Hatua za kufuata ili kufungua ama kumiliki butcher ya nyama

Dolla_Mbili

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
1,207
Reaction score
2,981
Habari wakuu,

Bila kuwapotezea muda kwa maneno mengi, ngoja niende moja kwa moja kwenye mada tajwa.

Naomba kupata ufafanuzi kwa anayejua namna ama hatua mpaka kupata kibali cha kufungua butcher ya vitoweo kama nyama na samaki, aidha kwa utaratibu wa vibali ama na mlolongo mzima kwa ujumla.
 
Inategemea na mtaji wako. Na unataka kuanza kwa ukubwa gani?
 
Kawaida tu, ila swala kubwa ninalotaka kujua ni vibali....
  • Sajili kampuni
  • Nenda TRA wakupe TIN upate na Tax clearance
  • Nenda Halmashauri kwaajili ya leseni, au ingia tausi.tamisemi.go.tz
  • Mtafute Afisa Afya apitie bucha lako,na akupe fomu za kupima Afya (Medical Examination forms for Food Handlers) kwaajili ya wahudumu wakapime.
  • Hakikisha una bucha zuri lenye marumaru, feni, Jokofu na msumeno wa umeme ( siyo gogo)
  • Uza Nyama yenye mhuri wa Daktari wa mifugo.

Anza kazi
 
M3 ila mi nakushauri fungua bucha la samaki sato na sangara na tafuta location nzuri utakuja nishukuru ,jitofautishe na wengine mabucha ya nyama yapo MENGI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…