Hatua zilizochukuliwa na Serikali kudhibiti mfumuko wa bei nchini

Hatua zilizochukuliwa na Serikali kudhibiti mfumuko wa bei nchini

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
204
Reaction score
231
Tathmini zinaonyesha kwamba kuna uhimilivu mkubwa wa bei kwa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini, huku hatua kadhaa zikichukuliwa na serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Samia Suluhu kupunguza athari zitokanazo na kupanda kwake kwa wananchi.

Serikali ya awamu ya sita imefanya jitihada kubwa za kuweka mazingira rafiki ya ufanyaji biashara nchini, kwa kuchukua hatua mbalimbali katika kudhibiti ongezeko la bei za bidhaa ikiwemo udhibiti wa upandishwaji holela wa bei.

Hatu zilizochukuliwa na serikali ni pamoja na :
  1. kuimarisha uzalishaji wa ndani wa bidhaa ili kupunguza utegemezi wa kuagiza mahitaji muhimu kama vile vyakula kutoka nje ya nchi.
  2. Kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa wazalishaji wa ndani wa mafuta ya kupikia yaliyosafishwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa lengo la kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa hiyo nchini.
  3. Kuondoa VAT kwa wazalishaji wa mbole kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kuwapunguzia wakulima gharama wazalishaji wa ndani wa unga wa ngano na kuleta unafuu wa bei katika soko la ndani.
  4. Serikali imepunguza kiwango cha ushuru wa forodha kutoka asilimia 35 hadi asilimia 10 kwa waagizaji wa ngano ili kuwapunguzia gharama wazalishaji wa ndani wa unga wa ngano na kuleta unafuu wa bei katika soko la ndani.
Lengo la kuchukua hatua hizo ni kumlinda mlaji kwa kuhakikisha anapata bidhaa bora kwa bei stahiki na kuzuia upandishwaji holela wa bei za bidhaa na kuchukua hatua za kisheria kwa yeyote atakayepandisha bei za bidhaa bila kuzingatia gharama halisi za uzalishaji au uingizaji nchini wa bidhaa husika.
 
-kwa mtazamo wako mlaji anapata bidhaa kwa bei stahiki kwa wakati huu hasa mafuta ya kula, nafaka na vyakula vingine?

-Unaweza kutoa mfano wa mtu au kampuni iliyochukuliwa hatua kwa kupandisha bei za bidhaa mbalimbali tunazotumia?

-Unawezaje kusema bidhaa zinauzwa kwa bei himilivu wakati bei ya mafuta ya petrol bado ipo juu hali inayosababisha kupanda kwa gharama za usafirishaji wa ama mazao kutoka mashambani kwemda kwenye masoko na kutoka kwenye masoko kwemda kwa walaji? Hali kadhalika gharama za usafirishaji wa bidhaa kutoka viwandani kwenda kwa walaji?

Hiki ulichoandika ni nadharia tu hasa linapokuja swala la maisha halisi,
Tunaweza kusema kwamba lipo kundi la watu wachache linalonufaika na initiative za serikali kuliko kundi kubwa la watanzania maskini ambao ni wavumilivu au hawana msemaji!

Hivi unajua kwamba miezi mitatu iliyopita ndizi mbichi tatu ziliuzwa 500 sasa hivi ni tatu 1000/=

Na watu hawana namna wanaadjust na kukaa kimya kwani hakuna wa kuwasemea sababu wasemaji na watunga sera ndio wanufaika wa hizo relief za serikali?
 
maumivu kila kona

kwa walotoa fedha kwenye ATM/bank kuanzia tar 1 /7/2022 hadi leo, banks zimeanza kukusanya tozo za serikali.
mshahara unakatwa kodi
ukitoa fedha kwa mifumo iliyopo unakatwa tozo
ukinunua vitu dai risiti - unakatwa kodi
ni muhimu ukafwatilia yanayofanyika kwenye account yako ili kuepuka malalamiko ya baadae.
 
maumivu kila kona

kwa walotoa fedha kwenye ATM/bank kuanzia tar 1 /7/2022 hadi leo, banks zimeanza kukusanya tozo za serikali.

ni muhimu ukafwatilia yanayofanyika kwenye account yako ili kuepuka malalamiko ya baadae.
Na hii imefanywa kimya kimya kwa Hiyo ninwatu wachache wameweza kugundua mabadiliko hayo na tangazo la waziri halikuwafikia wananchi! Sasa serikali inaendeshwa kwa Siri katika suala la kukusanya Kodi!
 
-kwa mtazamo wako mlaji anapata bidhaa kwa bei stahiki kwa wakati huu hasa mafuta ya kula, nafaka na vyakula vingine...
Mkuu asipokuelewa hapa atakuwa ana shida au ni chawa kama chawa....
 
Na hii imefanywa kimya kimya kwa Hiyo ninwatu wachache wameweza kugundua mabadiliko hayo na tangazo la waziri halikuwafikia wananchi! Sasa serikali inaendeshwa kwa Siri katika suala la kukusanya Kodi!
Unapokea SMS " .... ndugu XXXX kiasi cha fedha Tsh XXX kimetolewa kutoka katika account yako inayoishia na 0000. Kama hutambui mwamala huu piga namba 0000XXX. Kwa maelezo zaidi.

ukute ulishapangia budget hahaaaaaa .... unahisi maumivu fulani iviii
 
Nilishapigwa hii kama laki na nusu, kufuatilia kujua kulikoni nikakuta tozo mfululizo kwenye bank statement.....bongolala sasa ni wendo wa kukamuliwa kila pahala...
 
Mkuu asipokuelewa hapa atakuwa ana shida au ni chawa kama chawa....
Hawa ni watu wanatafuta kuonekana na watawala kwa njia ya kuwasifia na kudhani kuwa wanauelemisha umma juu ya utendaji wa serikali, ilihali ikiwa mambo ya hovyo yanaonekana mambo mazuri hayahitaji kunadiwa yataonekana yenyewe!
 
Back
Top Bottom