"Hatuangalii sura mtu tunataka umeme upatikane katika Bwawa la Mwalimu Nyerere" Mbunge Manyanya

"Hatuangalii sura mtu tunataka umeme upatikane katika Bwawa la Mwalimu Nyerere" Mbunge Manyanya

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
MBUNGE wa Jimbo la Nyasa, Injinia Stella Martin Manyanya ameweka wazi kutoridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere na kuweza wazi msimamo wake kuwa Tanzania lazima tujitambue na hatutaangalia sura ya mtu bali umeme upatikane Bwawa la Mwalimu Nyerere.

"Na hapa nauzungumzia Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, Tanzania lazima tujitambue kuna wakati tunaweza tukawa tuna malengo makubwa mazuri ambayo yametupa heshima katika nchi yetu halafu baadae kwa sababu moja ama nyingine kwa sababu labda uongozi mmoja haupo umekuja uongozi mwingine watu wengine wanaweza kufikia kujaribu tukuchezea kwa kutushauri tofauti ili tushindwe kwenda kule tulikotaka kwenda"

"Kwa sababu Mheshimiwa Rais amedhamiria na ametangaza hadharani nawaomba Wizara ya Nishati tafadhalini tusimuangushe Mh Rais wetu tuhakikishe mradi huu wote kwa pamoja tunashirikiana timu iliyoko sasa na hata ile iliyokuwa mwanzo kama kuna jambo ambalo wao wanalifahamu mshirikiane kuhakikisha kwamba tunaenda vizuri sisi hatuangalii sura mtu tunaangalia umeme upatikane katika Bwawa la Mwalimu Nyerere" amesema Stella Manyanya alipozungumza bungeni.


 
Eti uongozi mmoja haupo umekuja mwingine
Mnachekesha
Kama kila awamu itakuja na lake sasa mnafanya nini hapo
Na hamtaelewana maisha mpaka kuwe na katiba nzuri na muwe mnaendeleza kila jambo bila kumpa nguvu zote Rais
 
MBUNGE wa Jimbo la Nyasa, Injinia Stella Martin Manyanya ameweka wazi kutoridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere na kuweza wazi msimamo wake kuwa Tanzania lazima tujitambue na hatutaangalia sura ya mtu bali umeme upatikane Bwawa la Mwalimu Nyerere...
Huyu ajengewe sanamu amekaa kuwa chawa
 
Kuna mdau alisema chama kile Ni ukoo wa panya
 
Back
Top Bottom