Hatuajiri wanawake kuonyesha sura, ATCL wamjibu mbunge CCM

Makanyaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2007
Posts
11,129
Reaction score
7,321
Wakati mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Husna Mwilima akisema wahudumu wa ndege za ATCL hawana mvuto kwa wateja, shirika hilo limesema haliwachagui kwa ajili ya kuonyesha sura 3.

“Hatuchagui wanawake kwa ajili ya kuwapeleka kuonyesha uzuri kuna vigezo lazima tuwapime uelewa. Lazima kujua wana uwezo upi wa kufuatilia mafunzo watakayopewa ili watoe huduma inayotakiwa kwa wateja wetu na si sura,” alisema Ladislaus Matindi, mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Awali jana bungeni mjini Dodoma wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo mwaka 2020/2021, Mwilima aliwaponda wahudumu wa ATCL kuwa hawana mvuto.

Chanzo: Mwananchi
 
Haa😀😁😂😃😄😅
Sura Hata Mbuzi Anayo!!!!
Ccm Hoyee
 
Mara ya mwisho Huyo mama kupanda hizo ndege ilikua lini..asijekuwa anazungumzia ATCL ya zamani. Na huo mvuto anakutaka yeye anao?
 
Wakati mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Husna Mwilima akisema wahudumu wa ndege za ATCL hawana mvuto kwa wateja, shirika hilo limesema haliwachagui kwa ajili ya kuonyesha sura 3.

“Hatuchagui wanawake kwa ajili ya kuwapeleka kuonyesha uzuri kuna vigezo lazima tuwapime uelewa. Lazima kujua wana uwezo upi wa kufuatilia mafunzo watakayopewa ili watoe huduma inayotakiwa kwa wateja wetu na si sura,” alisema Ladislaus Matindi, mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Awali jana bungeni mjini Dodoma wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo mwaka 2020/2021, Mwilima aliwaponda wahudumu wa ATCL kuwa hawana mvuto.

Chanzo: Mwananchi
Sasa huyo mbunge yeye Ana uzuri gani kenge huyo
 
He he! Mbona sisi wanaume hatujalalamika..? Achunguzwe huyo mama
 
Angesema hawana customer care, kwakweli nimetumia ATCL mara nyingi ila wahudumu wale hawana smile kwa wateja na Sauti zaunyenyekevu, unaweza ukafikiri niwahitimu wa JKT, Naomba wajifunze zaidi customer care bila hivo Biashara itakua ngumu akipatikana mpizani mzuri wa hiyo biashara
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom