Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,772
- 22,598
Kutokana na hali ngumu ya kiuchumi na ukosefu wa ajira, kujiajiri imekuwa njia bora ya kujipatia kipato. Watu wengi wanasukumwa kuingia kwenye biashara au ujasiriamali kutokana na kukosa ajira au kipato cha ajira kuwa kidogo ukilinganisha na gharama za maisha. Ili kuweza kufanikiwa kwenye biashara unahitaji kuwa na wazo zuri la biashara. Je unajua jinsi ya kupata wazo hilo zuri la biashara?
Watu wengi wamekuwa wakiomba ushauri ni wazo gani zuri la biashara ambalo linaweza kuwapatia faida na mafanikio. Ukweli ni kwamba wazo ambalo ni bora kwa mtu fulani linaweza lisiwe bora kwako.
Moja ya sababu zinazofanya biashara nyingi kufa au kutokuendelea ni kuiga, yaani mtu akianza biashara leo baada ya muda unakuta watu wengine wameiga biashara ile ile, wanaifanya eneo lile lile na kwa mbinu zile zile. Hii ni njia rahisi sana ya kushindwa kwenye biashara. Leo tutajadili njia tano unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara ambayo itakupatia mafanikio makubwa. Kwa kutumia njia hizi utatengeneza wazo lako mwenyewe na utaweza kulifanyia kazi vizuri sana.
Zifuatazo ni njia tano unazoweza kupitia katika kutengeneza wazo zuri la biashara:
1. Unapenda vitu gani?
Kila mmoja wetu kuna vitu ambavyo anavipenda sana. Vitu hivi vinaweza kuwa ni vipaji vyako au ni vitu ambavyo umetokea kuvutiwa navyo na hivyo kupenda kuvifuatilia. Inawezekana unapenda mitindo, unapenda kutumia intaneti, unapenda kujifunza zaidi, unapenda watoto, unapenda magari au unapenda michezo fulani. Orodhesha vitu vyote ambavyo unapenda kuvifanya na unapenda kuvifuatilia. Hakikisha vitu unavyoorodhesha unavipenda kweli na upo tayari kuvifanya hata kama hulipwi fedha.
2. Una ujuzi au uzoefu gani?
Katika maisha yako kuna ujuzi au uzoefu ambao umeupata. Yawezekana umesomea fani fulani au umewahi kufanya kazi ambayo ilikupatia ujuzi fulani. Orodhesha ujuzi wote ambao umeupata kutoka kwenye elimu na hata kujisomea au kufuatailia watu waliofanikiwa. Pia orodhesha uzoefu wowote ambao umewahi kuupata kwa kazi ambazo umewahi kufanya, iwe ni ajira kujiajiri au hata kujitolea.
habari zaidi, soma=>http://www.fikrapevu.com/hatua-tano-muhimu-za-kutengeneza-wazo-bora-la-biashara/