SoC01 Hatua zaidi zichukuliwe ili walemavu wapate elimu bora

Stories of Change - 2021 Competition

Uchumi wa Mifugo

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2021
Posts
345
Reaction score
580
Elimu ni moja ya haki za msingi kwa kila mtoto wa Kitanzania bila kujali mtoto huyo ni mlemavu au la.Pamoja na sera na mikakati ya kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi na wale wa kidato cha kwanza hadi cha nne lakini elimu inayotolewa kwa watoto walemavu hasa wale wa kuona,akili na kusikia bado hauridhishi.

Tofauti na walemavu wengine kama wale wa viungo na ngozi ambao wanaweza kusoma kwenye shule za kawaida walemavu wa kuona,kusikia na akili wanahitaji shule maalum zenye walimu maalum waliopata mafunzo ya kufundisha walemavu wa aina hiyo pia wanahitaji vifaa maalum vya kufundishia kama vitabu vya nukta nundu,miwani ya kusomea na fimbo za kutembelea.

Pamoja na serikali kutenga shule maalum za kufundishia walemavu hao lakini bado shule hizo hazina walimu wabobezi wa kufundishia walemavu wa akili,kuona na kusikia.

Tarehe 19 August 2021 nilitembelea shule ya msingi Mlandizi iliyopo halmashauri ya wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani ambayo ina kitengo cha kufundishia walemavu aina ya viziwi na akili na ndiyo shule pekee kwenye halmashauri hiyo yenye kitengo cha walemavu niligundua watoto wenye ulemavu wanakutana na changamoto nyingi zinazokwamisha ndoto zao za kupata elimu bora shule hiyo haina walimu wa kutosha na haina vitabu vya kutosha vya nukta nundu kwa ajili ya kufundishia walemavu wasioona watoto pia wanatoka maeneo ya mbali kwenda shuleni na watoto hawa wengi wanatoka kwenye kaya masikini ambazo hazina uwezo wa kuwapeleka kila siku shuleni.

Nini kifanyike?

Ujenzi wa mabweni

Shule zote zenye vitengo vya walemavu ziwe na mabweni ya kulala ili wanafunzi wenye ulemavu wawe wanalala shuleni badala ya kutembea umbali mrefu kila siku kwenda shuleni.Si sahihi mtoto mwenye ulemavu wa akili,kusikia au kuona atembee umbali mrefu kwenda shule kwa sababu ya changamoto za njiani.Pia umbali huu unasababisha wazazi wapate uvivu wa kuwaandikisha shule watoto wa aina hii.

Kuwepo na vifaa vya kufundishia walemavu
Ali Salum mkazi wa Kibaha aliwahi kusoma shule ya msingi Kilosa ambayo ni maalum kwa wanafunzi wasioona na wale wenye uoni hafifu anasema uhaba wa vifaa vya kufundishia kama mashine ya nukta nundu,vitabu vilivyoandikwa kwa nukta nundu na vyenye maandishi makubwa ni kikwazo kikubwa cha mafanikio ya elimu kwa wanafunzi wasioona na wale wenye uoni hafifu"uhaba wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia inachangia pia kwa mwalimu kumfanya ufundishaji wake kuwa mdogo"alisema Salum .Vifaa muhimu vya kufundishia kwa wanafunzi wasioona au wenye uoni hafifu ni kama mashine ya nukta nundu ambayo ni muwasiliano wa herufi kwa njia inayoshikika au kutambulika kwa vidole ambapo herufi na namba au hata noti za muziki na alama za kisayansi zinachorwa kiasi kwamba mtu asiyeona au mwenye uoni hafifu anaweza kutambua na kusoma kama kawaida.

Pia kukosa miwani maalum inayokuza herufi nayo ni kikwazo kwani wanafunzi wengi wanatoka kwenye kaya masikini hivyo hushindwa kuwanunulia watoto wao miwani .

Wazazi wenye watoto wenye ulemavu wawajibike kikamilifu
Serikali na wadau wengine watoe elimu kwa wazazi wenye watoto wenye ulemavu kuacha kuwafungia ndani na badala yake wawapeleke shule pia baadhi ya wazazi hawajui kama kuna shule maalum za kufundisha watoto wenye ulemavu.Neema Steven mkazi wa Visiga wilayani Kibaha alimpeleka mtoto wake Rehema Boniface mwenye ulemavu wa kusikia kwenye shule ya kawaida ambayo haikuwa na mwalimu hata mmoja anayejua lugha ya alama na hivyo kusababisha Rehema kutokupata elimu bora kwani alichanganywa na wanafunzi wa kawaida na maendeleo yake darasani yalikuwa mabaya alikuwa wa mwisho kwenye darasa lao na hivyo wanafunzi wenzake walikuwa wanamdhihaki mara kwa mara pia walimu walikuwa wanamgombeza kwa sababu ya kushindwa kuelewa haraka.Hali hiyo ilimfanya Rehema aichukie sana elimu aliona shule ni kama sehemu ya kutweza utu wake.Rehema alimaliza darasa la saba mwaka 2019 yeye peke yake ndiye hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari mpaka leo Rehema hataki kusikia kuhusu kusoma.

Nilifanya pia mahojiano na bi. Aneth Gerana mwanzilishi wa taasisi ya Furaha ya wanawake wajasiliamali viziwi Tanzania (FUWAVITA) yeye alishauri wazazi wa watoto wasiosikia wajifunze lugha ya alama kwa sababu nao wana nafasi kubwa katika makuzi na maendeleo ya watoto wao.Wanapoelewana na watoto wao kimawasiliano ni rahisi kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya watoto wao na rahisi pia kuwasaidia.

Walimu wanaofundisha walemavu wa kuona,kusikia na akili wawe waliobobea
Mwenyekiti wa Chama cha viziwi mkoa wa Pwani na mjumbe wa bodi ya Chama cha viziwi Tanzania (CHAVITA) Adam Shabani anasema pamoja na uwepo wa shule zenye vitengo maalum vya kufundisha walemavu lakini walimu waliopo wanashindwa kufikia matamanio ya watoto hao kutokana na sababu zifuatazo;

Walimu wengi wa viziwi wamesoma kinadharia zaidi kuliko vitendo na hivyo lugha ya alama hawaiwezi.Watoto viziwi wanatumia lugha ya alama hivyo mawasiliano kati ya walimu na wanafunzi yanakuwa magumu wengine hata alama za msingi tu wanashindwa .

Walimu wengi wa elimu maalum hawana moyo wa kuwatumikia watoto hao kutokana na kukosa motisha, mshahara mdogo na hakuna marupurupu yoyote.

Shabani aliongeza kuwa walimu wa elimu maalum wanapangiwa vipindi vingi kwenye madarasa mengine ya wanafunzi wa kawaida hivyo wanakosa kabisa muda wa kufundisha watoto wenye ulemavu ambao wanahitaji muda mrefu ili waweze kuelewa.

Shabani anasema CHAVITA mkoa wa Pwani imejaribu kutoa ushauri kwa idara inayohusika bila mafanikio baadhi ya mambo waliyowahi kushauri ni pamoja na kuongeza vitengo vya elimu maalum wilayani Kibaha,kuongeza walimu wenye uwezo na moyo wa kujitolea.Pia kutoa motisha kwa walimu wa elimu maalum,walimu wa elimu maalum wasipangiwe madarasa mengine wabaki wanawasaidia watoto hao tu.

Pia alishauri kampeni ya uandikishwaji darasa la kwanza na madarasa ya awali kwa watoto wenye ulemavu ifanyike.

Pia kunaitajika takwimu za watoto walemavu waliopo mitaani ili kuweza kuwafikia kirahisi.
Shabani alimalizia kwa kusema pia walitoa ushauri kuanzishwa kwa vitengo vya elimu maalum katika shule za sekondari ili watoto wanaofaulu kwenda sekondari waweze kuhudumiwa na kusoma ndani ya wilaya yao kwani watoto wengi wanaomaliza shule za msingi hushindwa kwenda kusoma kwenye shule za mbali nje ya wilaya kutokana na uchumi duni wa wazazi na hivyo kuishia njiani.

Ni wajibu wa wadau wote wa elimu kusaidia juhudi za makusudi kuokoa kundi hili la watoto wenye ulemavu ili nao waweze kupata elimu bora kwa manufaa yao wenyewe pamoja na jamii zao.Kwani elimu ni ufunguo wa maisha,sasa fikiria mtu mwenye matatizo ya kuona,kusikia na akili ananyimwa ufunguo wa maisha.

Karibuni kwa mjadala na kupiga kura.
 
Upvote 8
Miaka ya 2000 nilikuwa nasoma pamoja na wanafunzi viziwi na mabubu,kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne shule iliyokuwa mchanganyiko yenye wanafunzi zaidi ya 500 lakini ilikuwa na mwalimu mmoja tu aliyekua anajua lugha ya alama hali iliyokuwa inasababisha wanafunzi wengin wawe wakalimani wa wenzao kwa kifupi matokeo ya viziwi yalikuwa mabaya sana.
 
Kama hakuna walimu wa kutosha waliobobea kufundisha walemavu ni miujiza kutegemea walemavu hao kufaulu kwenye masomo yao.
 
Serikali ilianzisha vitabu vya maandishi makubwa na nukta nundu huo mpango sijui kama unaendelea na sijui viliwafikia watu wangapi wenye uhitaji.
 
Prof Ndalichako ana matatizo
 
Vmf
 
Kuna suala la stigma, kwa kiswahili niite kunyanyapaa, utakuta wazazi wanawaficha watoto wao wenye ulemavu hasa mtindio wa ubongo ndani hawataki hata kuwatoa nje. Hiki kwangu naona ni kikwazo namba moja kinachosababisha wenye ulemavu kukosa elimu bora kama ulivyoandika.

Pakishatolewa elimu ya kutosha kuhusu hilo tatizo kwenye vyombo vya habari, wazazi wakaamka hasa maeneo ya vijijini ambao wengine wanaamini ulemavu ni sawa na kuleta mikosi kwenye familia, wengi watakuwa tayari kupeleka watoto wao shuleni.

Baada ya hapo, serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, watengeneze mazingira yatakayowezesha wenye ulemavu wapate elimu bora ikiwa ni pamoja na uwepo wa vifaa vya kutosha vya kufundishia, hasa maeneo ya vijijini.

Hapa shule binafsi au taasisi, na watu binafsi wachajiwe kodi ndogo zikiingiza vifaa vya kufundishia walemavu ili kuipunguzia mzigo serikali kutoa elimu peke yake, kwa kufanya hayo naamini tutapiga hatua fulani kwenye kumaliza tatizo la ukosefu wa elimu kwa wenye ulemavu.
 
mimi siafiki kulala bwenini,wana complex needs itakua ngumu/complicated kukaa bwenini, wakae kwa wazazi wao,sema nahisi zijengwe shule nyingi zaidi , au shule zote ziwe na facilities zao, kukiwa na shule nyingi zenye kuwa include moja itasaidia ku create awareness ya mambo ya ulemavu and second itawa motivate wazazi kupeleka watoto wao wenye ulemavu shuleni,
 
Zipo shule za hao watoto mfano Uhuru mchanganyiko ipo Dsm, kule sifahamu kama wanalala, lakini jirani na ninapoishi (Dsm) ipo shule nyingine ya watoto wa aina hiyo wao hurudi nyumbani, but tayari kuna mabweni yamejengwa kwa ajili yao nadhani muda sio mrefu watahamia.Naona kama kuanzisha mabweni kwa ajili yao ndio mpango uliopo.

Kuhusu facilities zote kwa wakati mmoja ni ngumu, lakini huwa wanaongeza taratibu kulingana na mahitaji yanayojitokeza, tatizo la mambo ya serikali ni kuchukua muda kwa jambo husika kutatuliwa mpaka budget ipitishwe, hii ni changamoto.
 
Zipo shule za hao watoto mfano Uhuru mchanganyiko ipo Dsm, kule sifahamu kama wanalala, lakini jirani na ninapoishi (Dsm) ipo shule nyingine ya watoto wa aina hiyo wao hurudi nyumbani, but tayari kuna mabweni yamejengwa kwa ajili yao nadhani muda sio mrefu watahamia.

Kuhusu facilities zote kwa wakati mmoja ni ngumu,lakini huwa wanaongeza taratibu kulingana na mahitaji yanayojitokeza, tatizo la mambo ya serikali ni kuchukua muda kwa jambo husika kutatuliwa mpaka budget ipitishwe, hii ni changamoto.

Sawa Mkuu, ila mimi sidhani hii ya kuongeza facilities kulingana na mahitaji yanavyojitokeza iko sawa, mahitaji yapo siku zote ni wao kuweka vitu/policies ndipo watu watakapojitokeza, kimuundo wazazi wakiona evidence serikali inatambua umuhimu wa elimu kwa vijana wao (walemavu) kwa kuwajengea shule nyingi zaidi, watafeel supported na hivyo kuja foward kuchukua hizo opportunities,.............

Kuhusu kukaa bwenini kwa vijana wenye varying complex needs mimi sishauri ingawa ni opportunity for some....
 
Mahitaji yapo lakini hutofautiana kulingana na sehemu, mfano idadi ya watoto itaenda sambamba na uwepo wa walimu wa kukidhi mahitaji yao, wakiwa wachache walimu watakuwa wachache pia, lakini kadri watakavyoongezeka kulingana na mwamko wa wazazi na ndivyo mahitaji ya walimu yatakavyongezeka.

Issues nyingine kama vyumba vya madarasa, na vifaa vya kufundishia navyo vitaongezeka kulingana na idadi ya wanafunzi.
 
mmnhh haya bwana, wangefanya kila wilaya kuna shule mbili za walemavu ungeshangaa muitikio, inashangaza shule za walemavu ndio zinaangalia mahitaji kwanza kama yapo, wakati shule za kawaida zipo kila kona,huu ni muendelezo wa unyanyapaji kwa walemavu
 
Idadi yao ni wachache ukilinganisha na wasio walemavu, kama pangekuwa na "same proportion" hapo ingebidi ziende kwa style ya shule za kata.
 
Prof Ndalichako ana matatizo
Tatizo wenye mamlaka ya kutatua matatatizo ya walemavu siyo walemavu na inawezekana hawana ndugu mwenye ulemavu kwahiyo hawajui changamoto wanazokutana nazo wanafunzi wenye ulemavu na inakuwa ngumu kuwasaidia kutatua matatatizo hayo.Kuna waziri mlemavu anashughulikia walemavu kwenye Ofisi ya waziri mkuu lakini mchango wake hauonekani.
 
Elimu ni moja ya haki za msingi kwa kila mtoto wa Kitanzania bila kujali mtoto huyo ni mlemavu au la.Pamoja na sera na mikakati ya kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi na wale wa kidato cha kwanza hadi cha nne lakini elimu inayotolewa kwa watoto walemavu hasa wale wa kuona,akili na kusikia bado hauridhishi.

Tofauti na walemavu wengine kama wale wa viungo na ngozi ambao wanaweza kusoma kwenye shule za kawaida walemavu wa kuona,kusikia na akili wanahitaji shule maalum zenye walimu maalum waliopata mafunzo ya kufundisha walemavu wa aina hiyo pia wanahitaji vifaa maalum vya kufundishia kama vitabu vya nukta nundu,miwani ya kusomea na fimbo za kutembelea.

Pamoja na serikali kutenga shule maalum za kufundishia walemavu hao lakini bado shule hizo hazina walimu wabobezi wa kufundishia walemavu wa akili,kuona na kusikia.

Tarehe 19 August 2021 nilitembelea shule ya msingi Mlandizi iliyopo halmashauri ya wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani ambayo ina kitengo cha kufundishia walemavu aina ya viziwi na akili na ndiyo shule pekee kwenye halmashauri hiyo yenye kitengo cha walemavu niligundua watoto wenye ulemavu wanakutana na changamoto nyingi zinazokwamisha ndoto zao za kupata elimu bora shule hiyo haina walimu wa kutosha na haina vitabu vya kutosha vya nukta nundu kwa ajili ya kufundishia walemavu wasioona watoto pia wanatoka maeneo ya mbali kwenda shuleni na watoto hawa wengi wanatoka kwenye kaya masikini ambazo hazina uwezo wa kuwapeleka kila siku shuleni.

Nini kifanyike?

Ujenzi wa mabweni

Shule zote zenye vitengo vya walemavu ziwe na mabweni ya kulala ili wanafunzi wenye ulemavu wawe wanalala shuleni badala ya kutembea umbali mrefu kila siku kwenda shuleni.Si sahihi mtoto mwenye ulemavu wa akili,kusikia au kuona atembee umbali mrefu kwenda shule kwa sababu ya changamoto za njiani.Pia umbali huu unasababisha wazazi wapate uvivu wa kuwaandikisha shule watoto wa aina hii.

Kuwepo na vifaa vya kufundishia walemavu
Ali Salum mkazi wa Kibaha aliwahi kusoma shule ya msingi Kilosa ambayo ni maalum kwa wanafunzi wasioona na wale wenye uoni hafifu anasema uhaba wa vifaa vya kufundishia kama mashine ya nukta nundu,vitabu vilivyoandikwa kwa nukta nundu na vyenye maandishi makubwa ni kikwazo kikubwa cha mafanikio ya elimu kwa wanafunzi wasioona na wale wenye uoni hafifu"uhaba wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia inachangia pia kwa mwalimu kumfanya ufundishaji wake kuwa mdogo"alisema Salum .Vifaa muhimu vya kufundishia kwa wanafunzi wasioona au wenye uoni hafifu ni kama mashine ya nukta nundu ambayo ni muwasiliano wa herufi kwa njia inayoshikika au kutambulika kwa vidole ambapo herufi na namba au hata noti za muziki na alama za kisayansi zinachorwa kiasi kwamba mtu asiyeona au mwenye uoni hafifu anaweza kutambua na kusoma kama kawaida.

Pia kukosa miwani maalum inayokuza herufi nayo ni kikwazo kwani wanafunzi wengi wanatoka kwenye kaya masikini hivyo hushindwa kuwanunulia watoto wao miwani .

Wazazi wenye watoto wenye ulemavu wawajibike kikamilifu
Serikali na wadau wengine watoe elimu kwa wazazi wenye watoto wenye ulemavu kuacha kuwafungia ndani na badala yake wawapeleke shule pia baadhi ya wazazi hawajui kama kuna shule maalum za kufundisha watoto wenye ulemavu.Neema Steven mkazi wa Visiga wilayani Kibaha alimpeleka mtoto wake Rehema Boniface mwenye ulemavu wa kusikia kwenye shule ya kawaida ambayo haikuwa na mwalimu hata mmoja anayejua lugha ya alama na hivyo kusababisha Rehema kutokupata elimu bora kwani alichanganywa na wanafunzi wa kawaida na maendeleo yake darasani yalikuwa mabaya alikuwa wa mwisho kwenye darasa lao na hivyo wanafunzi wenzake walikuwa wanamdhihaki mara kwa mara pia walimu walikuwa wanamgombeza kwa sababu ya kushindwa kuelewa haraka.Hali hiyo ilimfanya Rehema aichukie sana elimu aliona shule ni kama sehemu ya kutweza utu wake.Rehema alimaliza darasa la saba mwaka 2019 yeye peke yake ndiye hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari mpaka leo Rehema hataki kusikia kuhusu kusoma.

Nilifanya pia mahojiano na bi. Aneth Gerana mwanzilishi wa taasisi ya Furaha ya wanawake wajasiliamali viziwi Tanzania (FUWAVITA) yeye alishauri wazazi wa watoto wasiosikia wajifunze lugha ya alama kwa sababu nao wana nafasi kubwa katika makuzi na maendeleo ya watoto wao.Wanapoelewana na watoto wao kimawasiliano ni rahisi kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya watoto wao na rahisi pia kuwasaidia.

Walimu wanaofundisha walemavu wa kuona,kusikia na akili wawe waliobobea
Mwenyekiti wa Chama cha viziwi mkoa wa Pwani na mjumbe wa bodi ya Chama cha viziwi Tanzania (CHAVITA) Adam Shabani anasema pamoja na uwepo wa shule zenye vitengo maalum vya kufundisha walemavu lakini walimu waliopo wanashindwa kufikia matamanio ya watoto hao kutokana na sababu zifuatazo;

Walimu wengi wa viziwi wamesoma kinadharia zaidi kuliko vitendo na hivyo lugha ya alama hawaiwezi.Watoto viziwi wanatumia lugha ya alama hivyo mawasiliano kati ya walimu na wanafunzi yanakuwa magumu wengine hata alama za msingi tu wanashindwa .

Walimu wengi wa elimu maalum hawana moyo wa kuwatumikia watoto hao kutokana na kukosa motisha, mshahara mdogo na hakuna marupurupu yoyote.

Shabani aliongeza kuwa walimu wa elimu maalum wanapangiwa vipindi vingi kwenye madarasa mengine ya wanafunzi wa kawaida hivyo wanakosa kabisa muda wa kufundisha watoto wenye ulemavu ambao wanahitaji muda mrefu ili waweze kuelewa.

Shabani anasema CHAVITA mkoa wa Pwani imejaribu kutoa ushauri kwa idara inayohusika bila mafanikio baadhi ya mambo waliyowahi kushauri ni pamoja na kuongeza vitengo vya elimu maalum wilayani Kibaha,kuongeza walimu wenye uwezo na moyo wa kujitolea.Pia kutoa motisha kwa walimu wa elimu maalum,walimu wa elimu maalum wasipangiwe madarasa mengine wabaki wanawasaidia watoto hao tu.

Pia alishauri kampeni ya uandikishwaji darasa la kwanza na madarasa ya awali kwa watoto wenye ulemavu ifanyike.

Pia kunaitajika takwimu za watoto walemavu waliopo mitaani ili kuweza kuwafikia kirahisi.
Shabani alimalizia kwa kusema pia walitoa ushauri kuanzishwa kwa vitengo vya elimu maalum katika shule za sekondari ili watoto wanaofaulu kwenda sekondari waweze kuhudumiwa na kusoma ndani ya wilaya yao kwani watoto wengi wanaomaliza shule za msingi hushindwa kwenda kusoma kwenye shule za mbali nje ya wilaya kutokana na uchumi duni wa wazazi na hivyo kuishia njiani.

Ni wajibu wa wadau wote wa elimu kusaidia juhudi za makusudi kuokoa kundi hili la watoto wenye ulemavu ili nao waweze kupata elimu bora kwa manufaa yao wenyewe pamoja na jamii zao.Kwani elimu ni ufunguo wa maisha,sasa fikiria mtu mwenye matatizo ya kuona,kusikia na akili ananyimwa ufunguo wa maisha.

Karibuni kwa mjadala na kupiga kura.
Umeupiga mwingi safi sana
 
Mchango wako mzuri sana.

Back
Top Bottom