Hatua ya China kuondoa ushuru yaonyesha wajibu wa kama nchi kubwa ya “Dunia ya Tatu”

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111410195014.jpg

Kuanzia Desemba, China itafutilia mbali ushuru kwa bidhaa za nchi zilizo nyuma zaidi kimaendeleo duniani, zikiwemo Tanzania na nchi nyingine 32 za Afrika. Wakati dunia inakabiliwa na ongezeko la vitendo vya kujilinda kibiashara, hatua hii hakika itapunguza gharama za nchi hizi husika katika kuuza bidhaa zao nchini China, ikionyesha wajibu wa China kama nchi kubwa ya "Dunia ya Tatu" na kundi kubwa la kiuchumi duniani.

Katika biashara ya kimataifa, ushuru ni jambo muhimu, kwani huathiri moja kwa moja gharama za bidhaa na ushindani sokoni. Kwa nchi nyingi za Afrika, kutokana na maendeleo duni ya viwanda, bidhaa zinazouzwa nje zaidi ni zile za ngazi ya msingi kama mazao ya kilimo, matunda, na bidhaa za baharini. Hali hii hufanya ushuru kuwa mzigo mkubwa kwao katika kuuza bidhaa nje.

Kwa hivyo, hatua hii ya China itachochea moja kwa moja ukuaji wa mauzo ya nje ya nchi hizi kuja China, kukuza maendeleo ya viwanda vyao, na kusaidia kupunguza pengo la biashara kati ya China na Afrika.

Hali halisi ni kuwa, utekelezaji wa hatua hii ya kufikia kuondoa ushuru haukutimizwa ndani ya siku moja, bali ni juhudi za miongo kadhaa za China na Afrika kupitia mazungumzo na ushirikiano wakati uhusiano wao unaimarika. Kuanzia mwaka 2005, China ilipoanza kutoa ushuru sifuri kwa bidhaa 190 kutoka nchi 25 zilizo nyuma kimaendeleo barani Afrika, hadi mwaka 2012 ilipotangaza kutoa ushuru sifuri kwa asilimia 97 ya bidhaa kutoka nchi zilizo nyuma kimaendeleo za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China, na mwaka 2021 ilipotangaza mpango wa kuagiza bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 300 kutoka Afrika ndani ya miaka mitatu, na hadi mwaka 2024, China inakuwa nchi ya kwanza inayoendelea kufuta ushuru wa bidhaa kutoka nchi zilizo nyuma kimaendeleo duniani.

Hatua hizi zimethibitisha kuwa China inatimiza ahadi zake za kupanua soko kwa nchi za Afrika, na jambo hili limepokelewa kwa mikono miwili na nchi husika.

Kinachostahiki kutajwa ni kuwa hatua hii ya ushuru sifuri sio tu kwamba inanufaisha China na Afrika, bali pia itakuwa na athari chanya kwa muundo wa maendeleo ya dunia. Kwanza, hatua hii itaimarisha zaidi ushirikiano kati ya China na Afrika, na kutoa mwongozo na mfano kwa nchi nyingine za "Dunia ya Tatu" kujishughulisha katika kujenga usasa.

Kwa sasa, malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa yanakabiliwa na changamoto kubwa, si kwa sababu nchi nyingi zimeingia katika usasa, bali kwa sababu ni nchi chache sana zinazofikia usasa. Wakati China na Afrika zinajumuisha theluthi moja ya idadi ya watu wote duniani, zikifanikiwa kufikia usasa kwa pamoja, hakika zitahamasisha nchi nyingine za Dunia ya Kusini kufuata njia ya usasa, na kuchangia ukuaji endelevu wa dunia nzima. La sivyo, maendeleo ya dunia yaliyo na uwiano na uthabiti yatabaki katika hali ya sintofahamu.

Wakati huo huo, hatua hii itasaidia kulinda uwazi na ushirikiano katika mazingira ya kimataifa badala ya kujilinda kibiashara. Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya nchi za magharibi, zinavuruga biashara ya kimataifa kwa sababu ya maslahi yao binafsi, mara nyingi kupitia kuongeza ushuru ili kujiandalia faida za mazungumzo. Mfano maarufu zaidi ni serikali iliyopita ya Marekani iliyokuwa chini ya rais wa zamani Donald Trump, ambaye sasa ni rais mteule anayekaribia kuanza muhula wake wa pili. Wakati wa kampeni yake safari hii, Trump alisema kuwa "neno zuri zaidi katika kamusi yake ni ushuru." Kwa kuzingatia hili, kuna uwezekano mkubwa kwamba atarejea sera ya "Marekani Kwanza" na pengine ataongeza vizuizi vya biashara kwa nchi nyingine hasa za Kusini, ikiwa ni pamoja na kutathmini upya Mkataba wa Ukuaji na Fursa za Afrika (AGOA), ambao umetoa fursa kwa nchi nyingi za Afrika kuuza bidhaa zao bila ushuru nchini Marekani.

Kwa hivyo, hatua ya China kufungua soko lake kwa hiari kwa nchi zilizo nyuma kimaendeleo itapunguza hofu ya nchi za Dunia ya Kusini kuhusu umwamba wa kimataifa, na kuchangia nguvu ya China katika kuimarisha uhuru na uthabiti wa biashara ya kimataifa.
 
Wac
View attachment 3162998

Kwa hivyo, hatua ya China kufungua soko lake kwa hiari kwa nchi zilizo nyuma kimaendeleo itapunguza hofu ya nchi za Dunia ya Kusini kuhusu umwamba wa kimataifa, na kuchangia nguvu ya China katika kuimarisha uhuru na uthabiti wa biashara ya kimataifa
Nchi ya China wana VISION ya mbali kabisa kwa ajili ya kuendelea kuwa Economically Giant katika dunia ya leo.
 
Back
Top Bottom