hawana Adabu basi tunapasa kuanza na wewe kuwa HUNA ADABU YA AKILI YAKO.

Ukiona unaweza kopa Sehemu yenye unyonyaji kama huo basi ujue nawe Akili zako haziko sawa.
 
Ukikosa pesa hadi vijana wahuni wanajitukania tu...duuh!!!
Msikope hovyohovyo mitandaoni...mtakuja uza utu wenu kwa pesa ndogo...
Shida zipo na zinapiga but tuwe makini pia
 
Hao jamaa waliwahi kunisumbua sana nilikopa elfu 18 nikalipa elfu 33 baada ya wiki tatu. Na wakti huo walikuwa wananipigia simu kila dakika mbili nimalize deni mana wanadai nilipitiliza muda. Unaambiwa kopa elfu 50 ukikopa unatumiwq elfu 35 ndan ya siku 6 ulipe 50.

Kama ukishindwa kila siku inayoongezeka ile deni inajiongeza asilimia kumi. Yani elfu 35 ndani ya wiki tatu usishangae ukakuta ishafika laki na ushee..

Kuna kipindi hapo walifungiwa nashangaa kwa nn wameachiliwa mikundu yao hawa
 
Back
Top Bottom