Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
HATUA ZANGU CHACHE PEMBENI YA ABDILATIF ABDALLA, UINGEREZA, UJERUMANI NA KENYA
Abdilatif Abdallah alipokuwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam tukionana kwa mbali labda kwa kuwa hapakuwa na kitu cha kutuunganisha.
Abdilatif ni katika wale watu ambao unakutananae siku moja na huachaninae kamwe hata kama mnatenganishwa na maelfu ya kilomita.
Nakumbuka Abdilatif wakati wa gazeti la Africa Events miaka ya 1980.
Gazeti hili likichapwa London na lilikuja kuwa gazeti maarufu sana Tanzania tukilingoja kwa hamu kila mwezi.
Ndani ya gazeti hili kulikuwa na makala zilizohusu Tanzania na khasa Zanzibar zilizowavutia wasomaji wengi sana na nyakati zile kusoma habari zinazokwenda nje ya zile zilizokuwa zikichapwa na magazeti ya ndani ya Uhuru, Mzalendo na Daily News ilikuwa ikitupa raha na burudani ya aina yake.
Uwanja huu wa uandishi ulitawaliwa na Abdulrahman Babu, Ahmed Rajab, Ahmed Saleh Yahya, Mohamed Mlamali Adam kwa kuwataja wachache ninaowakumbuka.
Nami mara moja moja nikiandika na halikadhalika Hamza Njozi.
Nilipofika London kwa mara ya kwanza na kuwatembelea hawa ndugu zangu Banner Street zilipokuwa ofisi za Africa Events sikuwa mgeni sana, kulikuwa na mengi ya kuzungumza na nilikuwa na kazi kubwa ya kueleza jinsi Rais Ali Hassan Mwinyi alivyokuwa anashambuliwa hata na magazeti ya chama chake na gazeri la serikali yake pale ofisini.
Tukiendelea na mazungumzo yetu tukiwa hoteli za Wapakistani tukila biriani.
Nakumbuka siku moja niko Cardiff marehemu Ahmed Saleh Yahya alinipigia simu akiwa ofisini kwake London akanieleza kuwa amepokea makala kutoka Dar es Salaam ambayo ni nzuri kupita kiasi akasema kuwa inaelekea mwandishi ana elimu kubwa sana, akaniuliza kama namfahamu Hamza Njozi.
Waandishi hawa walilinyanyua juu sana gazeti hili.
Abdilatif ana historia kubwa na gazeti hili hadi lilipoacha kuchapwa katika mwaka wa 1994.
Kuna watu Tanzania hawakulipenda sana gazeti hili na lilipofunga shughuli zake naamini walishusha pumzi.
Miaka ikapita mingi nikakutana na Abdilatif Berlin, Ujerumani, akanilialika nyumbani kwake Hamburg.
Ukiwa na Abdilatif mtu unajihisi uko darasani unasomeshwa.
Nasoma nikiwa na Abdilatif nyumbani kwake Humburg, nasoma nikiwa na yeye kwenye gari yake, nasoma tukiwa kwenye treni tunakwenda mjini.
Mwisho wa yote haya kwangu ni nini?
Mwisho nimekusanya hazina ambayo nisingeweza kuipata mahali popote na katika maktaba yoyote duniani.
Sasa baada ya kujua haya yote nilifanya nini?
Nilimuomba aandike kumbukumbu zake.
Nilikuwa na Abdilatif Mombasa mwaka jana kwenye mkutano Fort Jesus na muda mrefu tukawa pamoja hadi mjini na iko siku tukaalikwa chakula cha mchana mimi na yeye nyumbani kwa Prof. Mohamed Khalil.
Mtu hupati fursa kama hizi kila siku na jana yake mimi, Abdilatif na Prof. Khalil tulikuwa nyumbani kwa kaka yake Abdilatif, Sheikh Abdilah Nasir.
Sheikh Abdilah Nasir ana mengi katika historia ya Kenya na historia ya uchapaji vitabu.
Kuna wakati alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Oxford University Press Nairobi na alihariri tafsiri ya Mwalimu Nyerere ya William Shakespeare, ‘’Julius Caesar.’’
Utacheka, utaburudika kumsikiliza Sheikh Abdilah Nasir katika yote aliyokutananayo katika maisha kama mwalimu kisha kama mwanasiasa wakati wa kupigania uhuru wa Kenya.
Abdilatif kaona haya yote kwa macho yake akiwa na Sheikh Abdilah Nasir.
Sheikh Abdilah Nasir alikuwa mwalimu wa mtoto mdogo Salim Abdallah ‘’Sal Davis’’ mwimbaji kutoka Mombasa aliyetia fora Ulaya katika miaka ya 1960 akiwa kijana mdogo wa miaka 18 akiimba katika club za Soho London.
Sal Davis ana historia ya pekee katika wanamuziki wa Afrika ya Mashariki.
Nimefika Soho mara moja na sikurejea.
Sal Davis ni mtoto wa Shariff Abdallah Salim aliyekuwa mjumbe wa Legico kwa zaidi ya miaka 30 wakati wa ukoloni.
Unatamani usifike wakati wa kuaga.
Picha: Abdilatif na Mwandishi ofisi za Africa Events, London 1991, Abdilatif Abdallah, Ahmed Rajab na Oginga Odinga, Zanzibar 1993 na Abdilatif na Prof. Mohamed Khalil Mombasa 2020.