SoC03 Hatua tatu

SoC03 Hatua tatu

Stories of Change - 2023 Competition

mackj

Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
84
Reaction score
98
Ni matumaini yangu uheri mzima wa afya msomaji na mfuatiliaji wa jukwaa hili la "stories of change" Naam katika ustawi wa taifa lolote lile ni lazima afya za watu wake ziwe bora, ikiwa afya zao zinakuwa duni basi upatikanaji wa maendeleo katika taifa hilo ni ndoto.

Kwa msingi huo ndio maana serikali mnamo mwaka 2003 ilitunga sera ya taifa ya afya, pamoja na mambo mengine sera hii ilitaja makundi yanayo stahili kupata matibabu bure bila malipo kuwa ni pamoja mama wajawazito, watoto walio na umri chini ya miaka mitano, pamoja na wazee. Lakini dhana ya uwajibikaji katika kutekeleezeka kwa sera hii kwa vitendo imekuwa ni kilio kikubwa kwa makundi lengwa. Ikumbukwe kuwa miongoni mwa makundi haya wazee ndio kundi pekee lenye umoja wao au chama kiitwacho (SAWATA) saidia wazee Tanzania.

Kila october mosi ni siku ya wazee duniani ambapo wazee hutumia siku hiyo kuanika madhila wanayokutana nayo pindi waendapo katika hospitali na vituo vya afya vya uma kupata matibabu ikiwa ni pamoja na kuiomba serikali kuitungia sera hii sheria ili waweze kuwabana watoa huduma pale wanaposhimdwa kutimiza wajibu wao wa kuwapatia huduma wazee kwa mujibu wa sera lakini uwajibikaji wa serikali katika uutekelezwaji wa ombi hili ambalo ni haki ya msingi na ya kisheria imekuwa ni butu miaka 20 sasa tangu kuanzishwa kwa sera yenyewe, kitu ambacho ni jambo la kuhuzunisha nimeipa makala hii kichwa cha habari kiitwacho "HATUA TATU" kwakuwa Mungu katika uumbaji wake dhidi ya mwanadamu hutupitisha katika hatua tatu muhimu ambazo ni ujauzito, utoto, kisha utu uzima au uzee.

Hatua hizi kimuundo hubainisha makundi haya matatu amabayo ndiyo wahanga katika kukumbwa na maradhi mara kwa mara kulingana na hali halisi ilivyo lakini serikali kupitia wizara ya afya imeshindwa kuwajibika katika kutoa matibabu bure katika makundi haya.

Awali serikali iliweka itaratibu wa vitambulisho vya wazee vilivyokuwa vikitolewa na halmashauri za miji, manispaa pamoja na majiji hapa nchini ili watoa huduma waweze kuwatambua wazee lakini utaratibu huo ulishindwa kufanya kazi kutokana kutokuwepo eneo maalum la wazee kupata huduma km kundi lenye uhitaji kisera, isipokuwa waliunganishwa katika madirisha ya bima ambapo watoa huduma walikuwa wanawabagua wazee kwakuwa hawakuwa na kadi za bima.

Katika hospitali ya mkoa wa mara hivi karibuni nilipokuwa katika utafiti wa makala haya nilipata wasaa wa kuzungumza na mzee kassim juma, mwenye umri wa miaka 71 mkazi wa kigera manspaa ya musoma alisema kuwa wanakalishwa kwenye mabenchi kwa kuambiwa kuwa wangoje kwanza wenye bima wamalizike ndio watasikilizwa "Mimi nina fomu ya msamaha ndio inanipa sababu ya kuwa hapa lakini nesi anasema hiyo siyo kadi ya bima nisubiri kwanza kila unapoinuka wa bima anaingia ninakaa nimechoka naenda nyumbani ninakaa mbali na miguu ni mibovu siwezi kutembea vizuri" alisema mzee kasim juma.

Ilinibidi niende chumba namba 2 ambapo niliambiwa ndipo kuna mtoa huduma wa fomu hizo za wazee amabazo ni utaratibu mpya unaotumika ili kumpa mzee ahueni ya kusikilizwa na watoa huduma hapa nilikutana na bwana maulid Hussein ambaye ni afisa kutoka ofisi ya maendeleo ya jamii manispaa alisema wao wanatimiza wajibu wao wa kutoa fomu za msamaha na kumuelekeza mzee kwenye dirisha la wagonjwa wa nje wenye bima "sisi wajibu wetu ndio huo lakini sasa pale napo kwa mfumo wa sasa kila data inaingia kwenye systeam kwahiyo hata manesi wanaogopa kwakweli sema mfumo wa matibabu kwa haya makundi yaliyotajwa kisera especially wazee umekaa kisiasa maana hauna maelekezo ya kutosha kwakweli inauma sana ila hatuna jinsi" Alisema Maulid Hussein.

Hivyo ndivyo hali ilivyo katika sektaa ya afya lakini mwarobaini wa hoja hii umekosekana kweli tangu mwaka 2003? Au kuna utashi wa kisiasa? Kama asemavyo maulid? Na kama upo mnufaika ni nani ama kwa hakika ikiwa sera hii itatungiwa sheria kama wanavyoomba wazee kila mara katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani, watoa huduma ambao wanaonekana kutoa huduma kwa wazee kwa huruma na siyo kwa kuzingatia miongozo basi sheria ingechukua mkondo wake.

Kisanga hiki kinanikumbusha kisa cha kuku na yai nani alianza? Ambapo najiuliza je nini huanza kutungwa kati ya sera na sheria? Na je ni kwanini sheria ya sera hii imeshindikana kutungwa hadi leo? Lakini ikumbukwe kwamba hakuna atakayeweza kuukwepa uzee labda ufariki dunia, na ikiwa tanzania ni nchi inayoongozwa na Rais mwanamke ambaye ni mama anaejua uchungu wa kuzaa na pia ni mama anaeelekea katika uzee anajua madhila yatokanayo na umri mkubwa ikiwa ni pamoja kuishiwa nguvu za kufanya kazi ili kujikimu basi bila shaka kupitia safu hii jambo hili litapatiwa ufumbuzi ili kunusuru jamii hii muhimu amabayo ni azina ya taifa na uwajibikaji ukiwepo katika hili, taifa litapona kuepuka laana za wazee ambao kwa sasa wanaona kama hawana haki katika nchi yao.

Mpaka kufikia hapo makala hii inakuwa haina la ziada nilikuwa nikiangazia sekata ya afya juu ya dhana ya uwajibikaji wa serikali katika kutekeleza matakwa ya kisheria ya kutungiwa sheria sera ya afya ya taifa ya mwaka 2003 kitu amabacho kimekuwa kilio cha muda mrefu cha wazee mimi ni makj.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom