Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,915
- 3,422
Habari njema Matajiri Wawekezaji,
Karibuni kwenye mfululizo wa masomo yetu ya programu ya NGUVU YA BUKU, ambapo tunajifunza na kufanya uwekezaji kwa hatua ndogo ndogo na kujenga utajiri kwa uhakika.
Kauli mbiu yetu kwenye NGUVU YA BUKU, ambayo pia ndiyo imani yetu ni KILA MTU ANAWEZA KUWA TAJIRI. Hilo tuna uhakika nalo kwa sababu kwa fedha ndogo ndogo ambazo kila mtu anazipata, tukiziwekeza kwa muda mrefu kwa msimamo bila kuacha, tunaweza kujenga utajiri mkubwa.
Mfumo wetu wa elimu umetukaririsha mambo mengi sana, mengi ambayo hatuna matumizi nayo ya moja kwa moja. Lakini kitu muhimu kama fedha, hakijapewa uzito kwenye elimu rasmi tuliyopata.
Na kwa bahati mbaya, hata kwenye familia na jamii, bado pia hatupati elimu sahihi kuhusu fedha, kwa sababu waliopo nao hawajui kwa usahihi. Hilo limepelekea wengi wetu kuyaendesha maisha yetu bila ya uelewa sahihi wa mambo ya kifedha.
Moja ya eneo ambalo watu hawana uelewa nalo wa kutosha ni uwekezaji. Hata watu ambao wamefika elimu ya juu, wakapata kazi na kulipwa vizuri, bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu uwekezaji. Matokeo yake ni wengi kushindwa kunufaika na fursa nzuri za uwekezaji zinazotuzunguka.
Wengi wanakuja kujua kuhusu uwekezaji umri ukiwa umeshaenda sana na wamekaa kwenye kazi na/au biashara kwa muda mrefu lakini hawakuwa wanawekeza kile wanachopata.
Wengi wanapojua kuhusu uwekezaji ndiyo wanaona kwamba walichelewa sana kujua kuhusu uwekezaji. Wengi hueleza jinsi ambavyo kama wangejua kuhusu uwekezaji mapema basi wangekuwa wamefika mbali sana.
Cha kushangaza sasa, hata baada ya kujua kuhusu uwekezaji, bado wengi hawawekezi kwa uhakika. Watapata moto mwanzoni wa kuonyesha kwamba watawekeza, lakini hawatadumu kwa muda mrefu. Wanaishia kurudi kwenye mazoea yao na kuzidi kushindwa kunufaika.
Ili kuondokana na hali hii ya watu kuona wamechelewa lakini bado hawachukui hatua sahihi, hatua zifuatazo zinapaswa kuchukuliwa.
Moja; Ndiyo Wakati Sahihi Kwako Kujua.
Rafiki, huwa kuna kauli ya wachina inayosema; ‘Mwanafunzi akiwa tayari, mwalimu huonekana.’ Hiyo ina maana kwamba walimu wapo wakati wote, ila kama mwanafunzi hayupo tayari, hawawezi kuonekana. Hukujua kuhusu uwekezaji mapema siyo kwa sababu maarifa hayakuwepo, bali hukuwa tayari. Maarifa yalikuwepo, ungekuwa unayataka ungeyapata.
Hivyo usijione umechelewa, badala yake ona ni wakati sahihi kwako kujua.
Mbili; Umeshajua, Fanya.
Kuna kauli nyingine nzuri ambayo inasema; ‘Wakati sahihi wa kupanda mti ulikuwa miaka 20 iliyopita, wakati mwingine sahihi ni sasa.’ Ukishajua kitu ambacho unaona ulipaswa kukijua mapema, onyesha hilo kwa vitendo kupitia kufanya. Kama kweli unaona ulichelewa, hupaswi kuendelea kujichelewesha, badala yake chukua hatua mara moja.
Fanya kile ambacho unaona ulipaswa kuwa umeanza kukifanya mapema, usijicheleweshe tena.
Tatu; Tumia Uzoefu Wako Kutokurudia Makosa.
Kwa kuwa tumeanza na kauli, basi tutaendelea nazo, kuna hii inasema; ‘Nyani mzee, amekwepa mishale mingi.’ Pamoja na kuchelewa kwako kuanza uwekezaji, kuna uzoefu mwingi ambao umeshajikusanyia kwenye maisha, ambao ukiutumia kwenye uwekezaji utakusaidia. Kadiri unavyokuwa umeishi na kufanya kazi na biashara kwa muda mrefu, ndivyo unavyokua umejifunza mengi kuhusu watu, uchumi na mengine. Yote hayo uliyojifunza ni muhimu sana kwenye kufanikiwa kwenye uwekezaji. Umeshapata hasara nyingi, kudanganya, kulaghaiwa na kufanya maamuzi yaliyokugharimu, usiyarudie tena kwenye mapya unayofanya.
Japo unaweza kuona umechelewa, kuna mambo utaepuka kuyafanya kwa sababu ya uzoefu wako, ambayo wasio na uzoefu watayafanya na kupoteza. Hivyo tumia uzoefu wako kuepuka makosa yanayoweza kukupoteza.
SOMA; Mfuko Wa Uwekezaji Wa Pamoja Wa Umoja Wa UTT AMIS.
Nne; Usitumie Njia Za Mkato.
Ipo kauli inayosema; ‘Ukiwa umechelewa, usijaribu kupitia njia ya mkato, kwani utachelewa zaidi.’ Wengi kwa kuona wamechelewa, hujaribu kutafuta njia za mkato, zenye matokeo makubwa na ya haraka kama njia ya kuokoa muda walipoteza. Lakini matokeo yake huwa ni kilio, kwani huishia kupoteza sana. Kwa tamaa ya matokeo makubwa na ya haraka, wanaishia kutapeliwa na kupoteza zaidi.
Hata kama unaona umechelewa kiasi gani, wewe fuata njia sahihi, usijaribu kabisa njia za mkato. Waache wasio na uzoefu wahangaike na hayo na walipe gharama za kukosa uzoefu. Wewe unajua zaidi, fanya kilicho sahihi.
Tano; Kimbia Mbio Zako Mwenyewe.
Tutamalizia na kauli hii inayosema; ‘Mtu sahihi wa wewe kushindana naye ni wewe mwenyewe.’ Watu wengi wamejikwamisha kufanya makubwa kwa sababu ya kujilinganisha na kushindana na wengine. Wanafanya kile ambacho wengine wanafanya, bila kujua kwamba kila mtu ana malengo na mipango yake, ambayo haifanani na ya wengine.
Katika kipindi ambacho umejua kuhusu uwekezaji, kokotoa hesabu zako kwa usahihi ni kiasi gani cha kuwekeza na kwa wakati gani ili ufikie lengo la uhuru wa kifedha. Ukishapata jibu, lifanyie kazi hilo na acha kuhangaika na yale wanayofanya wengine.
Rafiki, japokuwa mtu unaweza kujiona umechelewa kujua na kuanza uwekezaji, wakati unaokuwa umejua ndiyo wakati sahihi kwako. Wajibu wako ni kuchukua hatua, ukitumia kila rasilimali unayokuwa nayo kuhakikisha unanufaika kupitia uwekezaji.
SIKILIZA SOMO HILI KWENYE ONGEA NA KOCHA.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA tumekuwa na mjadala mzuri wa somo hili ambapo washiriki wamekuwa na maswali na michango mbalimbali. Karibu usikilize hapo chini ili ujifunze na kuchukua hatua sahihi.
View: https://youtu.be/fTu0KjjuZDI
MJADALA WA SOMO.
Karibu kwenye mjadala wa somo hili, shiriki kwa kutuma majibu ya maswali haya;
1. Kwa kipindi ambacho umeanza kufanya uwekezaji, je unajiona umewahi au umechelewa? Kwa nini?
2. Nini kilichokuchelewesha kuanza uwekezaji pale tu ulipoanza kuingiza kipato?
3. Ni uzoefu gani wa nje ya uwekezaji ambao umekuwa unautumia ili kuhakikisha unawekeza kwa manufaa?
4. Kwenye uwekezaji, ni mbio zipi ulizochagua kukimbia mwenyewe na kutokusumbuka na mambo ya wengine?
5. Karibu kwa maswali, maoni, mapendekezo na shuhuda kuhusu somo hili na programu nzima ya NGUVU YA BUKU na UHURU WA KIFEDHA.
Tuma majibu ya maswali hayo kama uthibitisho wa kusoma, kuelewa na kutekeleza somo hili la uwekezaji.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com
www.amkamtanzania.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.