JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
- Nunua chanjo, kama inahitaji ubaridi hakikisha umefungiwa kwenye kifungashio Chenye barafu.
- Safisha vyombo vya maji vya kuweka chanjo yako na ikifaa viache vikauke. Kwa maji ya bomba, kisima na mvua inashauriwa yachemshwe na uyaache yapoe kabisa ndipo utachanganya na chanjo.
- Iwapo utatumia vidonge vya kutibu maji MFN Cevamune, Chlorex Blue, Vacc-Sure n.k. Utatakiwa kuloweka kidonge kwenye maji yasiyo na chanjo na changanya vizuri Kwa kifaa cha plastic. Acha maji hayo yakae kwa dakika 15-30 kisha changanya na chanjo yako. Kama utatumia maziwa ‘Skimmed Milk’ weka tone 2 kwa lita moja ya maji changanya vema na uache kwa dakika 30.