Hatua za dharura za kuchukua kupambana na janga la ajira nchini

Hatua za dharura za kuchukua kupambana na janga la ajira nchini

Knuckletouchez

New Member
Joined
May 7, 2021
Posts
3
Reaction score
6
Pamoja na kwamba Mimi ni mshabiki wa Magu, lakini hilo haliniondolei kuona madhaifu yake.

Jamaa aliacha kuajiri wahitimu ambao serikali zilizopita ziliwaandaa, na kuwapa kipaumbele katika kupata mikopo ya elimu ya juu ili kuweza kukidhi mahitaji ya waalimu na watumishi wa afya

Lakini miaka mitano ya jpm wahitimu waliachwa mtaani na wameendelea kumiminika mtaani huku ajira zikitolewa kwa matone,

Hili janga linahitaji immediate solution na linahitaji hali ya dharura kuchukuliwa kukabiliana nalo,

1: Serikali ibadili vipaumbele vyake kwa aina ya wahitimu wanaohitajika, serikali itoe kipaumbele kwa wahitimu wa kupata elimu ili wajiajiri, mfano kozi za kilimo, biashara, uchumi, teknolojia na mengineyo ambayo mwanafunzi anaposoma anajua kichwani kwake ya kwamba maarifa atakayopata ndo atakayoenda kutumia kujipatia kipato, tofauti na sahivi ambapo mwanafunzi yupo.tyari kuibia na kukariri majibu ili afaulu mtihani amalize chuo na kuajiriwa.

2: Serikali itenge bajet maalum kwa ajili ya kuwaajiri wale wahitimu ambao wakati wanasoma kozi zao zilipewa kipaumbele kwenye mikopo na of a mbalimbali kwani wahitimu wamezalishwa wengi sana kwa sababu ya Sera ya serikali ya kupewa kipaumbele, ikiwa na tafsiri ya kwamba wataajiriwa,

3: Serikali iamue kupunguza mikopo kwenye kozi hizo za elimu na afya ili kupunguza idadi ya wanaotaka kusoma.

4: Serikali iwe inatoa muongozo wake wa miaka mitano wa Sera zake. Mfano, serikali iseme tunahitaji waalimu na wauguzi kiasi flani, na hapo ndipo vyuo vikuu vinapewa nafasi ya kudahili kulingana na nafasi.

NB: Hili tatizo JPM angekuwepo na angetaka kulimaliza, uwezo huo alikuwa nao, sema hakuamuaga na yeye alikuwa na kipaumbele vyake.
 
Mungu alisikia kilio na dua za wengi. Yule hakuwa mtu ila zimwi hatari. Kama Gagula wa kwenye kitabu cha Mashimo ya Mfalme Suleiman

1621972134073.png
 
Hiyo reply hapo [emoji115]ni yakijinga kuwahi tokea apa jukwani
 
Mnapaswa kujua mambo yafuatayo:

1. Serikali ina ajiri kulingana na uhitaji.

2. Population inaongezeka so as the graduates. So kusema JK aliweza kuajiri wahitimu wote while JPM ni sawa na sisi kulalamika kua kuajiriwa enzi za JK angalau uwe na degree while wazee wetu walipata vyeo vya ubos wa certificate zao za form 4 or 6 or diploma enzi hizo, mzee wangu kamaliza DIT karandinga la Jeshi linamsubiri akaanze kazi kitu ambacho huwezi kukiona Leo.

3. Tax base ya walipa kodi haikui kulingana na mahitaji, unless tukubaliane serikali iajiri tu iachane na miradi ya kimaendeleo.

4. Serikali itoe elimu kua serikali sio muajiri mkuu bali facilitator, kuna mentality za kishamba kua uki graduate lazima uajiriwe na zaidi uajiriwe serikalini.
 
Serikali wangetoa Mikopa kwenye vyuo vya Ufundi VETA. Wanafunzi wengi wanapenda Mkopo watakwenda huko wakimaliza wanajiajiri wenyewe.
 
Vipaumbele vya
1. Kununua ndege
2. Kuamishia mbuga charo
3. Kujenga balabala uku wapitaji choka mbaya
4. Kufanya ddm itawale daima ( kununua wapinzani)
5. Kufany watu waishi kama wendawazimu

N.k

Bora kaenda zake, inahuzunisha lkn muda mwingine ni furaha iliyoje
 
Back
Top Bottom