Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Juzi kuna mteja alituita kuwa gari yake aliipaki na kuingia kwenye supermarket kupata mahitaji yake. Ila baada ya kurudi kwenye gari haikuwaka kabisa, ingawa taa zilikuwa zinawaka, radio inafanya kazi wiper zinafanya kazi ila stator motor ilikuwa haigoti kabisa.
Tukatuma fundi wetu kwenda kuangalia na kweli naye akasema diagnostics inahitajiwa ambayo asingeweza kuifanya pale kwenye parking lot, hivyo tukapeleka tow truck (breakdown kinyumbani) yetu kulivuta gari lile. Huwa tunachaji dola 100 kwa towing services. Baada ya kuvuta gari lile na kulifikisha kwenye karakana yetu, likafanya kazi kama kawaida bila matengezeo yoyote!
Tukagundua kuwa inawezekana ile switch ya parking ilikuwa haikushika sawasawa kwa vile magari yaenye automatic transmission huwa hayastart iwapo transmission haiko kwenye P au N. Ili gari lile liwekwe sawa kabla ya kubebwa na tow truck, ilibidi liwekwe kwenye neutral halafu lisukumwe hadi kwenye jaw za tow truck, na process hiyo ndiyo iliyotatua tatizo lote.
Ushauri wangu sasa: Ukipata kadhia ya namna hiyo na gari yako, jaribu kuhamishahamisha stick ya auto-transmission kati ya P-R-N-R-P kabla ya kujaribu kustart tena. Inaweza kukusaidia sana kuondoa kero na vile vile kukupunguzia gharama za kutafuta mafundi.
Kich: Certified ASE Consultant