Hatufanyi vizuri kwenye Utalii wa Picha

Hatufanyi vizuri kwenye Utalii wa Picha

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Sijui kama kuna mtu hapa amewahi kuombea Mgeni (mtalii) kibali cha kupiga picha akaona ugumu uliopo?

Kiujumla taratibu zilizopo sio rafiki (hazipo wazi) yaani kuna wizara sijui ngapi zinahusika hivyo kupata kibali bila maarifa ni ndoto ya mchana kwani unaweza kutumia miezi nk hivyo mgeni hawezi hata kupanga safari
Ushauri

1. Naona kama baadhi ya taratibu zinazofuatwa zimepitwa na wakati hivyo ziangaliwe upya.

2. Kuwe na one stop Centre ya kuomba Vibali vya Picha hasa hizi za kupiga kwenye mbuga za wanyama.

3. Kuwe na muda ambao Lazima muombaji apewe majibu kuwa amepata au amekosa (mfano: siku 7)

4. Kuwe na uwazi na urahisi Mfano: Form ya kujaza online inayoelekeza vielelezo vya kuambatanisha. Sio hii ya sasa ambapo wengi huishia njiani na wachache kufanikiwa kwa maarifa.

5. Kwa mtazamo wangu, taratibu zilizopo ni rahisi zaidi kupitisha watu wasiokuwa na sifa kwa sababu ya maarifa.

Mwisho: Taribu zikiwa tayari zitangazwe wazi wazi pengine kupitia vyama mbalimbali vya utalii TATO nk ili wadau wazifahamu.
 
Back
Top Bottom