HATUA ZA MKATABA!

SHIPPPA

Member
Joined
Apr 7, 2016
Posts
14
Reaction score
3
Nina nyumba imechakaa ipo katika eneo zuri la biashara binafsi sijawa na uwezo wa kuirekebisha kwa sasa, kaja mtu anataka kuirekebishe kisha afanye biashara. Tayari kashaingalia na anasema gharama zinazoitajika ni milioni 3. Makubaliano na kufanya biashara mpaka pesa yake irudi kisha ndio aanze kulipa kodi! msaada unahitajika taratibu za mkataba na mambo ya kisheria.
 
Mkataba ni makubaliano ya wahusika (parties) katika mkataba huo. Mkataba unaweza ukawa wa maandishi au wa maneno (oral contract).

Sheria inahitaji pande mbili zinazoingia au kusaini huo mkataba muwe mmefanya mambo yafuatayo;
i. Ridhaa iwepo (free consent)

ii. malipo (consideration)

iii. Makubaliano ya kitu kilicho halali legal (object) n.k

Bila ya kufanya yaliyotajwa hapo juu utakuwa ni batili mkuu.

Baada ya mkataba kusainiwa lazima utawafunga na ikitokea mmoja wenu kauvunja au mkataba lazima utamfidia mwenzako kwa kuvunja huo mkataba.

Pia mkataba wenu lazima ueleze wajibu na majukumu (duties and responsibilities) ya wahusika katika mkataba huo.

Masharti na vigezo (terms and conditions) lazima vizingatiwe/ yazingatiwe na kuheshimiwa na wahusika wa upande zote mbili.

ZINGATIA
Ukiona unadhulumiwa haki yako mahakama zipo kwa ajili ya kutafsiri ya sheria, kulinda majukumu ya wahusika katika Mkataba na kuamua na kutenda haki.

Nipo tayari kusahihishwa nilipokosea.
 
Joshydama upo sahihi kabisa lakini kwa scenario ya huyu ndugu, Kuna technicalities za vipengele vitakavyozungumzia makato ya gharama zitakazotumika kufanya ukarabati.

Kwanza kwa asili ya makubaliano Kama haya, ningependa kukushauri kuwa Ni vyema mngekubaliana Na mpangaji wako kuwa akukate asilimia kadhaa katika kodi mpaka hiyo m3 itakapoisha, Mfano Kama kodi Ni 500000, basi awe anakulipa angalau 200000 kila mwezi.

Lakini pia, embu angalia huo ukarabati Ni kwa manufaa ya nani, Na siku yeye akihama je, unaweza nufaika Na huo ukarabati?, Na hata kwa kipindi hiki cha mkataba wewe mwenye nyumba unanufaika vipi Na huo ukarabati?, hii itasaidia kukufanya uwe Na maamuzi sahihi maana wengine hutumia ujanja huo Ili kulipa gharama kidogo.

Kingine, angalia kodi ya mwezi, itaweza kulipa gharama za pesa iliyotumika kufanya ukarabati kwa miezi mingapi?, Mfano gharama za ukarabati Ni M3, alafu kodi Ni laki 1, Ina maana hapo utaanza kupokea kodi baada ya miaka miwili Na miezi sita, ambayo Ni muda mrefu Sana kitu ambacho mpangaji anaweza kuwa amemaliza mkataba wake Na usiambulie chochote.

Lakini cha zaidi kwenye mkataba wenu kuwepo Na kipengele cha kumbana mpangaji kuwa Na upangaji wa muda mrefu, angalau kuanzia miaka miwili.

Haya niliyoyasema nimekisia kulingana na maelezo yako kuwa finyu, lakini naamini yanaweza kukupa mwanga.

Note: Mkataba Ni jambo la kisheria,Na Ni jambo la kitaaluma, Ni vizuri ukamlipa wakili angalau hata Kati ya 30000-50000 Ili mkataba wako uwe salama kwa pande zote mbili, maana atakupa na ushauri zaidi.

Tafuta wakili aliye jirani yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…